Ushuhuda wangu: Mimi ni muathirika wa HIV (HIV Positive)

Pole. Na pia naweza sema wewe hujielewi. Unasema mtu ana upendo wa dhati kwako alafu anakuambukiza ukimwi kwa makusudi. Huyo jamaa ana roho mba sana na hafai kuishi kwenye jamii. Hivi mtu unajua kabisa unaumwa alafu unaenda kumuambukiza mwenzio kwa makusudi kabisa. Dah binadamu tunatofautiana kwa kweli
 
Pole sana. Hii para pia imenistua sana (si kwa sababu ni mmoja wao). Ina maana vijana wa humu wengi umeshawaonja? Unasema "WAnajijua".

Lakini asante kwa ushuhuda wako, naamini wengi watajifunza kitu....sio wadogozako tu...hata watu wazima pia. Nashauri uendeleze kidogo ushuhuda wako kwa kutushirikisha namna unavyomudu maisha katika hali Hiyo na changamoto unazopitia? Unakosa nini kwa kuwa na hali hiyo ya maambukizi? Kwa mfano, una mtoto/watoto, nk? Maisha yako kwa ujumla.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…