Ushuhuda wangu: Mimi ni muathirika wa HIV (HIV Positive)

Ushuhuda wangu: Mimi ni muathirika wa HIV (HIV Positive)

Kaka imenibidi nirudi nisome kwa utulivu hii comment yako! Vipi umeniona huko kwenye list? Tuambizane Kaka nikamtafute Paroko nianze kutubu
Kaka wewe kausha tu.
Kuna watu wengi sana wanatembea na waathirika ila hawaathiriki.
 
Mwee kwahiyo na yule prof anaekusomesha nje ya nchi nae umeshamgawia ?
First, let me declare kwamba mimi ni member wa muda mrefu humu JamiiForums na nimependa kuja nah hii ID mpya ili kuweza kuficha utambulisho wangu wa hapo mwanzo, ili kuepeuka mambo kadhaa kutoka kwa member ambao nimebahatika kuonana/kukutana nao.

Naitwa Priscallia (si jina langu halisi) na umri wa miaka 29 na ni mtumishi wa serikali katika mamlaka fulani hapo nyumbani Tanzania kwa sasa nipo nchi X nikisomea shahada ya juu ya mambo fulani fualni pia ni muathirika wa virusi vya UKIMWI.

Anyway, kwa ufupi ilikuwa ni mwezi wa 6 mwaka 2014 kipindi nipo chuo mwaka wa mwisho ambapo nilianza kuhisi homa na mafua makali kwa muda wa wiki moja baadae nilienda hospitalini kufanya vipimo na baada ya vipimo ikagundulika niko na typhoid ambapo nilipewa dawa nikaanza dose na baada ya kumaliza zile dalili zote zilipotea.

Ila baada ya kumaliza UE mwezi mmoja baadae nilipokuwa field ile hali ya mafua na homa zikanirudia na safari hii kilichonishtua ni kuongezeka kwa baadhi ya dalili kama vile kupoteza hamu ya kula, kutapika na baadhi ya rashes katika baadhi ya sehemu ya mwili wangu, niliamua kutumia baadhi ya dawa na tubes kwa muda wa wiki kadhaa lakni sikuona mabadiliko yoyote nikaamua kwenda hospitali ili kuchukua vipimo upya, nakumbuka ilikuwa ni mwezi wa saba (7) mwishoni kuelekea wa nane (8) baada ya kuonana na daktari na kumueleza nilivyokuwa najisikia (consultation) daktari akaniandikia baadhi ya vipimo kama vile choo, mkojo na damu baada ya muda fulani majibu yalipotoka yote yalisoma negative.

Baada ya majibu hayo, dokta akataka kunichukua vipimo vya HIV na akaniuliza kwa upole “Kama nilishawahi kuchukua vipimo vya ukimwi hapo kabla?” nikamjibu kwa kujiamni kuwa nilipima mwaka mmoja nyuma baada ya kuachana na aliekuwa mpenzi wangu na majibu yalikuwa Negative.

Akaniuliza tena kwa sasa upo katika mahusiano nikamjibu kwa ufasaha kuwa "NDIO" nikaenda mbali zaidi nikamwambia mahusiano haya yana miezi mitano (5) sasa na mwanzo tulipoingia katika mahusiano tulikuwa tunatumia kinga ila tulipozoeana na baada ya mwenzangu kunihakikishia kuwa yuko sawa (HIV negative) tukajikuta tukishiriki tendo bila kutumia kinga kama ilivyokuwa hapo mwanzo.

Baada ya mazungumzo hayo na daktari nikakubali kuchukuliwa damu kwa mara nyingine ili kuweza kujua status yangu ya HIV, baada ya muda majibu yalirudi nikaitwa kwenda kuonana na daktari nilipokuwa naingia daktari alikuwa akinitazama kwa huruma na hakuonesha ule uchangamfu wa mwanzo nilipoingia ofisini kwake. Katika mazungumzo akaniambia kwa upole kuwa anashindwa afikishe vipi majibu yaliyoko mezani kwake kwangu hapo mapigo ya moyo yalibadilika na hofu ilianza kuingia ndani yangu, ndipo hapo akaniambia ya kwamba majibu yamerudi na kwa masikitiko makumbwa vipimo vinaonesha mimi ni muathirika wa virusi vya ukimwi.

Hakika ile siku ilikuwa mbaya sana katika maisha yangu, I go into shock. I did'nt think of anything rather than I’m going to die nililia sana siku ile, dokta alinimbeleleza sana siku ile akaniambia nisihohofu/nisijali kila kitu kitakuwa sawa na kwamba huo sio mwiosho wa maisha yangu. Siku ile nilijiuliza maswali mengi kichwani mwangu kwanini mimi? Kwanini imetokea kwangu? Tena kwa wakati huu ambapo nilikuwa ndio nimemaliza masomo yangu ya shahada nilijisika vibaya mno.

Baada ya hapo nilimpigia simu yule mwanaume ambaye pia alikuwa ni mwalimu wangu huku nikilia nikamwambia kila kitu, alionekana kusikitika/kushangaa na muda mwingi alikuwa akijichanganya sana katika mazungumzo na muda mwingine alikuwa hana cha kunijibu na kubaki kimya.

Nilimblock kwa muda wa miezi kadhaa hapo sasa nikawa nawaza nitawaambia nini wazazi wangu nikawa sina jinsi maana wao ndio familia yangu, baada ya siku 5 niliwambia kuwa kuna jambo nataka niwaeleze hivyo wakawa nashauku ya kujua baada ya chakula cha usiku nilivunja ukimya nikawaambia sikuwa na jinsi ya kuficha tena kuhusu hali yangu. Nakumbuka mama yangu na mdogo wangu wa kike walilia sana ila nashukuru hapo baadae waliamua kukubaliana na hali halisi ingawa Baba na kaka yangu walisikitika sana ila mwisho wa siku walinisamehe pia.

Ilinichukua muda sana kukubaliana na hali ile but mwisho wa siku ilibidi iwe hivyo. Because I knew now I am not going to die, in fact in pretty good health, more stronger, confidence and having a good life. Kufupisha story ni kwamba baadae, tuliwasiliana na huyo mwalimu wangu alikiri kuwa yeye ndio aliniambukiza nilimsamehe na nilikuja kugundua kuwa hata mke wake alimpteza kwa ugonjwa huo baada ya kuugua kwa muda mrefu pia na nikiri wazi alikuwa ana upendo wa dhati kwangu maana baada ya kuhitimu masomo yangu alinitafutia kazi katika mamlaka fulani ambapo nipo nafanya kazi hadi leo hii.

Mwisho, ningependa kuwaasa wadogo zangu waliopo vyuoni hasa hawa waliopo mwaka wa kwanza wasiwe wepesi kurubuniwa maana hawa ndio wahanga wakubwa maana mara nyingi ugeni wa chuo na exposure zinawachanganya sana hawa wadogo zangu na mwisho wa siku huishia kufanya mapenzi bila kutumia mipira na hivyo hujikuta wakiharibu afya zao.

Pia na kwa wale dada zao waliopo mwaka wa pili na kuendelea pia muwe makini sana, najua wengi wenu huwa mnaishia kuingia katika mitego ya mahusiano na walimu wenu wa chuo,mkumbuke hawa ndio waathirika wakubwa hivyo mjitahidi sana kabla ya kukutana kimwili mhakikishe mnapima kwanza afya zenu na ikiwezekana mtumie mipira maana huwezi kumjua muathirika kwa kumuangalia kwa macho.

Lastly, kuna vijana baadhi nilikutana nao humu ndani they were good guys lakni niligundua wengi wao hawajali afya zao na wanaongozwa sana na sexual desire, maana unakuta mwanaume mko nae faragha baada ya mzunguko wa kwanza from nowhere anataka muende peku au katikati ya tendo anavua mpira kwa makusudi, wanajijua watakuwa mashahidi nilikuwa nawakatilia katukatu maana nilikuwa nawajali sana.

All in all ukimwi upo, mjitahidi mlinde afya zenu maana Afya ni mtaji. Ahsanteni niwatakie mchana mwema.

Priscallia.
 
Nilitaka Kutoa Poleee.... Ila nilivyosoma Comments za Wadau nimeona Huyu Dada ni MUONGO! Ametunga Story! Siku zote Mtu akiamua Ku declare kwamba Ni Muathirika Hawezi Kuficha Identity yake! Ila Jamii ijifunze na Ielemike kupitia Yeye! Lakini huyuu Amekuwa Sio Mkweli

ID Yake mpya kawa Member 9/11 Tarehe 11/11 kapandisha post yupo anakula maisha na Profesor wa Chuo mpaka ajenge ndio atamuacha! Sijajua hapo kati kati post zake, Leo Tarehe 28/11 Kapost kuwa ni Muathirika baada ya kupata shika kwa muda fulanii Nikipiga hesababu toka tarehe 11/11 alipo post kuwa anakula maisha na Profesa hadi leo ni siku 17 sawa na Wiki 2 Ambazo kwa Maelezo yake ndio Alikuwa anaumwa typhoid! Kwanini uliwahauri wenzio wadate na wanaume wenye pesaa na Wazee kama Wewe unavyodate na Profesa?

Huu ni Uongo mkubwa hivyo hata story yako haielimishi Tena! kwasababu ya Uongo!

UKIMWI upo lakini usiwatishe Vijana wa Humu waliokutana na Wadada Wa humu na Kula Tunda kimasihara kwa kuanza kuogopa kudhani ni Wewe! Kumbei Sio na Nimuongo.........

Nawasilisha
 
Daah nimekuja hapa kwa niaba ya wadau wakubwa wa Uzi wa kula kimasihara ,machimbo,nilmtumia nauli sjui kama atafika ,biashara za badoo,nk niseme tu hatujapendezwa na huu Uzi wa kitisho unaoendelea hapa jamvini nimepende kuwahakikishia wanachama wenzangu wasivunjike moyo huu ugonjwa siku hizi haupo

Mwisho nitoe rahi kwa wana matukio yaendelee kwa wingi nyuzi zetu pendwa zizidi kujaa wana wapata mafunzo mbalimbali ila kinga muhimu


Daah ila kwa nzia Leo nimeamini ubaharia sio ishu wala nini salamu za majozi ziwaendee Mendez wote wazamiaji piemu mshaskia mwenyewe amesema alikuwa na I'd nyengine na mabaharia wamesababisha najua kuna watu wanaumiza kichwa sjui atakuwa ni nani
 
ESPRESSO COFFEE, pWewe ndio hujaelewa!

Kwa mujibu wa mleta mada aliyemwambukiza ukimwi ni huyo profesa wake wa chuo na wadau wameshaunganusha dot hapa kwamba huyo profesa anajulikana ni mwathirika alifiwa na Mkewe!

Mimi nikiangalia huu uzi na ule alikuwa a nashangaa wenzie kutembea na wasio na hela naona hii stori ina ukweli 100%
 
ID aliyotumia kwenye uzi ule wa kujimwambafai ni hii hii.

Worse enough atakuwa amemgawia ngwengwe na yule prof, prof nae kwa uzembe atagawia wanafunzi wake wakati wakimpatia Coursework allowance, wakirudi likizo vijana nao wanapigana vikumbo kula vipapatio vyao.

Baadae finance wa tuition fee nae anapewa kutoka home mama watoto home anapelekewa.

Maisha matamu sana ila ni mafupinsana
Kaandika ana I'd mbili usijipe moyo kusema nawe haupo kwani I'd nyingine huijui.
 
Pale unapogundua ulimla dada wa watu peku!
1574446518_1574446518-picsay.jpeg
 
Thank you dear. Na imani watu watajifunza kitu na watakuwa makini katika mahusiano yao
Umakini unatakiwa uanzie kwako af ndio ushauri wengine.

-Sijaelewa nia yako ya kutembea na wana jf kadhaa humu ilikua nini?
Angekua mmoja ts ok, ila wengi inamaanisha kitu kibaya sana. Kwanini unashidwa kujizuia na kua na mahusiano na mtu mmoja?
Yani unawatega alafu unawashauri wawe makini wasitegeke[emoji1][emoji1]
 
Back
Top Bottom