Ushuhuda wangu: Mimi ni muathirika wa HIV (HIV Positive)

Ushuhuda wangu: Mimi ni muathirika wa HIV (HIV Positive)

Huu uzi baada ya kusoma kma page mbili na kupitia replies ikanibidi niende kugoogle dalili za UKIMWI nikaona sielewi, nikasepa moja kwa moja hospital, nikapima. Baada ya majibu ndio narudi sasa kifua mbele kuendelea kusoma kwa aman. Huu ugonjwa atar sana
 
Moderator hili jina LA CONTROLA sikuliandika kwenye comment yangu, nani kaliweka? Why are keeping on changing comments za watu? Moderator sifurahishwi na hili
uko sahihi sana,niliona comment yako uliandika uliishia "jamaa wa sua anajiita Black T"

sasa hivi naona Moderator wamenipachika hapo mimi,kwamba ili iweje?

hivi nyie Moderator mna tumia akili za nn? vichwa vyenu ni vipi eti?

Fanyeni editing sawa ila kwann muingize ID za watu hv hamuoni ni uchonganishi huuu?

Maxence Melo angalia hawa vijana wako ki ukweli wanaboa,na kwa mwendooo huu sijui kama tutafika.
 
Maisha aya bwana. Kuomba Mungu tu atujaalie mwisho mwema. RIP dogo G. Ulitimiza wajibu wako katika kulinda afya yako, chanjo ya homa ya ini, gheto box la ndom mixer na vilainishi (yaani full equiped).

Ila ukaja poteza maisha ukiwa unatembea pembezoni mwa barabara (baada ya gari kuhama njia), nawaza tu na yawezekana kabisa ulikuwa unatoka kula dem na na ndom ulitumia. Pumzika kwa aman mdogo wangu, One Life
 
Nilijiuliza Je kwani huyu Black T ndio Controla? Last time ilikua ni manengelo nae yalimkuta haya
walivyo mandezi badala warekebishe yapo tu yamekalisha yanatoa macho ka matunguri ya mshana.

wachawi humu ndani hadi Staff ma mods wamejazana mi nasemaga.
 
HIV sio kitu cha kunyoosheana vidole.
Haya maambukizi hayaangalii nani mzinifu au nani mwaminifu....
Kana watu hapa hawajawahi chepuka toka kwenye mahusiano yao lakini wameletewa na wenza wao ambao hawakua waaminifu na kuna vijana wengi pia wamezaliwa wakiwa HIV+ wako mashuleni na vyuoni wanaanzisha mahusiano na unapokutana nao unaweza dhani umepata kitu kipya kabisa kumbe maambukizi yapo.
Tukumbuke pia tunaweza tukawa hatuna maambukizi leo lakini usiku wa kuamkia kesho au kesho kutwa tukawa tumeshayapata sababu hatuwezi kumchunga mtu mzima au ukampiga kufuli asichepuke.
Kwa tulio negative tumshukuru Mungu kwa hilo, tuendelee kujilinda na tusiwanyanyapae waathirika...
na tulio positive tujitahidi kuwalinda wenzetu pamoja na kutunza afya zetu
Kama alivyosema mtoa mada kila mmoja ajitahidi kuitunza afya yake
 
Back
Top Bottom