Ushuhuda wangu: Mimi ni muathirika wa HIV (HIV Positive)

Ushuhuda wangu: Mimi ni muathirika wa HIV (HIV Positive)

Pole
FB_IMG_15745402615752609.jpeg
 
Asante kwa neno Dada yangu mzuri zuri, Mungu akupe furaha ya moyo wako
 
Kutumia condom ni sawa na kuogelea kwenye bwawa lenye mamba mmoja possibility ya kuliwa ni kubwa ila kutokutumia condom ni sawa na kuogelea kwenye bwawa lenye mamba wengi possibility ya kuliwa ni kubwa zaidi.
 
First, let me declare kwamba mimi ni member wa muda mrefu humu JamiiForums na nimependa kuja nah hii ID mpya ili kuweza kuficha utambulisho wangu wa hapo mwanzo, ili kuepeuka mambo kadhaa kutoka kwa member ambao nimebahatika kuonana/kukutana nao.

Naitwa Priscallia (si jina langu halisi) na umri wa miaka 29 na ni mtumishi wa serikali katika mamlaka fulani hapo nyumbani Tanzania kwa sasa nipo nchi X nikisomea shahada ya juu ya mambo fulani fualni pia ni muathirika wa virusi vya UKIMWI.

Anyway, kwa ufupi ilikuwa ni mwezi wa 6 mwaka 2014 kipindi nipo chuo mwaka wa mwisho ambapo nilianza kuhisi homa na mafua makali kwa muda wa wiki moja baadae nilienda hospitalini kufanya vipimo na baada ya vipimo ikagundulika niko na typhoid ambapo nilipewa dawa nikaanza dose na baada ya kumaliza zile dalili zote zilipotea.

Ila baada ya kumaliza UE mwezi mmoja baadae nilipokuwa field ile hali ya mafua na homa zikanirudia na safari hii kilichonishtua ni kuongezeka kwa baadhi ya dalili kama vile kupoteza hamu ya kula, kutapika na baadhi ya rashes katika baadhi ya sehemu ya mwili wangu, niliamua kutumia baadhi ya dawa na tubes kwa muda wa wiki kadhaa lakni sikuona mabadiliko yoyote nikaamua kwenda hospitali ili kuchukua vipimo upya, nakumbuka ilikuwa ni mwezi wa saba (7) mwishoni kuelekea wa nane (8) baada ya kuonana na daktari na kumueleza nilivyokuwa najisikia (consultation) daktari akaniandikia baadhi ya vipimo kama vile choo, mkojo na damu baada ya muda fulani majibu yalipotoka yote yalisoma negative.

Baada ya majibu hayo, dokta akataka kunichukua vipimo vya HIV na akaniuliza kwa upole “Kama nilishawahi kuchukua vipimo vya ukimwi hapo kabla?” nikamjibu kwa kujiamni kuwa nilipima mwaka mmoja nyuma baada ya kuachana na aliekuwa mpenzi wangu na majibu yalikuwa Negative.

Akaniuliza tena kwa sasa upo katika mahusiano nikamjibu kwa ufasaha kuwa "NDIO" nikaenda mbali zaidi nikamwambia mahusiano haya yana miezi mitano (5) sasa na mwanzo tulipoingia katika mahusiano tulikuwa tunatumia kinga ila tulipozoeana na baada ya mwenzangu kunihakikishia kuwa yuko sawa (HIV negative) tukajikuta tukishiriki tendo bila kutumia kinga kama ilivyokuwa hapo mwanzo.

Baada ya mazungumzo hayo na daktari nikakubali kuchukuliwa damu kwa mara nyingine ili kuweza kujua status yangu ya HIV, baada ya muda majibu yalirudi nikaitwa kwenda kuonana na daktari nilipokuwa naingia daktari alikuwa akinitazama kwa huruma na hakuonesha ule uchangamfu wa mwanzo nilipoingia ofisini kwake. Katika mazungumzo akaniambia kwa upole kuwa anashindwa afikishe vipi majibu yaliyoko mezani kwake kwangu hapo mapigo ya moyo yalibadilika na hofu ilianza kuingia ndani yangu, ndipo hapo akaniambia ya kwamba majibu yamerudi na kwa masikitiko makumbwa vipimo vinaonesha mimi ni muathirika wa virusi vya ukimwi.

Hakika ile siku ilikuwa mbaya sana katika maisha yangu, I go into shock. I did'nt think of anything rather than I’m going to die nililia sana siku ile, dokta alinimbeleleza sana siku ile akaniambia nisihohofu/nisijali kila kitu kitakuwa sawa na kwamba huo sio mwiosho wa maisha yangu. Siku ile nilijiuliza maswali mengi kichwani mwangu kwanini mimi? Kwanini imetokea kwangu? Tena kwa wakati huu ambapo nilikuwa ndio nimemaliza masomo yangu ya shahada nilijisika vibaya mno.

Baada ya hapo nilimpigia simu yule mwanaume ambaye pia alikuwa ni mwalimu wangu huku nikilia nikamwambia kila kitu, alionekana kusikitika/kushangaa na muda mwingi alikuwa akijichanganya sana katika mazungumzo na muda mwingine alikuwa hana cha kunijibu na kubaki kimya.

Nilimblock kwa muda wa miezi kadhaa hapo sasa nikawa nawaza nitawaambia nini wazazi wangu nikawa sina jinsi maana wao ndio familia yangu, baada ya siku 5 niliwambia kuwa kuna jambo nataka niwaeleze hivyo wakawa nashauku ya kujua baada ya chakula cha usiku nilivunja ukimya nikawaambia sikuwa na jinsi ya kuficha tena kuhusu hali yangu. Nakumbuka mama yangu na mdogo wangu wa kike walilia sana ila nashukuru hapo baadae waliamua kukubaliana na hali halisi ingawa Baba na kaka yangu walisikitika sana ila mwisho wa siku walinisamehe pia.

Ilinichukua muda sana kukubaliana na hali ile but mwisho wa siku ilibidi iwe hivyo. Because I knew now I am not going to die, in fact in pretty good health, more stronger, confidence and having a good life. Kufupisha story ni kwamba baadae, tuliwasiliana na huyo mwalimu wangu alikiri kuwa yeye ndio aliniambukiza nilimsamehe na nilikuja kugundua kuwa hata mke wake alimpteza kwa ugonjwa huo baada ya kuugua kwa muda mrefu pia na nikiri wazi alikuwa ana upendo wa dhati kwangu maana baada ya kuhitimu masomo yangu alinitafutia kazi katika mamlaka fulani ambapo nipo nafanya kazi hadi leo hii.

Mwisho, ningependa kuwaasa wadogo zangu waliopo vyuoni hasa hawa waliopo mwaka wa kwanza wasiwe wepesi kurubuniwa maana hawa ndio wahanga wakubwa maana mara nyingi ugeni wa chuo na exposure zinawachanganya sana hawa wadogo zangu na mwisho wa siku huishia kufanya mapenzi bila kutumia mipira na hivyo hujikuta wakiharibu afya zao.

Pia na kwa wale dada zao waliopo mwaka wa pili na kuendelea pia muwe makini sana, najua wengi wenu huwa mnaishia kuingia katika mitego ya mahusiano na walimu wenu wa chuo,mkumbuke hawa ndio waathirika wakubwa hivyo mjitahidi sana kabla ya kukutana kimwili mhakikishe mnapima kwanza afya zenu na ikiwezekana mtumie mipira maana huwezi kumjua muathirika kwa kumuangalia kwa macho.

Lastly, kuna vijana baadhi nilikutana nao humu ndani they were good guys lakni niligundua wengi wao hawajali afya zao na wanaongozwa sana na sexual desire, maana unakuta mwanaume mko nae faragha baada ya mzunguko wa kwanza from nowhere anataka muende peku au katikati ya tendo anavua mpira kwa makusudi, wanajijua watakuwa mashahidi nilikuwa nawakatilia katukatu maana nilikuwa nawajali sana.

All in all ukimwi upo, mjitahidi mlinde afya zenu maana Afya ni mtaji. Ahsanteni niwatakie mchana mwema.

Priscallia.

[/QUOTEduh, hatari sana, kama ndio hiv, na matunda yanaliwa kimasiahara
 
kulingana na watafiti kwa sasa Tanzania kila siku watu 200 wanaambukizwa HIV, Kwa maana hiyo siku unavyoshiriki moja kwa moja unaingia kwenye "Number of Sample Space" inabakia issue ya Probability tu...haijalishi unashiriki na nani unaweza kuambukiza au kuambukizwa bila kujijua sababu network ya haya mambo ni moja kati ya Complicated Unseen Network In The Word.
 
Its life my sister, nothing new, nothing strange, neither is there anything new under the sun, the wisest man who ever lived said so, Now back to your issue i really wonder why people get very or so scared of HIV while there are more serious and life thretening uncurable diseases in this universe, take the case of cancer, most people discover they have cancer when it has reached that stage where it can neither be controlled or cured, on the other hand HIV is controlable, even an israel universtity has came up with a vaccine ( tho its now on clinical tails) which will engulf the hiv virus, and that means this virus will not be able to mutate, or spread neither will they be able to infect the white blood cells, WHAT GOOD NEWS IS THAT TO OUR FELLOW HUMAN BEINGS WHO HAVE HIV VIRUS, and once you get this vaccine, you stay for 10 years, no taking of medication, after 10 years you take another vaccine, you stay for another 10 years no taking of medications and so on till the lord calls you home.so in my own personal opinion hiv is not such a threat, there are other illness that are a major threat more than hiv. i think the stigma cames in that hiv is associated with sex, nothing else, keep on keeping on dear girl, enjoy your weekend
 
Hivohivo na mimi Misca alitakaga kuniua jamani? mtoto yule mume wake anajua alikufa kwa ngoma na yeye ana ngoma ananifuata eti nimuoe kweli?

Yaani siku hiyo Mungu tu alinisimamia!

wadada /wa kaka msiusambaze ukimwi kwa maksudi ili kutukomesha, kwa sababu tu, tuna elimu na kazi nzuri!
 
Huyo Misca ni jina la aidii hapa jeiefu?
Hivohivo na mimi Misca alitakaga kuniua jamani? mtoto yule mume wake anajua alikufa kwa ngoma na yeye ana ngoma ananifuata eti nimuoe kweli?

Yaani siku hiyo Mungu tu alinisimamia!

wadada /wa kaka msiusambaze ukimwi kwa maksudi ili kutukomesha, kwa sababu tu, tuna elimu na kazi nzuri!
 
Back
Top Bottom