Tutor B
JF-Expert Member
- Jun 11, 2011
- 9,025
- 6,598
Hiyo gharama uliyotaja ni ya juu sana na haiwafanyi watanzania kudhubutu. Niliposoma ile post ya kuku 6 kukupatia kuku 200 nilivutiwa sana. Uwezo wa hao kuku nilikuwa nao; hivyo nilipowanunua nilitumia Tshs. 48,000/= kununua kuku, 30,000/= kununua sehemu ya kuku kushinda, 10,000/ kifaa cha maji na Tshs. 4,500/= kununua kifaa cha chakula. Sehemu ya kulala nilikuwa nawalaza jikoni. Chakula nilikuwa nanunua kila wiki nachanganya mwenyewe pale nyumbani.
Walipoongezeka kufikia 50, ndo nilijenga banda dogo mita 3 x 4 kwa ajili ya kulaza wale kuku wasiohatamia.
Hivyo sikubaliani na mtoa mada kuwa unahitaji mil 1.5 kuanza - HAPANA. Hicho ni kiasi kukubwa sana; unataka kuwaogopesha watu wasijaribu kufuga eti kwa sababu hawana hiyo pesa.