USHUHUDA: Watanzania tuwe wakweli juu ya ufugaji wa kuku

USHUHUDA: Watanzania tuwe wakweli juu ya ufugaji wa kuku

Tanzania kuna upotoshaji mkubwa sana, wengi wetu ni waongo waongo sana. Penye ukweli tunapindisha.

Ili ufuge kuku wa kienyeji, tena kwa banda la hali ya chini kabisa, ni lazima uwe na vitu vifuatavyo :-

(Kwa banda la mita 9 kwa mita 3)

1. Eneo la kutosha kwa ajili ya banda

2. Muda wa kutosha kuwahudumia kuku

3. Uwe na mtaji wa siyo chini ya Milioni 1.5 kwa ajili ya kujengea banda tu

Gharama ya fundi siyo chini ya laki 1.5 , mabati used siyo chini ya mabati 15 @ 8,000 TZS , matofali ya kuchoma 800 300 TZS, misumari ya bati 2 kg @ 5,000 TZS , Binding wire , bawaba , cement 12 bags , kufuli 1 @ 5,000 TZS , kitasa 1 @ 4,000, mbao ( 2 x 2 , 3 x 2 ) 800 Rft , mirunda 12 @ 5,000 TZS , Chicken mesh 1 Roller 80,000 TZS , Wavu mgumu 2 Rollers @ 12,000 , usafiri na mengineyo madogo madogo.

4. Uwe na walau laki 3 za kununua kuku wakubwa wanaokaribia kutaga

Ikumbukwe tu , kuku 1 ni kati ya TZS 10 - 15,000

Watanzania tuwe wakweli , tuache uongo na ushabiki wa vitu tusivyovijua kwa vitendo.
ndio zao hao mi nilishawishiwa kilimo kina lipa hasa cha muhogo kwa heka naweza uza kwa hasara milioni moja.....heeeeeh sasa naenda sokoni et heka laki mbili😡😡😡
 
Hahaaaa nilipewa dili la kufuga bata nikajenga banda nikanzungushia eneo langu chicken wire nikanunua bata km kumi nikaanza kuwalisha ebhana wakafika 80 nia yangu wafike 100 niuze ikaja mvua ikapiga ile mbaya sikua najua mvua na bata hazipatani walikufa bata km hamsin kumbuka hao nilikua nanunua gunia la pumba kila wiki plus cost za ujenzi wa banda nikajikuta nimebaki na bata wadogo 18 na wakubwa 12 nilishikwa na hacra nikawagawa tu.Sasa hivi nafuga kuku wa kienyeji siwazingatii kivile ila naona wamekubali nao km 32.Ufugaji bila kujipanga ni hasara na tafuta mtaalamu sio hao waongo wa kwenye mitandao akufundishe kabla ya kuanza ufugaji.
Bata wanakufa kisa mvua??? Hata kuku nao msimu mvua ukianza wanakufa balaaaaa... So fuga kwa akili ukiona masika yanakujaa Uzaaa mzeee...
 
Bata wanakufa kisa mvua??? Hata kuku nao msimu mvua ukianza wanakufa balaaaaa... So fuga kwa akili ukiona masika yanakujaa Uzaaa mzeee...
Me nilimwelewa maana nina wa fuga alikuwa Ana walaza kwenye banda lenye maji kipindi cha mvua kwa mchana maji ya mvua kwao sio mabaya Ila kama banda lake lina ingiza maji na kama hawana umri mkubwa wana kufa!
Uzuri wa bata hana magonjwa kama kuku kuku ni hatari haswa ukiwafuga kwenye eneo dogo!
 
Duh! Umesema kweli! Bata wanakula unaweza kuogopa. Unawajazia chombo ndoo ya Lita 20 bata 30 kwa siku hawashibi! Wanakula na kunya hapo hapo na maji kibao kuloweka midomo yao! Acha kabisa!!
Hahahahaha hatari Sana Hawa viumbe wangu wamefika mia na kitu hawali wana saga kama machine ya mahindi Bora bukini hawali Sana kama hawa wa kawaida!
Ila usiogope kuwa fuga mkuu me nina penda bata sababu hana Mambo ya kupewa dawa kama kuku!
IMG_20181118_112258.jpg

Hawa hawali Sana Ila siyo Ila hawa zaliani kama hawa wa kawaida!
 
Me nilimwelewa maana nina wa fuga alikuwa Ana walaza kwenye banda lenye maji kipindi cha mvua kwa mchana maji ya mvua kwao sio mabaya Ila kama banda lake lina ingiza maji na kama hawana umri mkubwa wana kufa!
Uzuri wa bata hana magonjwa kama kuku kuku ni hatari haswa ukiwafuga kwenye eneo dogo!
Aah kumbe sasa nae alizingua..Alidhani ni samaki wale au???[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hahahahaha hatari Sana Hawa viumbe wangu wamefika mia na kitu hawali wana saga kama machine ya mahindi Bora bukini hawali Sana kama hawa wa kawaida!
Ila usiogope kuwa fuga mkuu me nina penda bata sababu hana Mambo ya kupewa dawa kama kuku!View attachment 972929
Hawa hawali Sana Ila siyo Ila hawa zaliani kama hawa wa kawaida!
Hivi soko la bata lipo kweli???? maana duuh
 
Hiyo gharama uliyotaja .
Sawa kabisa. gharama ni kubwa mno.
Hata mimi kuku walikuwa wanakufa sana ila nimekuja kufahamu ukiwatibu vifaranga mapema kwa kinga hawafi, ingawa magonjwa yapo kwa kila mfugo yote. Mi natenganisha vifaranga na kinyesi chao kwa wiremesh. Nawapa joto kwa bulb. Mwezi sasa hakuna kifaranga aliyekufa.
Changamoto ninayopata ni sehenu ya kutagia wanagombania.

Nilichoona kinachowashinda wengi kuku wanataka kufuatiliwa na kuwajua. Mimi nikimwangalia kuku akitembea na ulaji wake na kinyesi naweza jua kuku mzima au mgonjwa.

Pili. Magonjwa ya virus kwenye kuku yanasumbua yanataka tiba mbadala za dukani mara nyingine hazifanyi kazi.
Kuku wanakufa lakini mara chache kuna paka na kenge n k nao wanataka kula kuku..

Kuku wanafugika, sasa kwasababu wengi mmekimbia kufuga, sisi ndio tunapata fursa nzuri ya kuoiga hela ndeeefu.
 
Hahahahaha hatari Sana Hawa viumbe wangu wamefika mia na kitu hawali wana saga kama machine ya mahindi Bora bukini hawali Sana kama hawa wa kawaida!
Ila usiogope kuwa fuga mkuu me nina penda bata sababu hana Mambo ya kupewa dawa kama kuku!View attachment 972929
Hawa hawali Sana Ila siyo Ila hawa zaliani kama hawa wa kawaida!
Mzee nikupe dume hao unipe jike mana hapa na jike moja dume mbili zinapanda hatari watamuua
 
Gharama za ufugaji kuku kwa kiasi kikubwa zinategemea mazingira ya unapofugia hao kuku wako.....

Kikubwa wanachokosea hawa Wahamasishaji wa hii miradi ni pale wanapozirahisisha changamoto za ufugaji zionekane rahisi rahisi sana kuliko uhalisia...na hapo ndipo wanapowafelisha watu wengi....
Mkuu inategemea mwezi wa 9/2018 nimetumia laki 5 kujenga banda lenye ukubwa wa 3*5M
Nikanunua kuku 5 jogoo 1 na tetea 4 kwa 67,000
Nikanunua chakula nikachanganya mwenyewe pumba debe 7 mashudu,dagaa, chokaa, mifupa tolat 48,000
Chanjo ya kideri 7elfu!
Mpaka sasa nina vifaranga 43 wana mwezi sasa.ninewanyanganya mama yao Nategemea mwezi wa1 2018 wataanza kutaga tena!
Ukisikiliza wanaopinga wanadhani garama za ujenzi zipo costant nchi nzima!!
Kuna amabo wana access ya kupata mabanzi... Pia wapo wenye accesa ya kupata used playwood so inategemea.

Unaweza kuanza hata kwa laki 2 tuu
 
Back
Top Bottom