USHUHUDA: Watanzania tuwe wakweli juu ya ufugaji wa kuku

Ex
Exactly ..
Inategemea eneo na mazingira husika
 
Kidogo sana niliwahi kutotolesha vyangu nilinunuwa incubator mkuu kuku zikanizingua nikahamia kwenye mabata!
Niulize tu mkuu!
Kuna mteja wangu kanunua mayai kwangu Sasa alikopeleka hayakutotolewa yote alivyomuuliza huyo mwenye mashine anasema Eti ukisafirisha mayai kiini kinachanganyika!

Hili ni kweli? maana sijawahi sikia hii kitu mkuu!

Au amempiga panga maana wengine yanatotolewa vizuri tu tena yote!
 
Mkuu kwa ninavyo faham kidogo sio lazima yawe yame tikiswa ndio yasi anguliwe !!
Inategemea pia ulikuwa umeya hifadhi vip mayai ya kuanguliwa yana hitaji uangalifu sana kwenye kuya tunza ukitaka yanguliwe 90%
Incubator zile tray zake inatakiwa zishafishwe na dawa kila baada ya kuanguliwa mayai! Pia hizo zako pia zinatakiwa kama ni za plastic inabidi uzisafishe na dawa kila unapotaka kuweka mayai kwa ajili ya kuangulia maana kuna bacteria mayai yanapata kutoka kwenye hizo tray kama zimetumika mda!
Kama ni za karatasi sio nzuri kuhifadhia mayai ya kuangulia kwa muda!
Maana hazi safishiki!
 
Shukran mkuu
 
Watotoreshaji wengi ni wezi wanaibia watu vifaranga na kuuza ukiwauliza wana visababu vya ajabu ajabu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
 
2.4 million banda tuu la kuku mkuu, πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ we jamaa umezingua,ufugaji wa kuku ni rahisi sana mazee, nimezaliwa nimekuta home wafugaji wa kuku,bata,ng'ombe ,mbuzi,kanga,njiwa,bata mzinga na kondoo , kuku wana faida ni kinoma, as long as unawajali,chanjo kwa wakati,wasikose chakula,PPIA YAPASA UWAPENDE KWANZA/UPENDE UNACHOKIFANYA,FAIDA BAADAYE SOON NATEGEMEA KURUDI NYUMBANI NKAANZE KUFUGA NA MIE MAANA MABANDA NI KAMA YOTE
 
Mkuu unipe hiyo elimu.
 
Kweli kuna gharama lakini hizi zako zimekuwa too theoretical..nyingi....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…