drginwey
Member
- Feb 23, 2017
- 11
- 8
Sasa hivi ukipita barabarani kuanzia mwanza mpaka Mtwara ni mabango ya CCM au Mama Samia yakielezea amefanya moja au mbili na pongezi kibao. Ziwe za kweli au uwongo zote zimepangiliwa njia nzima mithili ya maua kwenye misiba ya kishua.
Swali langu ni je, tunapata mapato yoyote kwenye mabango hayo?
Nani analipa ushuru wa mabango hayo ya kumtambulisha mtu ambaye tunamjua kana kwamba hajulikani? Inaumiza kuona watu wanalipishwa mabango yaliyopo kwenye biashara zao halafu tuna mabango ya propaganda ambazo hazieleweki wala hayaakisi uhalisia wa maisha ya Mtanzania wa kawaida.