Sasa hivi bei gani?Gari kutoka Zanzibar kwenda Bara, zimeongezewa ushuru maradufu... Ndugu zetu mnakusudia kuuwa biashara ya gari Zanzibar kama mulivyouwa biashara ya vitambaa?
Viongozi wetu mbona mpo kimya? Wapi tunaelekea?
Ikiwa nchi tofauti za Jumuiya ya Ulaya hazitwangani ushuru, iweje sisi nchi moja kuna ushuru wa kuuwa biashara?
kwa uchache Zanzibar kila gari moja huajiri watu angalau watatu, kuiuwa biashara hii kumefanya karibu nusu ya car importers nao waache kuzileta... Tanzania, hivi tunajenga au tunabomoa?
Gharama ya ushuru imeengezeka karibia 100% gari ambayo ungeliitoa kwa 2.5M juzi ilipigwa 5M!!!
Mamaaaaaa Impaler na Shark mko serious wakuu! Dah hii imekula kwangu sana kama kweli. Nimejikamua gari moja toka UK nikashauriwa niitolee Zanzibar than bara. Cost niliyoambiwa tu hapo awali kajasho kamenitoka sasa mwaniambia IMEONGEZWA!! :eek2:
Nafkiri nikishalitoa Zanzibar nihamie huku huko moja kwa moja niwe naliendesha huko huko!
Ila hawa wapumbavu hawawezi tu kuamka asubuhi na kujiamulia tu wanvyojiskia, na huwezi kuweka hio sheria wakati wengine gari zetu ziko melini!!
Hili li nchi bah! Wacha nilale mimi!!
masihara hayo mkuutra wanafanya hivyo ili kulinda viwanda vya magari vya hapa nchini kwani kwa kufanya hivyo watu mtanunua magari ambayo yanatengenezwa na viwanda vyetu vya tanzania, hutoagiza gari nje.
Alah! Hivi tuna viwanda vya magari?? Nimeshasahau.
Hakuna haja ya kulalamika. Mlipowataka wabara kuwa na paspoti kuja Zanzibar hamkujua mlikuwa mnaandaa nini. Heri hata wafanyabiashara toka Visiwani walitamalaki bara wangetozwa ushuru wa ziada kama experts. Pia wazanz wasingeruhusiwa kufanya biashara ya kimachinga ili waone faida ya kutaka wanachokitaka.
Gari kutoka Zanzibar kwenda Bara, zimeongezewa ushuru maradufu... Ndugu zetu mnakusudia kuuwa biashara ya gari Zanzibar kama mulivyouwa biashara ya vitambaa?