Ushuru wa magari kutoka Zanzibar kwenda Bara umeongezwa maradufu

Ushuru wa magari kutoka Zanzibar kwenda Bara umeongezwa maradufu

Impaler

Senior Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
163
Reaction score
75
Gari kutoka Zanzibar kwenda Bara, zimeongezewa ushuru maradufu... Ndugu zetu mnakusudia kuuwa biashara ya gari Zanzibar kama mulivyouwa biashara ya vitambaa?
Viongozi wetu mbona mpo kimya? Wapi tunaelekea?

Ikiwa nchi tofauti za Jumuiya ya Ulaya hazitwangani ushuru, iweje sisi nchi moja kuna ushuru wa kuuwa biashara?

kwa uchache Zanzibar kila gari moja huajiri watu angalau watatu, kuiuwa biashara hii kumefanya karibu nusu ya car importers nao waache kuzileta... Tanzania, hivi tunajenga au tunabomoa?
 
Hii haijakaa vyema kabisa.. na si suala la kulichukulia poa.
 
Gari kutoka Zanzibar kwenda Bara, zimeongezewa ushuru maradufu... Ndugu zetu mnakusudia kuuwa biashara ya gari Zanzibar kama mulivyouwa biashara ya vitambaa?
Viongozi wetu mbona mpo kimya? Wapi tunaelekea?

Ikiwa nchi tofauti za Jumuiya ya Ulaya hazitwangani ushuru, iweje sisi nchi moja kuna ushuru wa kuuwa biashara?

kwa uchache Zanzibar kila gari moja huajiri watu angalau watatu, kuiuwa biashara hii kumefanya karibu nusu ya car importers nao waache kuzileta... Tanzania, hivi tunajenga au tunabomoa?
Sasa hivi bei gani?
 
Gharama ya ushuru imeengezeka karibia 100% gari ambayo ungeliitoa kwa 2.5M juzi ilipigwa 5M!!!

We acha tu mkuu,
Juzi nimepigwa Altezza Kodi ya Tshs 3.7Million na hawa wezi sina hamu kabisa.
gari yenyewe nimeinunua zanzibar Tshs 10Million,
Wanadai wanakata tofauti, kumbe wizi mtupu.
Altezza from japan ina Kodi ya Tshs 4.1Mil, ya Zanzibar imelipiwa 1.4Mil, so should be at least tshs 2.7Mil.
Weka namba, wharf-age, Clearing na upuuzi mwengine imefikia mpaka 14.5Mil.
Imeniuma sana kwa kweli, maana gari yenyewe huko Zanzibar ilikua imetumika kama miezi miwili hivi.
Huu Muungano bora Ufe tu!!
Huu ni wizi wa mchana kweupe.
Yaani ni bora utoe gari Japan kuliko Zanzibar
 
TRA wanafanya hivyo ili kulinda viwanda vya magari vya hapa nchini kwani kwa kufanya hivyo watu mtanunua magari ambayo yanatengenezwa na viwanda vyetu vya Tanzania, hutoagiza gari nje.
Alah! hivi tuna viwanda vya magari?? nimeshasahau.
 
Mamaaaaaa Impaler na Shark mko serious wakuu! Dah hii imekula kwangu sana kama kweli. Nimejikamua gari moja toka UK nikashauriwa niitolee Zanzibar than bara. Cost niliyoambiwa tu hapo awali kajasho kamenitoka sasa mwaniambia IMEONGEZWA!! :eek2:
Nafkiri nikishalitoa Zanzibar nihamie huku huko moja kwa moja niwe naliendesha huko huko!
Ila hawa wapumbavu hawawezi tu kuamka asubuhi na kujiamulia tu wanvyojiskia, na huwezi kuweka hio sheria wakati wengine gari zetu ziko melini!!
Hili li nchi bah! Wacha nilale mimi!!
 
Hakuna haja ya kulalamika. Mlipowataka wabara kuwa na paspoti kuja Zanzibar hamkujua mlikuwa mnaandaa nini. Heri hata wafanyabiashara toka Visiwani walitamalaki bara wangetozwa ushuru wa ziada kama experts. Pia wazanz wasingeruhusiwa kufanya biashara ya kimachinga ili waone faida ya kutaka wanachokitaka.
 
Mpayukwaji kalale!! Huna mpya! Hii ni shida kitaifa!!! Kama umefilisika kimawazo... Kalale!

Justice Delayed Is Justice Denied
 
hivi muungano bado upo kweli? kwanini kuwe na utofauti mkubwa kwenye kodi? pia mnaofahamu naomba mnijuze kama huwa wanatoza kodi kutoa gari bara kupeleka zanzibar.
 
Muungano ulishajifia siku tele ndio maana mambo kodi kila upande kivyake vyake,wa zanzibar kama walikuwa wanalenga zaidi kuuza magari bara walie waje wafungue show rooms huku bara kama wanagtaka biashara za magari!
 
Kutoka bara kwenda Zanzibar hakuna kodi yeyote!!! Na hapo ndipo wanapochoka wengi!!!

Justice Delayed Is Justice Denied
 
Mamaaaaaa Impaler na Shark mko serious wakuu! Dah hii imekula kwangu sana kama kweli. Nimejikamua gari moja toka UK nikashauriwa niitolee Zanzibar than bara. Cost niliyoambiwa tu hapo awali kajasho kamenitoka sasa mwaniambia IMEONGEZWA!! :eek2:
Nafkiri nikishalitoa Zanzibar nihamie huku huko moja kwa moja niwe naliendesha huko huko!
Ila hawa wapumbavu hawawezi tu kuamka asubuhi na kujiamulia tu wanvyojiskia, na huwezi kuweka hio sheria wakati wengine gari zetu ziko melini!!
Hili li nchi bah! Wacha nilale mimi!!

Ila hawa jamaa wanakuwaga kama wana homa za vipindi mkuu Nyamgluu,
We liache kwanza Zanzibar kisha uwe unazungukia geti namba mbili kila mara kucheki upepo unaendaje!!
 
tra wanafanya hivyo ili kulinda viwanda vya magari vya hapa nchini kwani kwa kufanya hivyo watu mtanunua magari ambayo yanatengenezwa na viwanda vyetu vya tanzania, hutoagiza gari nje.
Alah! Hivi tuna viwanda vya magari?? Nimeshasahau.
masihara hayo mkuu
 
Hakuna haja ya kulalamika. Mlipowataka wabara kuwa na paspoti kuja Zanzibar hamkujua mlikuwa mnaandaa nini. Heri hata wafanyabiashara toka Visiwani walitamalaki bara wangetozwa ushuru wa ziada kama experts. Pia wazanz wasingeruhusiwa kufanya biashara ya kimachinga ili waone faida ya kutaka wanachokitaka.

nakuunga mkono mkuu.....

Zata hivyo tanganyika ilikuwa inapoteza kodi nyingi kwa mfumo wa zamani, heri wameongeza mkuu apate fedha za kusafiria nje ya nchi, ukizingatia znz ikikusanya kuke mapato wanatumia wenyewe ila tra mapato tugawane haiwezekani isee....
 
Zanzibar Airport ni watalii 4 katika 100 wanaopewa Visa ya kweli, wengine wanagongewa kamhuri cha karibu Zanzibar (sio Tanzania) na pesa direct inaingia mitini hapohapo.
 
Wakuu ,

Je ni kweli Zanzibar magari ya unazwa bei rahisi ukilinganisha , na bei ya Dar ?
 
hata bure unapata kule we nenda tu tena kabla ya uchaguzi wako kina yakheeeee wengi sana na kama utakuwa unatoka mombasa basi utarudi na kontena zima la motokaa
 
Gari kutoka Zanzibar kwenda Bara, zimeongezewa ushuru maradufu... Ndugu zetu mnakusudia kuuwa biashara ya gari Zanzibar kama mulivyouwa biashara ya vitambaa?
Viongozi wetu mbona mpo kimya? Wapi tunaelekea?

Ikiwa nchi tofauti za Jumuiya ya Ulaya hazitwangani ushuru, iweje sisi nchi moja kuna ushuru wa kuuwa biashara?

kwa uchache Zanzibar kila gari moja huajiri watu angalau watatu, kuiuwa biashara hii kumefanya karibu nusu ya car importers nao waache kuzileta... Tanzania, hivi tunajenga au tunabomoa?

Hili ni suala la kihistoria sasa. Nyie Watu wa Zanzibar mlisemwa tangu enzi za Nyerere. Yeye alisema Bara na Visiwani ni nchi moja, na ziko chini ya serikali moja. Hatuwezi kuwa na mifumo miwili ya kodi, kwamba gari ikiingizwa Zanzibar ilipiwe kodi kidogo, na ikija bara ilipiwe kodi kubwa. Nyie mlikataa katakata, mkijua kwamba bara wanaagiza sana magari hivyo mtakuwa mnaagiza magari toka nje na kuyauza bara.

Nyerere alichofanya, baada ya nyie kukataa mfumo mmoja wa kodi kwa Tanzania yote, ni kuagiza kwamba bidhaa kutoka Zanzibar zikija bara lazima zilipiwe ushuru ili kuweka usawaziko. Mkaanza kupiga kelele, ooh mnatuonea, kwa nini bidhaa moja itozwe kodi mara mbili wakati nchi ni moja Tanzania!

Ndipo Nyerere akawajibu kwamba mnakuwa kama mtoto mdogo – unambeba, anakunyea halafu yeye ndiye analia ukimweka chini baada ya kukunyea.
 
Back
Top Bottom