Raymanu KE
JF-Expert Member
- Jan 20, 2022
- 8,611
- 16,118
Salute comrades!
Hitmaker wa NIPENI MAUA YANGU, Roma Zimbabwe kupitia ukurasa wake wa Instagram amewausia vijana wa kiume wanaojiandaa kuoa kwamba wasikurupuke tu kufanya maamuzi ya kuoa bali wawafanyie wachumba wao " vetting" ya kutosha.
Roma amesema kabla hujamuoa huyo mchumba wako na kumfanya mkeo na mama ya watoto wako,Kwanza jiulize maswali muhimu yafuatayo;
👉Je, huyu mchumba wako ataweza kuwa mama Bora kwa watoto wako?
Ataweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo kama mama kwa watoto wenu?
👉Kwa mfano ikitokea siku ukapatwa na msala mzito utakaopelekea wewe kufungwa jela kwa miaka kadhaa,Je,huyo mkeo ataendelea kuwa mwaminifu kwako kwa kukutunzia tunda lako pamoja kulea watoto au ndo ataanza kuhanya hanya?
Au atakuwa anachepuka kisiri Siri ili angalau apate Cha kuwalisha watoto wenu akisubiria umalize kifungo?
👉Ukikumbwa na anguko la kiuchumi ukafilisika kabisa,je, huyo mkeo ataendelea kukupenda na kukutia moyo upambane mpaka pale utakapoinuka tena kiuchumi au ndo atakuacha upambane na umasikini wako?
Ukishajiuliza hayo maswali matatu hapo juu then unaweza kufanya tathmini yako ili ubaine Kama huyo unayetaka kumfanya mkeo anaweza shinda hayo majaribu endapo yatatokea.
Kijana usiangalie tu shape na sura ya mwanamke Kisha ukakurupuka kuoa, maana unaweza ukajutia uamuzi wako baadae.