Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,180
- 7,346
"Daktari nina maumivu makali ya tumbo, nahisi hivi vitakuwa vidonda vya tumbo kabisa"... Maelezo ya namna hii humkera daktari na inaweza kusababisha usipate huduma vizuri. Madaktari hawapendi kuelekezwa ugonjwa. Unachotakiwa kufanya ni kueleza dalili za matatizo yako ya kiafya.
Maumivu, uvimbe, kiungo kushindwa kufanya kazi... pia elezea ni kwa muda gani (usiogope kuambiwa kwanini hukuwa umeenda hospitali siku zote), elezea kwa ufasaha sehemu, upande na kama maumivu ni ya moja kwa moja au ya kuja na kupoa.
Unaweza pia kutoa historia ya watu wa famili yako, au watu wa karibu na wewe kama waliwahi kuwa na matatizo kama uliyo nayo. Lakini usikimbilie kutaja ugonjwa unaohisi kuwa unaumwa...