Usianzishe biashara wala kutafuta kazi kupitia waganga wa kienyeji

Usianzishe biashara wala kutafuta kazi kupitia waganga wa kienyeji

Natangaza maslahi yangu! Mimi sio mganga na sifanyi ushirikina tena!

Kati ya waganga wote wa kienyeji ni asililia kumi hivi kati ya mia moja ndio wakweli na kati ya hao wakweli ni asilimia 5 tu ndio wenye masharti nafuu na wanaoweza kukusaidia moja kwa moja..! Ishu ya kuwajua feki na wakweli tutaona huko mbele

Kwanza lazima tukubaliane kuwa ushirikina ni utumwa, na ushirikina ni masharti na vigezo..Na ushirikina ni kitu chenye kuhitaji update kila wakati.. Na waganga wengi ni wapigaji!

Pamoja na shida zako zote usijaribu kwenda huko kwenye ushirikina kutafuta 'assist' huko unaenda kufanya registration kwenye data base yao na hatimaye kuwa kwenye himaya yao. MAKINIKA!

Chochote kinachohusika na ajira ama biashara ukiachana na visomo vya kidini lazima kitahusisha damu. Automatically itakuwa damu ya mnyama hasa mbuzi na ng'ombe ama kuku.. Kwa uchache kabisa na kwa siri kubwa damu ya mtu itahusika.

Mnyama anayechinjwa kwa shughuli za ushirikina ni wazi analazimishwa kufa kabla ya muda wake wa kufa kutimia. Vita yake yoyote ya kiroho baada ya hapo utaibeba wewe.. Kwahiyo utakuwa na vita mbili ama zaidi ya kupigana.. Vita yako, vita ya kuku, vita ya mbuzi nknk.. Na hapa ndio siri ya side effect asiyokwambia mganga, Lakini lingjne ni hili... Yule mnyama aliyetumika kukutengenezea mambo yako ana ukomo wake wa kuwa, hivyo wakati wake wa kufa ukifika, kafara ulilotengenezewa nalo hufa rasmi..! Hapo ndio utaona mambo yako yanavyoanza kuyumba na hatimaye kuharibika kabisa

Lingine ni kwamba kuna wakati katika maisha mambo huenda mrama bila sababu yoyote ile..ni asili tu inafanya kazi, wewe kwa kuhofia kuwa tayari umeshapigwa na kitu kizito tena, utakimbilia kwa mtaalam wako tena, na yeye hata kama hakuna tatizo atalitengeneza na kukutisha sana. Juu ya yote kwakuwa tayari uko kwenye database zao kuna wakati huamua kukorofisha mambo ili tu umuendee ajione bingwa ama kuna kitu umtimizie

Mwishowe unakosa kabisa ladha ya maisha unafanya biashara lakini hutulii ni makafara kwa kwenda mbele, una kazi yako nzuri Lakini masharti ni kama yote unapata pesa Lakini huna furaha nazo.

Mganga naye ni binadamu akiamua kula bata hutengeneza tatizo kwakuwa kila mganga ni mchawi.. Pesa ya kutengeneza tatizo ndio huwa pesa ya starehe kwakuwa haimpi masharti kama ile pesa ya kilinge inayotokana na tatizo genuine!

Mwanzoni mwa biashara, ajira na hata mahusiano na miradi mingine epuka sana kuyanajisi na ishu za giza yasije yakaja kukutesa mbeleni, kwa kuwa kuingia huko ni rahisi sana lakini kutoka ni habari nyingine. Na ni shughuli pevu
So mnyama akichinjwa home anakufa kwa muda wake? Anayechinjwa kwenye kafara analazimishwa kufa kabla ya muda wake kutimia? Hatari sana hii logic yake. In short ushirikina ni dhambi.
 
Mshana Jr naomba nikuulize,
Mtu aliyechukuliwa msukule si inamaana hajafa kiroho na kimwili? Anaweza kurudishwa akawa kawaida?
Je ukifika wakati Wa Mungu kumchukua inakuaje?..

Jibu la hili swali ni la muhimu sana kaka, sijauliza kujifurahisha... Kuna mpuuzi Juzi kanywesha maji na akasomewa sijui nini huko na mgangaa kaanza kuropoka watu aliowachukua misukule.
 
So mnyama akichinjwa home anakufa kwa muda wake? Anayechinjwa kwenye kafara analazimishwa kufa kabla ya muda wake kutimia? Hatari sana hii logic yake. In short ushirikina ni dhambi.
Mnyama kuliwa ni haki yake Sio kwa ajili ya makafara
 
Mshana Jr naomba nikuulize,
Mtu aliyechukuliwa msukule si inamaana hajafa kiroho na kimwili? Anaweza kurudishwa akawa kawaida?
Je ukifika wakati Wa Mungu kumchukua inakuaje?..

Jibu la hili swali ni la muhimu sana kaka, sijauliza kujifurahisha... Kuna mpuuzi Juzi kanywesha maji na akasomewa sijui nini huko na mgangaa kaanza kuropoka watu aliowachukua misukule.
Zipo njia nyingi za kurejesha msukule zipo za maombi ya urejesho yaan njia za upande wa Nuru na za Giza pia,na za asili pia kupitia mimea mfano mgomba.
Dunia ina pande mbili ulimwengu usioonekana na unaoonekana.
Msukule ni mwanadamu aliyefichwa na wachawi asionekane na macho ya wanadamu huku akiendelea kuishi Duniani wachawi,bubu, watoto wasioanza kuongea,mbwa,paka,nk wanao uwezo wa kuona misukule.
Msukule akifa baada ya kumaliza ule mda aliopangiwa na Mungu ufa na kwenda kuzimu mwili wake uliwa na wachawi,kwann kuzimu sababu alichukuliwa dhambini,mtu mwenye ulinzi wa Mungu hawezi chukuliwa kiendacho kuzimu ni roho na nafasi yake,kule kuzimu uchukua mwili mpya kwa ajili ya mateso tokana na dhambi alizotenda Duniani.
Kuzimu ni kubwa kuliko dunia na Ina magereza kulingana na aina ya dhambi.
 
Kwahio ni mwili ndio huenda kuzimu ila roho sio lazima iende kuzimu?
 
Mshana Jr naomba nikuulize,
Mtu aliyechukuliwa msukule si inamaana hajafa kiroho na kimwili? Anaweza kurudishwa akawa kawaida?
Je ukifika wakati Wa Mungu kumchukua inakuaje?..

Jibu la hili swali ni la muhimu sana kaka, sijauliza kujifurahisha... Kuna mpuuzi Juzi kanywesha maji na akasomewa sijui nini huko na mgangaa kaanza kuropoka watu aliowachukua misukule.
Msukule ni mateka wa kiininacho anakuwa hajafa, ndio maana kinachozikwa ni gogo ama mgomba na huko matekani hupewa dada za kupumbaza akili ili asijitambue ikiwa ni pamoja na kukatwa ulimi asiweze kuongea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom