Usianzishe biashara wala kutafuta kazi kupitia waganga wa kienyeji

Usianzishe biashara wala kutafuta kazi kupitia waganga wa kienyeji

Kila lenye mwanzo halikosi tamati mkuu
Mkuu ili uwe salama mbele za Mungu, toa bure mali na kila kitu ulichokipata kupitia shirki ndio uanze upya kujikusanyia mali kupitia nguvu za Mungu. ulichokifanya ni sawa na mtu kupata mali kwa njia zisizo halali alafu anaenda kuzibariki kwa Mungu
 
Mkuu ili uwe salama mbele za Mungu, toa bure mali na kila kitu ulichokipata kupitia shirki ndio uanze upya kujikusanyia mali kupitia nguvu za Mungu. ulichokifanya ni sawa na mtu kupata mali kwa njia zisizo halali alafu anaenda kuzibariki kwa Mungu
Maneno ya Mungu mwenyezi Baba yanasema hivi tazama ya kale yamepita na sasa yamekuwa mapya
 
Ndugu mambo yamegoma kama ulivyo eleza kuwa kuna nyakati huwa hivyo kiasili. Hali sio njema kabisa je nifanyeje ili nipate unafuu?.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Natangaza maslahi yangu! Mimi sio mganga na sifanyi ushirikina tena!

Kati ya waganga wote wa kienyeji ni asililia kumi hivi kati ya mia moja ndio wakweli na kati ya hao wakweli ni asilimia 5 tu ndio wenye masharti nafuu na wanaoweza kukusaidia moja kwa moja..! Ishu ya kuwajua feki na wakweli tutaona huko mbele

Kwanza lazima tukubaliane kuwa ushirikina ni utumwa, na ushirikina ni masharti na vigezo..Na ushirikina ni kitu chenye kuhitaji update kila wakati.. Na waganga wengi ni wapigaji!

Pamoja na shida zako zote usijaribu kwenda huko kwenye ushirikina kutafuta 'assist' huko unaenda kufanya registration kwenye data base yao na hatimaye kuwa kwenye himaya yao. MAKINIKA!

Chochote kinachohusika na ajira ama biashara ukiachana na visomo vya kidini lazima kitahusisha damu. Automatically itakuwa damu ya mnyama hasa mbuzi na ng'ombe ama kuku.. Kwa uchache kabisa na kwa siri kubwa damu ya mtu itahusika.

Mnyama anayechinjwa kwa shughuli za ushirikina ni wazi analazimishwa kufa kabla ya muda wake wa kufa kutimia. Vita yake yoyote ya kiroho baada ya hapo utaibeba wewe.. Kwahiyo utakuwa na vita mbili ama zaidi ya kupigana.. Vita yako, vita ya kuku, vita ya mbuzi nknk.. Na hapa ndio siri ya side effect asiyokwambia mganga, Lakini lingjne ni hili... Yule mnyama aliyetumika kukutengenezea mambo yako ana ukomo wake wa kuwa, hivyo wakati wake wa kufa ukifika, kafara ulilotengenezewa nalo hufa rasmi..! Hapo ndio utaona mambo yako yanavyoanza kuyumba na hatimaye kuharibika kabisa

Lingine ni kwamba kuna wakati katika maisha mambo huenda mrama bila sababu yoyote ile..ni asili tu inafanya kazi, wewe kwa kuhofia kuwa tayari umeshapigwa na kitu kizito tena, utakimbilia kwa mtaalam wako tena, na yeye hata kama hakuna tatizo atalitengeneza na kukutisha sana. Juu ya yote kwakuwa tayari uko kwenye database zao kuna wakati huamua kukorofisha mambo ili tu umuendee ajione bingwa ama kuna kitu umtimizie

Mwishowe unakosa kabisa ladha ya maisha unafanya biashara lakini hutulii ni makafara kwa kwenda mbele, una kazi yako nzuri Lakini masharti ni kama yote unapata pesa Lakini huna furaha nazo.

Mganga naye ni binadamu akiamua kula bata hutengeneza tatizo kwakuwa kila mganga ni mchawi.. Pesa ya kutengeneza tatizo ndio huwa pesa ya starehe kwakuwa haimpi masharti kama ile pesa ya kilinge inayotokana na tatizo genuine!

Mwanzoni mwa biashara, ajira na hata mahusiano na miradi mingine epuka sana kuyanajisi na ishu za giza yasije yakaja kukutesa mbeleni, kwa kuwa kuingia huko ni rahisi sana lakini kutoka ni habari nyingine. Na ni shughuli pevu
kaka mshana nahitaji msaada wako, sijui ni vipi naweza kuwasiliana na wewe.
 
Back
Top Bottom