Usichanganye Imani yako na Biashara,si nzuri inakupotezea wateja

Usichanganye Imani yako na Biashara,si nzuri inakupotezea wateja

CONTROLA

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2019
Posts
7,001
Reaction score
23,449
Biashara zina mbinu nyingi sana za uendeshwaji kila mtu anatumia mbinu yake ili kupata wateja wake ila huwa nawambiaga watu kila siku ktk biashara hamna kitu kirahisi kama kupata mteja/wateja,yani katika vitu huwa virahisi hicho ni namba 1.

Shida/mtihani/mziki huja wapi unajua? Kumfanya yule mteja aliekuja kwako leo kununua sukari wiki ijayo sukari yake ikiisha arudi tena hapo hapo dukani kwako kununua sukari,Kumfanya yule mteja uliemshonea nguo leo,kesho pia akitaka kushona nguo ingine afikirie kurudi hapo hapo ofisini kwako kushona.

Kuna mambo mengi ambayo humfanya mteja arudi kupata huduma ofisini kwako,leo tuongelee hili swala la imani zetu za dini tulizonazo/tulizokuzwa nazo tangu utoto mpk sasa tumejitambua tumekua watu wazima,nitaweka tabia chache tu ambazo si nzuri kwa mfanyabiashara

Kufungulia Mahubiri/mawaidha

Ni kweli nafahamu wewe ni mlokole kweli tena umekuzwa katika maadili ya ulokole na utakatifu tangu utoto wako na najua jinsi gani unatamani kuwa karibu na Mungu wako wakati wote unapotembea/unapokaaa/unapopiita nk nk,na tena nafahamu wewe ni muislamu swafi kabisa usie na mawaa na wala hua ujinga wowote ktk maisha yako ila linapokuja swala la biashara tujue kutofautisha A na B,biashara na imani yako ni vitu viwili tofauti.

Mtu anafungua ofisi yake asubuhi na siku hizi Tangu flash ziingie ndio balaa,bora zamani ilikua mtu anaweka Radio station kuna ule muda wa matangazo hata mteja akiingia anajua hii radio,ila siku hizi unakuta mtu ana flash yake kaijaza mawaidha/mahubiri halafu sasa akiingia kazini anachomeka kwenye radio yake ofisini panageuka kanisani/msikitini kelele mwanzo mwisho,mahubiri anatoka mwakasege anaingia rwakatare,anafata gwajima,anakuja mwamposa yani Hamna Poo.

huku kwingine ni DUA au Mawaidha yanatoka ya dokta sule,anafata kipoozeo,anakuja othman maalim anakuja kishki yani ni bandika bandua ukiingia dukani/ofisini kwa mtu unakua huelewi yani unavurugwa tu yani kwa mfano mimi ninapoingia duka la mtu wa namna hii bila kujali n mkristu mwenzangu au muislamu huwa naweza jikuta naghairi natoka natafuta duka lingine.

Kufungulia Nyimbo za imani yako

Unaingia mahali unapokelewa na kaswida,kwaya,nk ki ukweli sisemi ni vibaya kuburudika ofisini kwako na nyimbo uzipendazo lakini kumbuka hapo n kwenye biashara na sio kwako,ukiwa nyumbani kwako pga kasidah/kwaya/mahubiri hadi chooni hutoskia mtu anaongea kitu kwasababu kule ni kwako,lakini tunapokuja huku kwenye biashara tambua hapo si kwako mwenye pake ni mteja wako.

Unajiskiaje mwenye eneo lake "mteja" kaingia (ni mkristu aliye kwiva kbsa) anakukuta unaskiliza mawaidha yale ya waislamu wakisema wakristu ni makafir kisha wanachangia kwa maneno yao yale ya ajabu ajabu,hv unafkiri huyu mteja akiskia unategemea next time atarudi kwenye hilo duka au hiyo ofisi kupata huduma? Sahau.

Unajiskiaje mwenye eneo lake "mteja" kaingia (ni muislamu wale wa itikadi kali) anakuta unaskiliza mahubiri ya hawa wahubiri wasio na break midomoni anasema "waislamu wote wana mapepo,waje kwa yesu awaokoe" hivi huyu mteja akaingia akakutana na hiki kipande unafikiri kesho yake kama anataka sukari imeisha kwake atarudi hapo kwako? sahau Anaweza kunywa hata maji na mkate nakuhakikishia.

Kuchoma/kufukiza UDI

Hii sijui maana yake nini lakini kusema ukweli ktk vitu nachukia mpaka nashkwa na kitu kooni ni pale ninapoenda sehemu ya mtu ya biashara halafu nasikia harufu za namna hii ki ukweli inakera inaboa na inaudhi,kama ni masharti ya waganga hebu ombeni waganga wawabadilishie hayo masharti maana ki ukweli wateja wengi huchukizwa na hicho kitu ni basi tu hawawezi kukwambia.

Imani zetu tujaribu kuzitenganisha na biashara zetu,tufahamu kwamba biashara si mali zetu,una duka la TV fahamu kwamba hizo TV si zako n za wateja zingekua zako ungezipeleka kwako lakini kwakua umefahamu sio zako umeamua kufungua frem ili mwenye tv yake aje ifata siku atakayoamua yeye,sasa kwanini unatengeneza mazingira ya ki ubaguzi kwenye ofisi yako?

unajua kuna watu hawapendi hata kuwasiliana na mtu ambae ni tofauti nae kiimani achilia mbali kununua bidhaa yake,humjui mteja wako n wa aina gani na atakuja vipi nadhani ni vyema unapokua ktk biashara uwe Neutral,simama kati kati akija muislamu msalimie kiislamu kama unajua kusalimia,akija mkristo msalimie ki kristo kama n mtu mpenda hzo salamu,kaa hapo kati kati.

Usiwatenge wateja wako na imani yako,wewe amini unachokiamini,Muamini unaemuamini lakini unapokuja kazini STAY NEUTRAL epuka kuweka/kuonyesha alama zozote za dini flani ktk eneo lako la biashara,usije ukasema hukuambiwa na kama unaona nina gubu sawa kama haikufai iache hapa hapa. END.
 
Mkuu kufungulia mawaidha au mahubiri, qaswida au nyimbo za kwaya nk haileti athari yyte kwa mteja, kama tatizo basi itakua ni la huyo mteja coz hajitambui kikichompeleka pale dukani au ofisini, Tz ni nchi moja wapo ambayo inayoishi kwa uvumilivu sana raia wake, sidhani kama kutakua na athari kwa hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kufungulia mawaidha au mahubiri, qaswida au nyimbo za kwaya nk haileti athari yyte kwa mteja, kama tatizo basi itakua ni la huyo mteja coz hajitambui kikichompeleka pale dukani au ofisini, Tz ni nchi moja wapo ambayo inayoishi kwa uvumilivu sana raia wake, sidhani kama kutakua na athari kwa hilo

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna umoja wapi mkuu?

Watu wameshajitenga wanasema kabisa kua "muislamu ndugu yake ni muislamu yeyote aliyekinyume nao ni kafir" halafu we unasema kuna umoja?

Kama kweli kuna umoja bas nenda zenji kafungue bucha la yule mnyama halafu baadae nitakutafuta unielekeze umelazwa hospitali gani nije nikuone
 
Kwanza unatakiwa ushukuru hio amani ulionayo mpaka sasa hujabaguliwa kidini na hata jirani yako Muislam.
Kuna umoja wapi mkuu?

Watu wameshajitenga wanasema kabisa kua "muislamu ndugu yake ni muislamu yeyote aliyekinyume nao ni kafir" halafu we unasema kuna umoja?

Kama kweli kuna umoja Nenda zenji kafungue bucha la yule mnyama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna umoja wapi mkuu?

Watu wameshajitenga wanasema kabisa kua "muislamu ndugu yake ni muislamu yeyote aliyekinyume nao ni kafir" halafu we unasema kuna umoja?

Kama kweli kuna umoja bas nenda zenji kafungue bucha la yule mnyama halafu baadae nitakutafuta unielekeze umelazwa hospitali gani nije nikuone
Nimecheka sana,eti umemshauri aende zenji akafungue bucha la nini?

STRUGGLE MAN amini nakwambia usione mtu kakunyamazia ufikiri

kapendezwa na hicho unachokifanya,tumshukuru MUNGU hajatupa uwezo

wa kuona moyo wa mtu mwingine unasemaje,tungekimbiana nakwambia.
 
Mkuu kufungulia mawaidha au mahubiri, qaswida au nyimbo za kwaya nk haileti athari yyte kwa mteja, kama tatizo basi itakua ni la huyo mteja coz hajitambui kikichompeleka pale dukani au ofisini, Tz ni nchi moja wapo ambayo inayoishi kwa uvumilivu sana raia wake, sidhani kama kutakua na athari kwa hilo

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwako yaweza kuwa sawa na wala isiwe na tatizo,ila

si wote wanaopendezwa na hilo mkuu na wala sio kwamba

hawajitambui La hasha,ila basi tu wanaona si eneo sawa kufanya hvyo.
 
Nina jirani ana mambo ya kiyahudi sana nami kwakuwa somehow ni anti-semitic situmii huduma zake za fedha.

Kuna wale wanaojidai kufata dini sana huwa sitaki mazoea na huduma zao unless awe familia ya kinabii au sheikh maana inawalazimu wawe hivyo hata kwa unafiki tu. Siwezi fanya kazi na mtu anayelazimisha nimuone ni mcha Mungu.
 
Umenena vyema sana ila kuna vichwa ngumu watakuja kukubishia hapa , mie vyote naweza kuvumilia japo kwa taabu ila sio hayo maharufu sijui ya udi ubani ni vitu ambavyo sijawahi kuvipenda kabisa
Mimi huwa nikienda sehemu nikakuta mtu kachoma/kafukiza udi

naghairi natoka sinunui kitu chochote duka hilo,sijui nielezeje jinsi nachukia.
 
Kama vituo vya mafuta vya victoria, yaani ukienda pale hata kama hauna mapepo unaanza kukemewa
Hii haileti picha nzuri hata kidogo

Kama ni mkristo: Unakuta kaning'iniza rozari juu au kaweka picha ya yesu ukutani

Kama haitoshi unakuta kakuwekea na kifungu marko 3:21-26

Kwa waislamu: unakuta kaweka maandishi ya kiarabu ambayo kwa wasiojua lugha wanaweza wakahisi ni madongo ambayo yanawalenga watu wasio waislamu

Au dukani unakuta kaweka picha inayoonesha jiwe la makka halafu pembeni kuna vidada viwili vya kiarabu vimenyoosha mikono ishara ya kuomba huku vikiangalia juu
 
Umesema kweli kabisa mkuu,nilikuwa nadogo nimemweka dukani yeye mda wote yupo na mambo ya dini nikajikuta biashara inataka kwenda loss.nikampiga stop ndio ikawa pona ya biashara yangu.wateja ni wabaguzi sana
Watu wanatafuta mchawi wakati mchawi ni tabia zao wenyewe mtu anabaki

analaumu anakosa wateja kumbe shda n yeye kageuza duka msikiti/kanisa
 
Back
Top Bottom