Usichanganye Imani yako na Biashara,si nzuri inakupotezea wateja

Usichanganye Imani yako na Biashara,si nzuri inakupotezea wateja

Mkuu kufungulia mawaidha au mahubiri, qaswida au nyimbo za kwaya nk haileti athari yyte kwa mteja, kama tatizo basi itakua ni la huyo mteja coz hajitambui kikichompeleka pale dukani au ofisini, Tz ni nchi moja wapo ambayo inayoishi kwa uvumilivu sana raia wake, sidhani kama kutakua na athari kwa hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaan i wish ungemuelewa mtoa mada hope ungenufaika sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna umoja wapi mkuu?

Watu wameshajitenga wanasema kabisa kua "muislamu ndugu yake ni muislamu yeyote aliyekinyume nao ni kafir" halafu we unasema kuna umoja?

Kama kweli kuna umoja bas nenda zenji kafungue bucha la yule mnyama halafu baadae nitakutafuta unielekeze umelazwa hospitali gani nije nikuone
Ukianza kwenda kumwona mkuu nishtue japo na mimi nimpeleke vidonge vya maumivu[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bila kusau salamu wanazotumia sana sana waislam, kila mtu wanaemuona ni salam aleku tu...
ukiwauliza utasikia salam aleku ni lugha ya kawaida tu kama za asubuh, asa kama lugha ya kawaida mbona haitumiki kanisani!!?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilishagombana na muarabu sjui mnani yule alinisalimia hivyo namimi

nikamjibu "bwana yesu asifiwe" ktk kulumbana tukapishana kauli mwisho

niliamua kuondoka ila nilimuacha anaongea sjui alimaliza saa ngapi kuongea.
 
  • Thanks
Reactions: _ly
Binafi hii ya kuchoma udi hua inanikera kwel mimi na nikipita duka hilo huwa sirudi tena
Binafsi hata mimi huwa sirudi hilo duka tena,labda

hata itokee bahati mbaya gani,sipendi sipendi kbsa
 
Na sisi tunaoweka status je?
Kama unatumia status kutangaza biashara zako elewa kuwa

hizo status ndio dukani kwako,sasa mtu kama mimi ni kiview

siku nikakuta mahubiri,next day nikakutana gospel asee sirudii

ku view status zako maana najua fika ntakutana na Injili that means

mteja kama mimi utanikosa siku utakapoweka mzigo mzuri maana tyr

ulinipoteza bila wewe kujua,Kama unaweka status instal whatsapp mbili

kwenye simu yako,weka Official whatsapp weka na FM whatsapp kisha

chagua namba ambayo utaitumia kwa biashara na kuweka status zako za kazi

na namba nyingine itumie kwa ishu zako,weka taka taka zote unazotaka huko status.
 
Hii mada nimewahi kuwaza kuandika, ulichosema ni kweli kabisa na kuna watu huwa wanakosea

Kwenye upande wa dini umeuelezea, kuna upande wa siasa pia

Unakuta mtu ameweka bendera ya Chama chake kwenye Ofisi yake ya kibiashara

Unakuta mtu mwanzo mwisho ni nyimbo za Chama chake cha siasa

Unakuta mmiliki mwingine wa biashara kazi yake ni kuvaa nguo za Chama flani

Kama ni mjasiriamali unapaswa kukumbuka kuwa, eneo lako la kazi halipaswi kugeuka kuwa sehemu ya Uenezi wa Chama chako. Watu wanasahau kuwa wateja wao wana itikadi tofauti tofauti za kisiasa
Biashara zina mbinu nyingi sana za uendeshwaji kila mtu anatumia mbinu yake ili kupata wateja wake ila huwa nawambiaga watu kila siku ktk biashara hamna kitu kirahisi kama kupata mteja/wateja,yani katika vitu huwa virahisi hicho ni namba 1.

Shida/mtihani/mziki huja wapi unajua? Kumfanya yule mteja aliekuja kwako leo kununua sukari wiki ijayo sukari yake ikiisha arudi tena hapo hapo dukani kwako kununua sukari,Kumfanya yule mteja uliemshonea nguo leo,kesho pia akitaka kushona nguo ingine afikirie kurudi hapo hapo ofisini kwako kushona.

Kuna mambo mengi ambayo humfanya mteja arudi kupata huduma ofisini kwako,leo tuongelee hili swala la imani zetu za dini tulizonazo/tulizokuzwa nazo tangu utoto mpk sasa tumejitambua tumekua watu wazima,nitaweka tabia chache tu ambazo si nzuri kwa mfanyabiashara

Kufungulia Mahubiri/mawaidha

Ni kweli nafahamu wewe ni mlokole kweli tena umekuzwa katika maadili ya ulokole na utakatifu tangu utoto wako na najua jinsi gani unatamani kuwa karibu na Mungu wako wakati wote unapotembea/unapokaaa/unapopiita nk nk,na tena nafahamu wewe ni muislamu swafi kabisa usie na mawaa na wala hua ujinga wowote ktk maisha yako ila linapokuja swala la biashara tujue kutofautisha A na B,biashara na imani yako ni vitu viwili tofauti.

Mtu anafungua ofisi yake asubuhi na siku hizi Tangu flash ziingie ndio balaa,bora zamani ilikua mtu anaweka Radio station kuna ule muda wa matangazo hata mteja akiingia anajua hii radio,ila siku hizi unakuta mtu ana flash yake kaijaza mawaidha/mahubiri halafu sasa akiingia kazini anachomeka kwenye radio yake ofisini panageuka kanisani/msikitini kelele mwanzo mwisho,mahubiri anatoka mwakasege anaingia rwakatare,anafata gwajima,anakuja mwamposa yani Hamna Poo.

huku kwingine ni DUA au Mawaidha yanatoka ya dokta sule,anafata kipoozeo,anakuja othman maalim anakuja kishki yani ni bandika bandua ukiingia dukani/ofisini kwa mtu unakua huelewi yani unavurugwa tu yani kwa mfano mimi ninapoingia duka la mtu wa namna hii bila kujali n mkristu mwenzangu au muislamu huwa naweza jikuta naghairi natoka natafuta duka lingine.

Kufungulia Nyimbo za imani yako

Unaingia mahali unapokelewa na kaswida,kwaya,nk ki ukweli sisemi ni vibaya kuburudika ofisini kwako na nyimbo uzipendazo lakini kumbuka hapo n kwenye biashara na sio kwako,ukiwa nyumbani kwako pga kasidah/kwaya/mahubiri hadi chooni hutoskia mtu anaongea kitu kwasababu kule ni kwako,lakini tunapokuja huku kwenye biashara tambua hapo si kwako mwenye pake ni mteja wako.

Unajiskiaje mwenye eneo lake "mteja" kaingia (ni mkristu aliye kwiva kbsa) anakukuta unaskiliza mawaidha yale ya waislamu wakisema wakristu ni makafir kisha wanachangia kwa maneno yao yale ya ajabu ajabu,hv unafkiri huyu mteja akiskia unategemea next time atarudi kwenye hilo duka au hiyo ofisi kupata huduma? Sahau.

Unajiskiaje mwenye eneo lake "mteja" kaingia (ni muislamu wale wa itikadi kali) anakuta unaskiliza mahubiri ya hawa wahubiri wasio na break midomoni anasema "waislamu wote wana mapepo,waje kwa yesu awaokoe" hivi huyu mteja akaingia akakutana na hiki kipande unafikiri kesho yake kama anataka sukari imeisha kwake atarudi hapo kwako? sahau Anaweza kunywa hata maji na mkate nakuhakikishia.

Kuchoma/kufukiza UDI

Hii sijui maana yake nini lakini kusema ukweli ktk vitu nachukia mpaka nashkwa na kitu kooni ni pale ninapoenda sehemu ya mtu ya biashara halafu nasikia harufu za namna hii ki ukweli inakera inaboa na inaudhi,kama ni masharti ya waganga hebu ombeni waganga wawabadilishie hayo masharti maana ki ukweli wateja wengi huchukizwa na hicho kitu ni basi tu hawawezi kukwambia.

Imani zetu tujaribu kuzitenganisha na biashara zetu,tufahamu kwamba biashara si mali zetu,una duka la TV fahamu kwamba hizo TV si zako n za wateja zingekua zako ungezipeleka kwako lakini kwakua umefahamu sio zako umeamua kufungua frem ili mwenye tv yake aje ifata siku atakayoamua yeye,sasa kwanini unatengeneza mazingira ya ki ubaguzi kwenye ofisi yako?

unajua kuna watu hawapendi hata kuwasiliana na mtu ambae ni tofauti nae kiimani achilia mbali kununua bidhaa yake,humjui mteja wako n wa aina gani na atakuja vipi nadhani ni vyema unapokua ktk biashara uwe Neutral,simama kati kati akija muislamu msalimie kiislamu kama unajua kusalimia,akija mkristo msalimie ki kristo kama n mtu mpenda hzo salamu,kaa hapo kati kati.

Usiwatenge wateja wako na imani yako,wewe amini unachokiamini,Muamini unaemuamini lakini unapokuja kazini STAY NEUTRAL epuka kuweka/kuonyesha alama zozote za dini flani ktk eneo lako la biashara,usije ukasema hukuambiwa na kama unaona nina gubu sawa kama haikufai iache hapa hapa. END.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Source ya biashara ni imani mkuu umefata sukari chukua sukari sepa mengine waachie wenyewe kama ulinyo ww hupendi mahubiri na wenzio hawawapendi wa2 wasiosikiliza mahubiri
 
1.wewe ni msabato,unabiaahara na siku sabato ikianza unafunga biashara yako eti sabato imeanza wale ambao ni wateja wako ambao sii wasabato unataka na wao waanze sabato?

2.wewe ni mkatoliki ama mlokole una duka ama hoteli mwezi wa kwaresma ,na jumapili unafunga eti ni mwezi watoba,wateja wako hawajui imani yako wanachojua ni kwamba umepewa leseni na serikali utoe huduma kwa umma bila ubaguzi sasa ukimaliza mwezi wako wa toba wateja wakiwa wamehama utarudi kanisani kuomba maji ya upako ili kurudisha wateja?

3.wewe umefunga mwezi mtukufu ,umepewa leseni kuhudumia umma lakini wewe unafunga biashara na kuwalazimisha wateja wako naowafunge6
 
Naunga mkono hoja mkuu
Kuwa neutral ni jambo muhimu sana.
Wadau wamegusia vizuri kwenye dini na siasa. Acha mimi niongezee kwenye ushabiki, unakuta mtu duka zima
Kalipiga mibendera ya club anayoshabikia, kavaa jezi, ukutani kalenda ya team yake yaani hata bidhaa anayokuuzia unakuta amekufungashia kwenye kigazeti kinachofagilia team yake.
Hua mara kadhaa tunazichukulia kama sababu ndogo ndogo lakini kwa mtazamo mpana zinaweza kuathiri soko la bidhaa za mtu.
Mimi binafsi imeshawahi nitokea mara kadhaa nikaacha kununua bidhaa kwa mtu kwa sababu tu kapiga uzi wa team yake inayopingana na team ninayo shabikia.
Tuweni neutral kwa masaa machache ya kazi, ukirudi nyumbani hata ukipenda jifunike mpaka shuka la team yako.
 
Back
Top Bottom