Kijakazi
JF-Expert Member
- Jun 26, 2007
- 7,093
- 10,469
Watanzania wengi walifurahishwa sana na hiyo iliyoitwa Katiba mpya ya Kenya na pengine si ajabu hata ndiyo moja ya sababu ya sisi pia kuanza mchakato wa kuandika hii iliyoitwa Katiba Mpya.
Lakini kuna kitu ambacho nafikiri Watanzania wengi hawakijui kuhusu Katiba Mpya ya Kenya, ambapo kwa maoni yangu nafikiri ni usanii mtupu kwa mfano Cheo cha Mkuu wa Wilaya hakijafutwa kama ilivyo hapa kwetu na bado anateuliwa na Raisi wa Nchi.
Yaani kwa maana nyingine hawa Magavana wao wa County hawana madaraka yoyote kwa maana kuna Mkuu wa Wilaya ambaye ndiye muwakilishi wa Raisi kwenye hiyo county na ndie ana mamlaka na Dola hapo kwenye county na siyo Gavana wa county, sasa ndiyo wamefanya nini?
Si ni kama Bongo tu?