Usichokijua kuhusu Pacquiao

Ngengemkenilomolomo

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2015
Posts
270
Reaction score
450
Jamaa mbali na kuwa bondia mkubwa sana lakini pia ni Mbunge wa huko nchini kwake Ufilipino na tetesi zilizopo ni kwamba anataka kugombea urais wa nchi hiyo maana raia wake wanamkubali sana kwa sababu kwanza kama tunavojua kua Ufilipino ni moja ya nchi maskini kwahiyo jamaa pamoja na kuwa Mbunge wala hakai mjini kwenye majumba ya maana kama walivo wenzake yan yeye yupo mtaa wa kawaida tu na wananchi wake, kwa Dar unaweza kusema Mbagala.

Halafu kingine ni kwamba wakati anaelekea Las Vegas alinunua tiketi zenye thamani ya Dola mil 100 kwa ajili ya washabiki wake 900 alosafiri nao kutoka Ufilipino..

Nawasilisha
 
mangumi yote anayopigwa kichwan atakuwa na akili ya kuongoza nchi kweli?
 
Ndugu yangu Dolla million 100 kwa ajili ya washabiki wake 900, ni ngumu kumeza au ulimanisha nini????????????????
 
Pia alikulia kwenye umaskini mkubwa akiwa ombaomba wa mitaani anyelala
kwenye mitaro. Kipaji cha ubondia ndicho kilichomtoa mitaroni.
 
Atumie dola million 100 kusafirisha mashabiki wakati hilo pambano bila kujali matokeo litamwingizia dolla million 99 hiyo itakuwa akili au matope?
 
Atumie dola million 100 kusafirisha mashabiki wakati hilo pambano bila kujali matokeo litamwingizia dolla million 99 hiyo itakuwa akili au matope?

Sory mkuu nilikusudia kusema dola mil 10 ila nkaandika 100 lkn cdhan kama 40% anayoipata ina thaman ya hzo mil 99 ulzosema
 
Kuna tetesi Myweather anataka kulikimbia pambano!
 
Kuna tetesi Myweather anataka kulikimbia pambano!

Hata mm nimesoma sehemu kuwa kunauwezekano mkubwa maywether kutotokea kwny pambano! Dah! Ikitokea ivyo basi ngumi kwake basi, aende tu hakapigwe,ila tahalibiwa sura yule
 
Hata mm nimesoma sehemu kuwa kunauwezekano mkubwa maywether kutotokea kwny pambano! Dah! Ikitokea ivyo basi ngumi kwake basi, aende tu hakapigwe,ila tahalibiwa sura yule

Itakuwa bonge la aibu!
 
Ndugu yangu Dolla million 100 kwa ajili ya washabiki wake 900, ni ngumu kumeza au ulimanisha nini????????????????

Duuuh jamaa anatupiga kamba mchana kweupe pacman kalipwa 50m$ then atoe hela yake yote plus 50m$ ingine 4 mashabiki
 
Pambano ni saa ngapi kwa EA time?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…