Usichokijua kuhusu Sensa ya Watu na Makazi

Usichokijua kuhusu Sensa ya Watu na Makazi

Rashda Zunde

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2022
Posts
204
Reaction score
231
Usiku wa kuamkia tarehe 23/8. Ni siku ya Sensa na itabaki kuwa tarehe rejea ya siku ya sensa. Kuhesabu Watu kutaendelea kwa takribani siku 6 hadi saba kwa kuzingatia tarehe rejea.

Ieleweke kuwa sensa haiwezi kukamilika kwa siku moja kwa nchi nzima. Hivyo hata ukipumzika inawezekana siku hiyo Kaya yako isifikiwe hivyo hakuna mantiki ya kupumzika kwa wale wanaofanya vibarua au Kazi za kila siku.

Unachotakiwa kufanya ni kuorodhesha na kuandika kwenye karatasi watu wote watakaolala Kwenye kaya yako usiku wa kuamkia siku hiyo.

Taarifa muhimu ni pamoja na:
1. Jina kamili (matatu)
2. Jinsia (me/ke)
3. Umri
4.Hali ya ndoa
5. Namba ya simu
6. Namba Nida
7. Taarifa za Elimu
8. Taarifa za hali afya
9. Umiliki wa Ardhi, Majengo, vifaa/rasilimali
10. Taarifa ya Shughuli za Kiuchumi
11. Mengineyo (uraia)

Pamoja na kuacha Taarifa hizo karani atakupigia simu kuhakiki Taarifa ulizoacha tafadhali toa ushirikiano.

Mimi niko tayari kuhesabiwa . WEWE je?
 
Sitaki hata kuwaona......mpaka waje na majibu ya government levy ndio nini kwenye miamala ya bank.......vinginevyo kama ni mwanaume akija kwangu atarudi kuwa shoga WA historia na kama ni ke ntamtia gundu la inzi WA chooni au mende mweusi........shubamiti
 
Back
Top Bottom