Mtume Muhammad alitumia busara kubwa sana kufundisha mema, alikua mjanja sana hakutaka vita na Shetani, wala binadamu muovu yeye alikua anawaeleza watu habari nzuri za Mungu wala hakutaka vita nao.
Ndio maana katika mahubiri yote yanayofanywa na Waislamu, yanaeneza amani hutawahi kusikia Imamu wala Sheikh akisema anampiga Shetani lakini hawa wengine mfano wachungaji wanadai kuwa wanampiga Shetani katika mahubiri yao, wewe unampigaje? kwanza hulingani nae kwa chochote, yupo tangu binadamu wa kwanza hajaumbwa, leo hii uzaliwe wewe umpige? Haingii akilini hata kidogo.
Natoa mfano rahisi- Jeshi la Tanzania linapigana na Jeshi la nchi nyingine na hutawahi kuona Jeshi la Tanzania likipigana na mgambo wa mtaa. Yaani Jeshi la Tanzania liwashe vifaru vyote na mizinga yote likapigane na mgambo wa mtaa? Huo utakuwa ni ujinga uliopitiliza na wala hutawahi kuona popote pale.
Binadamu akisimama na Shetani ni sawa na tembo na kuku.
Labda niseme hivi, nikwasababu tu Shetani anaona hawa hakuna wajuacho na wala hapigani vita na kuku lakini angeamua kuwamaliza ni kitendo cha dakika sifuri. Nasema hivi kwasababu kama Yesu alimalizwa wao ni akina nani awashindwe.
Yesu alieneza habari za Mungu kwa hasira kubwa ndio maana alichukua kiboko akawatandika wale wote waliokuwa wakifanya biashara kwenye hekalu la Mungu na kutangaza vita na Shetani hapo ndipo wazee wa mahekalu wakajawa na hasira kali na kumkamata.
Mkuu, naomba nikunukuu
......hutawahi kusikia Imamu wala Sheikh akisema anampiga Shetani lakini hawa wengine mfano wachungaji wanadai kuwa wanampiga Shetani katika mahubiri yao,................. Yesu alieneza habari za Mungu kwa hasira kubwa ndio maana alichukua kiboko akawatandika wale wote waliokuwa wakifanya biashara kwenye hekalu la Mungu na kutangaza vita na Shetani hapo ndipo wazee wa mahekalu wakajawa na hasira kali na kumkamata.
Naomba unifafanulie haya yafuatayo:
1. Hivi wale mahujaji (Hija)kuna siku hufanya Ibada ya kutupa jiwe/mawe (kokoto saba)katika bonde la Minah. Hapo huwa wanamrushia nani hayo mawe?
2. Hebu chukulia kwamba wewe ungekuwa ni Yesu. Katika Hekalu au mahali pa kuabudia huwa kuna Taratibu za kuzingatia uwapo mahali hapo na pia ni mahali panapostahili Heshima ya kipekee(Hii hata katika Misikiti ipo na inazingatiwa ipasavyo).
Sasa ikitokea watu kwa makusudi wanakiuka utaratibu huo na wala hawaheshimu mahali hapo panapotumika kumwabudu Mungu wewe kama Yesu Ungelifanyaje kwa sababu pameshakuwa au pamegeuzwa ni kama sokoni, gulioni au mnadani - hata ukipaza sauti hutosikika.
Hatua ya Yesu kuchukua kiboko ichukuliwe kama inavyokuwa kwa mzazi anayemuonya mwanae ampendaye au mwalimu anayefundisha wanafunzi wake.
****Kuna Upotoshaji mkubwa katika maelezo yako unapotumia neno
Hasira Kubwa.
Mkuu hebu soma tena Marko 11: 15-24 Hakuna neno au haijaandikwa kwa Hasira kubwa.
"Yesu aliingia
Hekaluni akaanza kuwafukuza
watu waliokuwa wakifanya biashara humo. Akapindua meza za waliokuwa wakibadilisha fedha na viti .."
Kwa hiyo hata leo ingekuwa ni Msikiti halafu wakatokea watu fulani wakaanza kufanya biashara humo, Unadhani Sheikh au Imamu au kiongozi wa Msikiti mahalia angelikaa kimya?. Je, utasema anahasira?
3. Yesu hakukamatwa na Wazee. Yesu alikamatwa na kikosi cha Askari (Yohana 18:3-12) na kundi la watu wakiongozwa na Yuda Iskariote (Marko 14:43-49).
Mkuu, katika hali ya kawaida, Wazee na uzee wao wasingeliweza hiyo shughuli ya kukamata au sio ?
4. Mtume Mohammad(s.aw.) alitoka (alikimbia) Makka kwenda Madina......... Je, unadhani waliokuwa wakimfutilia walikuwa ni kwa jambo la Kheri au ni kwa shari?
Ni nani (Roho gani) aliyewahamasisha watu hao kuwa wakorofi vile? unadhani sio Ibilisi / Shetani? By the way, mm siijui (ni mjinga kabisa) inapokuwa ni hoja za Quran.