OSEFUKANY
JF-Expert Member
- Jan 16, 2011
- 2,437
- 3,896
Pole aisee. Usimwendekeze bali MKATAE na Mambo yake yote.Acha tu amenifanya nyama hadi sasa nipo nipo tu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pole aisee. Usimwendekeze bali MKATAE na Mambo yake yote.Acha tu amenifanya nyama hadi sasa nipo nipo tu
Usiseme kirahisi kama ni rahisiPole aisee. Usimwendekeze bali MKATAE na Mambo yake yote.
Kweli sio rahisi kivile. Yakupasa ujitoe Kikweli-kweli na maumivu yatakuwepo ila hatimaye utaibuka mshindi- ni uhakika hilo.Usiseme kirahisi kama ni rahisi
YesKweli sio rahisi kivile. Yakupasa ujitoe Kikweli-kweli na maumivu yatakuwepo ila hatimaye utaibuka mshindi- ni uhakika hilo.
Shetani hakuondoka alimchapa kichapo kitakatifu msalabani na ukawa mwisho wa Yesu kuishi,Aah Bhana; Acha. Usipotoshe watu kwa maandiko yako binafsi. Soma Mat.4:1-2 " ..Kisha Roho alimwongoza Yesu mpaka Jangwani ili ajaribiwe na Ibilisi. Akafunga siku arobaini mchana na usiku....." Unaweza pia kuisoma toka Marko 1:12-13.
(hapo uelewe Roho ni Roho Mtakatifu na kamwe sio Ibilisi. Ibilisi sio mjinga amchukue Yesu na kupmpeleka jangwani ili Yesu akamshinde kwa Technical Knock-Outs. Kwani kila hoja Ibilisi aliyoitoa e.g. eti geuza mawe haya yawe mkate.., ukinisujudia nitakupa ......na blaablaaa nyingi, majibu Yesu aliyotoa yalimwacha Ibilisi mdomo wazi na hatimaye Ibilisi alisepa ki-mtindo.
Karibu tusome pamoja Mkuu
We bhana wee; wapi tena umeyasoma hayo? Hebu soma Mathayo 4: 11 ..Basi Ibilisi akamwacha .....Shetani hakuondoka alimchapa kichapo kitakatifu msalabani na ukawa mwisho wa Yesu kuishi,
Wale waliomsulubisha walikua wachamungu? Jiulize hilo swali,We bhana wee; wapi tena umeyasoma hayo? Hebu soma Mathayo 4: 11 ..Basi Ibilisi akamwacha .....
Pia soma Luka 4:13 Ibilisi alipokwisha mjaribu kwa kila njia, akamwacha kwa muda.
Sasa wewe unayatoa wapi hayo? Hayo ni ya kwako mzee.
Karibu tena tusome pamoja mkuu.
Tena nikukumbushe kwamba Yesu yu hai mzima sasa na hata milele.
Siwezi kujiuliza hilo swali kwani haliunganiki na hiki tunachobishania hapa. Waliomsulubisha Yesu ni maaskari na ukizingatia Askari yeyote ni lazima (kwa mujibu wa Taratibu za kazi yake) Aitii mamlaka iliyopo.Wale waliomsulubisha walikua wachamungu? Jiulize hilo swali,
Wale askari walitumwa na wapinga Kristo, kwa hiyo wapinga Kristo walishindaSiwezi kujiuliza hilo swali kwani haliunganiki na hiki tunachobishania hapa. Waliomsulubisha Yesu ni maaskari na ukizingatia Askari yeyote ni lazima (kwa mujibu wa Taratibu za kazi yake) Aitii mamlaka iliyopo. Askari wale hawakuwa na ugomvi wowote dhidi ya Yesu. Wao alitimiza wajibu wao. Lakini kwamba eti walikuwa wacha-Mungu hilo halinihusu. Anayejua ni nani mchaMungu na ni nani siyo mchaMungu ni Mungu peke yake. Je, wewe unafikiri kazi ya Uaskari siyo kazi halali kama kazi nyingine?
Yesu aliumba vyote? Ila kuna watu ni wajinga sana.Yesu Kristo ndiye aliyeumba vyote akiwepo shetani leo hii atakuwaje na nguvu kuliko Yesu?
Kwahiyo:-Watu wengi hasa hapa JF nimejifunza hata hawasomi vyanzo vya mambo ambayo wanayaandika.
Habari za shetani kutoka akiwa katika mlima wa Mungu mpaka kuwa Ibilisi zimeandikwa extensively na Bibilia. Ila kichekesho ni kuwa mtu anasikia stori somewhere labda Youtube kwa mtu then anachomoka na post ikiwa full na opinions zake na kinachofanana na chanzo halisi ni majina tu.
Mfano mtoa mada kamkuza shetani kana kwamba ni praise team ya shetani.
- Mosi, shetani hajawahi kuwa malaika proper, Shetani ni Kerubi aliyeasi.
- Pili, shetani hakuwahi kuwa malaika mkuu in any sense. Haya ni mawazo ya watu. Shetani alikuwa ni Kerubi afunikaye. Hakuna mahali Biblia inamtaja kama malaika mkuu
- Tatu, shetani sio kinyume wala usawa wa Mungu. shetani ni kiumbe tu na hana mamlaka yoyote nje ya kiumbe aliyo nayo. Shetani ana mamlaka kuliko mwanadamu kwa sababu yeye ni kerubi na sisi ni wanadamu. Lakini bado ni kiumbe tu na hana mamlaka yoyote mbele ya Mungu.
- Nne Ayubu aliyeruhusu ajaribiwe ni Mungu. Kifupi mtu aliyesoma kitabu cha Ayubu sura chache tu atajua mtoa mada hajui anachoandika!
- Nne Yesu pia hakusulubishwa kwa sababu shetani ana nguvu kama mwana wa Ibilisi alivyoandika. Yesu pale Gethsemane aliomba kwa Baba na si shetani kikombe kimuepuke. Ni Mungu mwenyewe aliyeamua iwe hivyo na shetani mpaka leo hapendi ukweli kwamba Yesu alikufa msalabani. Alichofanywa pale anakijua vizuri sana!
Mwisho niwashauri watu wanaopenda kuandika mambo ya imani, angalau itendee haki basi hayo maandiko unayonukuu badala ya kuchukua kichwa cha habari na kuandika kisichohusiana kabisa!
Shetan ni cheo kikubwa sana, hasumbui watu, sisi ndio tunamsumbua, miaka yote amekuwa akisingiziwa kuwa ana ubaya ili asipate wafuasi, habari zote za ubaya zilizoandikwa kuhusu yeye ni uongo mtupu.Kwahiyo:-
Shetani alitoka wapi? Kwanini anasumbua wanadamu? Kwanini Mungu hapendi tumfate shetani na mambo yake?
Hata wewe hapo ni raia. Ukifungwa jela maisha jina linabadilika...unakuwa mfungwaMkuu, mbona haileti Logic kwa sababu umesema Lucifer ni Malaika mkuu (kwa hiyo ni Malaika ukiachana na cheo chake) na tena ukasema malaika wa chini yake ( uzingatie kwamba nao pia ni Malaika japo hawakuwa na cheo). Baada ya vita ulioisema ya huko mbinguni Lucifer na wenzake wakafukuzwa mbinguni. Kufukuzwa mbinguni hakukuwafanya au kuwaondolea waache kuwa ni Malaika i.e. Hao wote (Lucifer na Wafuasi wake)ni Malaika WALIOASI.
Kwa mantiki hiyo Malaika walioasi(Lucifer + Wafuasi wake) walifukuzwa mbinguni na kutupwa duniani. Lakini Bado kwa kutupwa duniani hakukuwaondolea kuwa ni Malaika.
Sasa mkuu, uniambie hao unaowaita mapepo wakuu na Mapepo wa kawaida wametokea wapi tena?
Hii habari ya Malaika waliogeuka kuwa Mapepo wakuu naomba utoe reference ya mahali ulipoisoma.
Nakushauri soma Kitabu cha Enock Sura ya 6 - 9. Utapata mwanga kidogo.
Mkuu, mbona unaikwepa mada? Jikite kwenye hoja ya msingi. i.e. Kiumbe aitwaye Malaika na kama uasi wake ulimfutia/Ulimwondolea kuwa ni malaika. Habari ya vyeo isubirishe kwanza ili hoja hii ipate majibu kwanza.Hata wewe hapo ni raia. Ukifungwa jela maisha jina linabadilika...unakuwa mfungwa
Dah! aisee; Hivi unajisemea kwa nafsi yako(ie. kama unavyoona na kufikiri wewe binafsi) au kuna mahali maandiko(Reference) yanakuelekeza au ku-support hoja yako? Kama hakuna mahali unafanya Rejea(reference) hoja yako ni BUTU na HAINA mashiko. - Tupa kule.Wale askari walitumwa na wapinga Kristo, kwa hiyo wapinga Kristo walishinda
Aisee!!Ni kweli mkuu shetani hawezi kuwa na nguvu kuliko Yesu, lakini iko hivi:
Yesu kimwili ni Binadamu i.e alikua, aliishi sawa kama na sisi tunavyoishi.
Lakini Kiroho, Yesu ni Mungu na ndo maana ndiye aliyeumba vyote na Shetani analifahamu hilo na kukiri hivyo.
Kwa mantiki hiyo, Shetani alipambana na Yesu lakini ilikuwa ni kimwili zaidi na aliishia kuudhuru mwili.Hakuweza na Alishindwa kabisa Kiroho. Yesu alifufuka na kuvaa mwili usioharibika tena.
Hoja inaeleweka, ni kweli Ayubu alichapwa pamoja na Yesu, Adam na Hawa wakasomeshwa sasa kwanini nisiseme Shetan alishinda?Dah! aisee; Hivi unajisemea kwa nafsi yako(ie. kama unavyoona na kufikiri wewe binafsi) au kuna mahali maandiko(Reference) yanakuelekeza au ku-support hoja yako? Kama hakuna mahali unafanya Rejea(reference) hoja yako ni BUTU na HAINA mashiko. - Tupa kule.
Hadithi tu za kiyahudi hiziYesu Kristo ndiye aliyeumba vyote akiwepo shetani leo hii atakuwaje na nguvu kuliko Yesu?
Mkuu; Ujue hoja au majibu yako yanasomwa na wengi sio mm tu. Chukua tahadhariHoja inaeleweka, ni kweli Ayubu alichapwa pamoja na Yesu, Adam na Hawa wakasomeshwa sasa kwanini nisiseme Shetan alishinda?
Hoja yangu ni hivi, kwakua Yesu alisulubishwa vibaya alipokuwa akijaribu kumpinga Shetani basi Shetani sio wa kuingia nae vitani, Ikiwa Yesu pamoja na nguvu zake zote alipata adhabu yote ile basi sisi binadamu ni akina nani hata tuthubutu kuanzisha vita na Shetani?Mkuu; Ujue hoja au majibu yako yanasomwa na wengi sio mm tu. Chukua tahadhari