Moment of silent
JF-Expert Member
- Feb 19, 2021
- 855
- 1,483
Hakuna nabii hata mmoja kwa mujibu ya imani ya uislamu alishindwa mtihani baada ya kutahiniwa na shetani.Fuatilia jinsi yesu alivyoishi ndipo utatambua mcha Mungu anatakiwa kuishije
Hii utakuta katika biblia, jinsi ilivyokuwa na utovu wa adabu na mitume wa ALLAH.
Na hata akikutahini shetani kwa mja muumini na Kudura ya muumba ipo karibu yako basi kwamwe hutoweza kumuelekea shetani katika mrengo wake.
Adam na Hawa walitahiniwa na ALLAH kupitia shetani aliyelaaniwa ila walitubia kwa makosa yao wala hawakuweza kuelekea katika mrengo wa shetani..
TANBIHI: Kutahiniwa kupo na kukosea kupo kwa binaadam ila kutotubia ni kiburi na kufanya hivyo ndipo matakwa ya shetani yanapotimia.
Shetani ni adui wa kudumu wa mwanaadamu hii yote ni kutokana na husda zake pale alipoambiwa amsujudie adamu kwa sijda ya heshima akakataa na kukaidi maagizo ya muumba wake na kuendelea na kibri chake hapo ndipo alipo laaniwa hadi leo hii!!
Madaraka ya shetani yapo kwa wanaomtii.