Usidhani shetani ni mdogo kama unavyofikiri

Mtu amepigwa mawe mpaka kufa alafu anasema ameshindaje?
Kibinadam utamshinda ila kiroho na kiimani umemshinda.maana huu mwili niwamuda tu ila roho iliyosafi itaishi milele.ila roho ovu haitaishi milele.roho ovu zitateketezwa kabisa na hakutakuwa na uwasi tena
 
Shetani nae hata haeleweki,, aafu mungu alimuokota wapi. Shetani Mkubwa.
 
Biblia yenyewe inakiri kuwa yeye ndo mtawala wa dunia. Yesu alipokuwa anafunga siku 40, shetani alimfata akamchukua akamtembeza duniani kote akamwambia ukinisujudia mimi nitakupa umiliki dunia yote hii. Yule jamaa ni noma
 
Ni kweli kabisa na kwa kuijua nguvu ya Yesu kiroho alianza kulia na kusononeka pale alipofikia hatua ya kumwomba Yesu kwa kupiga magoti na kusema "Bwana, usituangamize bali tuamuru twende kwenye lile kundi la nguruwe." Marko 5:1-14
Wewe unaongelea mapepo...tunamuongelea Lucifer hapa braza
 
Reference zipo nyingi, wenzetu wengine hawa bado hawajamfahamu, wanapigana na mapepo kila siku wakidhani ni Shetani
 
Kusulubiwa kwa Yesu Kristo haukuwa mpango wa shetani hata kidogo, kasome maandiko ujue hili.
Hata kuteswa kwa Ayubu ni mpango wa Mungu na sio shetani kabisa!
Uwe unasoma maandiko kabla ya kukurupuka
 
Ukubwa wa shetani unatofautiana kati ya mtu na mtu. Ushetani unakuwa kwenye akili yako, mf. Ukitaka kuuwa ni ushetani wa kiwango cha juu. Shetani sio mtu ila ni wazo ovu analotengeneza binadamu.

Katika ulimwengu wa sasa ushetani ni mkubwa sana. Pima ushetani wa Putin ulivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na wala hakuwa shetani ni wanadamu tu na tamaa zao za madaraka, walidhani atawakwapua madaraka.

hakuna spirit inayofanya kazi dunian bila kuuvaa mwili..
hao wanadamu walikuwa under attack spiritual kutimizwa matakwa yasiyo mapenzi yao bali tamaa za yule mwovu
 
Watu wanadanganywa na manabii na mitume wa uongo kwamba wanadhani shetani anaogopa tu mafuta, pamoja na tu mafuta twao still bado wanagaragazwa vibaya na shetani
 
Kama shetani hakumuogopa Yesu ndo aogope huto tu mafuta na tumaji
 
Wewe unaongelea mapepo...tunamuongelea Lucifer hapa braza
Mwanzoni sikujibiwa tofauti kati ya mapepo na shetani. Sasa wewe unasema tunamuongelea Lucifer. Naomba nikuulize hesabu hili na unibainishie ni sawa au sio sawa.;
Pepo = Shetani =Lucifer?
 
Kusulubiwa kwa Yesu Kristo haukuwa mpango wa shetani hata kidogo, kasome maandiko ujue hili.
Hata kuteswa kwa Ayubu ni mpango wa Mungu na sio shetani kabisa!
Uwe unasoma maandiko kabla ya kukurupuka
Hebu tufafanulie ndugu, kwasababu Yesu alikuja kusahihisha watenda dhambi, nao hawakupendezwa kabisa kusahihishwa ndipo wazee wa hekalu wakamtia mikononi kwa lengo la kumwondoa kwasababu hawakupendezwa kusahihishwa.

Hata sasa kwa maisha ya kawaida ukasema unapambana na watumiaji wa madawa ya kulevya sidhani kama utakuwa salama.

Swala la kusahihisha makosa ni gumu sana ndio maana mtoto mchanga anaweza kuchezea kitu ukamwambia acha na asikutii akaendelea na makosa yake
 
mleta mada utakuwa umetumwa na shetani uje umtukuze humu?

Kwa taarifa yako, shetani ni adui aliyeshindwa. Yesu wa msalaba alimshinda pale msalabani (kwa kufa na kufufuka kwake) na sasa huyo Kristo Yesu anaishi ndani ya wote wamwaminio yaani wale wote walioupokea wokovu. Hivyo kwa sasa tunayaishi maisha ya ushindi dhidi ya adui shetani na ibilisi.

JESUS IS LORD
 
Ni kweli kabisa na kwa kuijua nguvu ya Yesu kiroho alianza kulia na kusononeka pale alipofikia hatua ya kumwomba Yesu kwa kupiga magoti na kusema "Bwana, usituangamize bali tuamuru twende kwenye lile kundi la nguruwe." Marko 5:1-14
yale yalikua mapepo mzee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…