Usidharau kinachotamkwa na mwanasiasa, hakuna bahati mbaya kwenye siasa

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Leo ninaandika nikiwa na mawazo mengi sana mchanganyiko. Kwanza nimeshtushwa na hili ongezeko la watu wanaoniita Anko/Mjomba badala ya kaka. Hii inaashiria nini kwa mimi kijana mdogo wa CCM mwenye miaka 38? Wakati nikitafakari hilo nikashtuka kuona mvi kwenye ndevu nilipojitazama kwenye kioo.

Ninaandika huu uzi kuwakumbusha wanaJF wote kuwa hakuna bahati mbaya siasani. Hii ni baada ya watu kupaniki kwa kuona sheria mpya imepitishwa kuwapa mafao wake za viongozi.

Kiukweli hata mimi ninatafakari ni sababu gani ya msingi sana iliyosababisha watu kukaa chini kuamua kuwaneemesha zaidi hizi familia tajiri ambazo hakuna wanachokosa maishani?

Kwenye ilani ya CCM kulikuwa na hizi ahadi kwamba tukichaguliwa tutahakikisha wake za viongozi wanapata ulaji? Mimi bado natafakari na kujipa muda kujifunza kama kuna tija yoyote katika hili.

Haya mambo huwa yanaanzaga katika hali kama ya masikhara hivi kumbe nyuma ya pazia tayari kila kitu kimeshapangwa. Mke wa Rais mstaafu hakuwa anabahatisha kwenye kauli yake.

Kwa wale wafuasi wa Mbowe mtakuwa mmejifunza pia. Viongozi wenu wamekuwa wakitoa kauli zisizoeleweka ila kwa ubishi wenu mmekuwa mstari wa mbele kutetea.
 
Hivi unataka mjane wa aliyekuwa mke wa Raisi kama mama Anna Mkapa, Maria Nyerere nk waonekane wanacheza vikoba, wanaishi kwa kukopa ama kuunga unga kama mke wa mchoma mkaa?
 
Business looks great on paper 😀😀😀
 
You are either too hopeless or slave-minded.
Yaani wake wa viongozi wakubwa wawe maskini?.
Piga picha Maria Nyerere mme wake alistaafu miaka 38 iliyopita. Hiyo hela waliyochuma itakuwepo mpaka leo?
Na kama unavyojua mshahara wa Rais kwa kipindi kile sidhani kama ulikuwa unafika Tsh elfu hamsini, kwa miaka 23 Nyerere aliyokaa madarakani angekuwa amechuma milioni 13.8 tu.
Je fedha hizo zingelikuwapo kwa leo, zingeweza kumtosha mama Maria?
 
Nadhani hata mume wa mama inamuhusu🤣🤣🤣🤣💺
 
Bora ukae kimya mzee siyo lazima kila hoja uchangie, ficha ujinga wako!!!!
 
Kama ni hivyo Mama Maria angekuwa wa kwanza kuomba uwepo wa hiyo sheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…