Usifanye kosa hili kwenye kichwa cha barua ya maombi ya ajira /kazi

Usifanye kosa hili kwenye kichwa cha barua ya maombi ya ajira /kazi

Acheni kufufua makaburi..
Mto mada atachikichia..

Mkuu toa nondo
Jinsi ya ku apply kazi online,cover letters na kila kitu.
 
Habari vijana wenzangu?

Sehemu iliyopita nilionyesha makosa wanayofanya vijana katika kuomba kazi hususasani kwenye taasisi za serikali.

Leo pia nitaeleza shortly juu ya kosa moja dogo nililoliona kwa vijana wetu Tanzania.

Kabla hujatuma maombi ya kazi jua kuwa hilo tangazo limetazamwa na maelfu na wengine wana pass nzuri zaidi yako, hivyo umakini ni kitu muhimu zaidi.

Twende kwenye mada. Mfano :Tangazo la kazi linaonyesha nafasi ni MHASIBU wewe usiandike Yahusu maombi ya kazi ya Uhasibu. Huu ni utoto. Hapo zunguka uwezavyo but lazima utaje nafasi kama ilivyotajwa kwenye tangazo husika. Unaweza kuandika Yahusu maombi ya kazi nafasi ya MHASIBU.

Pia kama wametaja daraja usiache nawe andika pia hii itakufanya usichaniwe barua yako wakati wa kusort hasa marua za mkono.

Kwa anayehitaji huduma ya kusaidiwa mambo mbalimbali ya kazi atachangia elfu 10 tu nitamsaidia but ukiwa makini inatosha hapa kuchukua kitu. Nitaendelea kutoa darasa humu free maana nina mambo mengi.

Mada zijazo:
1.Jinsi ya kutafuta connection
2.C.V bora
3.USAILI
4.Jinsi ya kupewa cheti chuo/secondary huku unadaiwa
N.K, n.k

Note :Wapo waliofanya kosa hilo hapo juu na wakapata kazi but hiyo hesabu kama ilikuwa accidentally
wasomi siku hizi hatuombi kazi tunajiajiri na kutoa kazi kuomba kazi ni utoto
 
Back
Top Bottom