Usifanye maamuzi ukiwa umelewa, yatakugharimu

Usifanye maamuzi ukiwa umelewa, yatakugharimu

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Siku moja nilipata safari kwenda mkoa anakoishi mchepuko wangu, ambaye tulibahatika kuzaa naye. Baada ya kufika katika huo mkoa, nilimjulisha na akanikaribisha niende kumtembelea nyumbani kwake.

Mida ya jioni ilipofika, nilifika nyumbani kwake, tukaongea stori za hapa na pale, huku mtoto akifurahi kumuona baba yake. Nikaona si vizuri, tuendelee kukaa pale, ikabidi nimuombe tutoke kidogo tuende sehemu ya wazi, tuweze kuzungumza huku tukipata moja moto moja baridi.

Kweli akaafiki, akajiandaa na baadaye tukatoka. Ile kufika huko ikawa ni vinywaji na stori za hapa na pale. Akawa ameniambia ana baadhi ya changamoto, mojawapo ni kodi ya nyumba n.k

Kutokana na hali niliyokuwa nayo ya kulewa, nikamjibu haina shida, utaenda kukaa kwenye mji wangu ambao uko hapa Dar, kwa sababu kwa sasa kuna kijana ndio huwa anaweka mazingira ya usafi tu. Nilifanya hayo maamuzi, kwa sababu nilikuwa nikimtizama mtoto, amechukua muonekano wangu, ingawa yeye ni wa kike na ukichanganya na hali ya pombe ilivyokuwa.

Baada ya kukaa muda mrefu, ilibidi tuagane mi nikaondoka; imepita miezi miwili sasa, ananikumbushia ule uamuzi niliompatia. Kusema kweli, nimeshindwa kumuambia ahamie, kwa sababu nilijaribu kulitafakari hilo jambo, nikaona naweza kutengeneza bomu la kusambaratisha ndoa yangu; kwa sababu sina uhakika kama akikaa pale, atakubali kuondoka, pale ambapo atatakiwa kufanya hivyo. Na mbaya zaidi, mke wangu hajui kama nilizaa nje.

Najaribu kumdanganya kuwa, bado kuna ukarabati unaendelea, kama ukimalizika mapema nitamjulisha. Ingawa ukweli, nilimpa ahadi isiyotekelezeka kutokana na ulevi wa pombe.

Wakuu, si nimefanya maamuzi sahihi?
 
Hujafikia hatua ya kulea familia wewe kama mwanaume....kwa hiyo uyoo mtoto wako unataka aishie kuishi kwenye hizo nyumba za kupanga??.
 
Hujafikia hatua ya kulea familia wewe kama mwanaume....kwa hiyo uyoo mtoto wako unataka aishie kuishi kwenye hizo nyumba za kupanga??.
Nasubiri kwanza akue kue, akifikisha miaka 7 hakuna shida
 
Maamuzi ya kulala na Mfalme Zumaridi utajilaumu kesho asubuhi.
UNALALA NA MALAIKA, UNAAMKA NA ZOMBIE.
IMG-20220305-WA0009.jpg
 
Ndio maana nimekwambia hujafkia level ya kulea familia kam mwanaune ww...sasa unasubili afike miaka.7..what if ukitangulia ww mbele ya haki kabla ya yeye hiyo miaka.7..
Hatuombi iwe hivyo
 
Back
Top Bottom