The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Usifanye makosa haya 5 kisa valentine
1: Mwili wako sio zawadi kwa unayempenda
Kama sio ndoa usitoe mwili wako kisa tu ni siku ya valentine, Siku moja inaweza kugharimu maisha yako yote,Jitunze na jiepushe mbali na tamaa za mwili.
2: Kukutana maeneo ya faragha
Usikubali kukutana naye eneo lolote lile ambalo litawashawishi kuanguka dhambini, Kutaneni eneo lenye uwazi na utulivu lisiloleta vishawishi.
3: Usijilinganishe na wengine
Jikubali hivyo hivyo na mahusiano yako na uwezo wa mwenzako,Usianze kutaka kufanyiwa kama fulani au kupelekwa sehemu fulani kama rafiki yako alivyofanyiwa. Furahia mahusiano yako.
4: Usishushe viwango vyako kisa siku moja
Usijishushe kiasi kwamba ukajiingiza kwenye mambo ambayo yanashusha thamani yako ya mwili na maisha kiujumla kisa tu na wewe uonekane una mtu kwa sababu ya siku moja.
5: Usifanye zaidi ya uwezo wako kwa ajili ya kumridhisha mtu fulani.
Kama hakupendi unaweza kumfanyia kila kitu na bado akakuacha hivyo usitumie nguvu kubwa sana bali fanya kwa uwezo wako na kuwa halisi.
Hitimisho
Upendo hauna siku moja maalumu bali tumeagizwa kupendana siku zote. Hivyo usiwekeze sana kwa ajili ya siku moja bali anza kuwekeza jinsi ya kumpenda huyo mwenzako siku zote
Hakuna zawadi yeyote yenye thamani ya mwili wako. Ukipokea zawadi sio kigezo cha wewe kutoa mwili wako na kama ni hivyo bora usipokee hiyo zawadi.
David Sima