Usiginwaji wa Katiba Bungeni: Watetezi wa Haki za Binadamu nchini walaani. Wawakumbushia umuhimu wa kila raia kuilinda Katiba ya Nchi

Usiginwaji wa Katiba Bungeni: Watetezi wa Haki za Binadamu nchini walaani. Wawakumbushia umuhimu wa kila raia kuilinda Katiba ya Nchi

Roving Journalist,
Wajulisheni kuwa Bunge haliendeshwi kwa kusikiliza vyombo vya habari vimetangaza nini kama Chadema hawakumjulisha Spika kuwa huyo mbunge uanachama wake wa Chadema umekoma basi Spika hawezi chukua maamuzi yoyote. Chadema inaupungufu sana kwenye mambo ya administrative. Hii ni sawa na issue ya Lissu eti utetezi wao ulikuwa eti Spika anajua kwa sababu vyombo vya habari vinatangaza alipo. Hawa nao sheria hawaijui au wanataka wawaonyeshe wafadhiri wao kuwa wanafanyakazi.
Wewe ni mpuuzi moja . Huyu Mwambe si alijiuzulu mbele yake yeye spike ?! Na bado Cdm wakamwandikia barua

Odhis *
 
AZIMIO LA KUMSHTAKI SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. JOB NDUGAI KWA KUKIUKA MISINGI YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BAADA YA KUMRUHUSU BW. CECIL MWAMBE KUENDELEA NA UBUNGE

Ndugu RAIA MWEMA,
Awali ya yote tunakushukuru na kukupongeza kwa kazi kubwa unayoifanya ya kuzuia kuenea kwa maambukizi ya COVID-19 hasa wakati huu ambapo dunia inaendelea kupambana na janga la virusi vya Corona (COVID 19). Sisi kama watetezi wa haki za binadamu tunapenda kukutia moyo uendelee kujilinda wewe pamoja na uwapendao.

Ndugu RAIA MWEMA,
Shirika la Elimu ya Uraia na Msaada wa Sheria (CILAO) limesikitishwa na kitendo cha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kufanya maamuzi yanayokiuka misingi ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Itakumbukwa kwamba, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Vyama vya Siasa vinaongozwa kwa mujibu wa Katiba na sheria zingine za nchi. Ibara ya 71 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza wazi kuhusu ukomo wa mtu kuwa Mbunge. Kwa mujibu wa Ibara ya 71(1)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni wazi kuwa Mbunge atapoteza nafasi yake ya ubunge ikiwa atapoteza uanachama wa chama chake kilichompatia dhamana ya ubunge wakati wa uchaguzi.

Mnamo tarehe 6 Mei 2020, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, aliruhusu, aliyekua mbunge wa Ndanda, Bw. Cecil Mwambe ambaye alishajiuzulu nafasi yake ya ubunge aendelee na kazi hiyo. Hata hivyo, Bw. Cecil Mwambe alishaonekana katika vyombo vya habari akitangaza kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kwa kuwa Bw. Mwambe alishatangaza kijiondoa CHADEMA, basi tunaamini pasipo shaka kwamba alipoteza tayari sifa ya kuendelea kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ndugu RAIA MWEMA,
Kitendo cha Spika kumruhusu Bw. Cecil Mwambe kuendelea kuwa Mbunge ni ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa kuwa Katiba inatamka wazi katika Ibara ya 26(1) kuwa kila RAIA ana wajibu wa kusimamia na kutetea Katiba na Sheria, sisi kama Taasisi tunaomba kushirikiana nawe na wadau wengine kusaini azimio hili la haraka ili kumtaka SPIKA kubatilisha maamuzi yake. Pia tunaomba tushirikiane haraka iwezekanavyo kufungua kesi katika Mahakama Kuu kuomba ufafanuzi wa Mahakama kuhusu kitendo hiki cha Spika.

#PamojaTulindeKatiba

Azimio hili limeandaliwa na: Civic and Legal Aid Organisation (CILAO)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na iwe hivyo haraka. Huyu mgogo asitufanye watu na akili zetu kama yeye. Ni spika wa hovyo kabisa. Peleka mahakamani huyu.
 
Vipi kuhusu Mheshimiwa Selasini Mbunge wa Rombo aliyetangaza hadharani kujivua uwanachama wa Chadema na kuhamia NCCR-Mageuzi na bado anaendelea na ubunge?.

Yaani Chadema inatangaza kwamba Wabunge wake waliohamia NCCR Mageuzi wataendelea na Ubunge lakini aliyehamia CCM avuliwe, hii ni akili?

Nakumbuka vizuri kwamba, Spika alihitaji Muhtasari wa Kikao cha chama cha CHADEMA kuhusu kumuondolea Mwambe Ubunge. Lakini Chadema waliwasilisha barua pekee pasipo viambatanisho.

Civil Society msitumike kama mawakala wa Mabeberu na Vyama vya upinzani, teteeni Haki za Kiraia zenye tija kwa wananchi na Taifa.

Lengo lenu ni kuikomoa CCM, Kumkomoa mbunge au Wananchi wa Rombo wasipate mwakilishi katika bunge la bajeti?.
Ikumbukwe kwamba, Mheshimiwa Zitto, wakati amezuliwa uwanacha na Chadema, bado aliendelea na ubunge, Mbona hamkuazimia kumshtaki spika wala mahakama?.

Mbunge ni mwakilishi wa wananchi sio chama, hivyo tulieni
 
Wewe ni mpuuzi moja . Huyu Mwambe si alijiuzulu mbele yake yeye spike ?! Na bado Cdm wakamwandikia barua

Odhis *
Wewe mjaluo usinisumbue kwa umbumbumbu wako. Kasome sheria ya uchaguzi na bunge ndiyo utajua nina maana gani acha mapovu ya wanasaccos.
 
Vizuri kabisa hili jambo lote limefanywa kuwaumiza cdm, mnazidi, kuna ugomvi upi, kuna iadui upi hasa ambao chadema wameufanya mpk mnatengenezaga magomvi haya yote.

Kuwa shambulia kuwavunja mikono kuwaua serikali inatakiwa iwaeleze Watanzania hao chadema wamefanya ubaya upi.

Kutwa kucha kuwazuia kufanya siasa, kuwashambulia maofisini mwao Mameya wao kuondolewa, madiwani wao. Haya basi muwamalize kuwaangamiza hao chadema wakija vyama vingine kuchukua madaraka mtapenda kufanyiwa hivyo?

Mnaona raha ipo siku yatawageukia, MUNGU awalinde CHADEMA na kuwapa ujasiri wa KUFANYA SIASA ZA UPINZANI KWA AMANI. MUNGU ALIE HAI AISHIE MILELE ASHUGULIKE NAO WATU WAISHIO KWA HIRA NA UCHOKOZI

Nnaunga mkono hoja hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mheshimia Selasini hajajivua msikilize vizuri
Vipi kuhusu Mheshimiwa Selasini Mbunge wa Rombo aliyetangaza hadharani kujivua uwanachama wa Chadema na kuhamia NCCR-Mageuzi na bado anaendelea na ubunge?.
Yaani Chadema inatangaza kwamba Wabunge wake waliohamia NCCR Mageuzi wataendelea na Ubunge lakini aliyehamia CCM avuliwe, hii ni akili?
Nakumbuka vizuri kwamba, Spika alihitaji Muhtasari wa Kikao cha chama cha CHADEMA kuhusu kumuondolea Mwambe Ubunge. Lakini Chadema waliwasilisha barua pekee pasipo viambatanisho.
Civil Society msitumike kama mawakala wa Mabeberu na Vyama vya upinzani, teteeni Haki za Kiraia zenye tija kwa wananchi na Taifa.
Lengo lenu ni kuikomoa CCM, Kumkomoa mbunge au Wananchi wa Rombo wasipate mwakilishi katika bunge la bajeti?.
Ikumbukwe kwamba, Mheshimiwa Zitto, wakati amezuliwa uwanacha na Chadema, bado aliendelea na ubunge, Mbona hamkuazimia kumshtaki spika wala mahakama?.
Mbunge ni mwakilishi wa wananchi sio chama, hivyo tulieni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni mpumbavu wa kiwango cha standard gauge, CAG alivyoliita bunge dhaifu na limeshikiwa akili na jiwe je aliandika barua kwa maandishi akamplekea ndugali au aliongea tu knyn chombo cha habari? Mbona alimwita sasa ajieleze kama hafanyii kazi habari za media?
Hopeless ass!
 
Anakadi namba ngapi Thelasini ya NCCR?

Tulimuona Mwambe akikabidhiwa kadi hadharani Tulimuona Mwambe akikabidhiwa kadi hadharani kupitia katibu wa ccm
 
Nakumbuka yale maneno ya miaka mingi.BUNGE NI DHAIFU.Ina maana wabunge wetu hawalioni hili wailinde katiba wanayoitumia kila siku wamkemee bosi wao.
Hopeless comment ever!!
 
Haya mambo mwalimu NYERERE, aliyaona sana, ndio maana akasema binadamu anaweza akajifanya MUNGU mtu, na ndio kinachotokea na hiyo ni spika tu chanzo ni radio ipo sehemu nyingine kijijini imetulia, mambo yanaendeshwa kama mpira wa makaratasi?
Solution ni kukataa huu ujinga , tatizo bongo bado Kuna ng'ombe wengi Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vizuri kabisa hili jambo lote limefanywa kuwaumiza cdm, mnazidi, kuna ugomvi upi, kuna iadui upi hasa ambao chadema wameufanya mpk mnatengenezaga magomvi haya yote.

Kuwa shambulia kuwavunja mikono kuwaua serikali inatakiwa iwaeleze waTZ hao chadema wamefanya ubaya upi.
Kutwa kucha kuwazuia kufanya siasa, kuwashambulia maofisini mwao Mameya wao kuondolewa, madiwani wao. Haya basi muwamalize kuwaangamiza hao chadema wakija vyama vingine kuchukua madaraka mtapenda kufanyiwa hivyo????

Mnaona raha ipo siku yatawageukia, MUNGU awalinde CHADEMA na kuwapa ujasiri wa KUFANYA SIASA ZA UPINZANI KWA AMANI. MUNGU ALIE HAI AISHIE MILELE ASHUGULIKE NAO WATU WAISHIO KWA HIRA NA UCHOKOZI

Nnaunga mkono hoja hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
AMEN

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wenye magonjwa yasiyotibika hawafai kuongoza mihimili ya dola
 
Back
Top Bottom