Raia mmoja
Member
- May 3, 2021
- 43
- 115
Mkuu Mshana, nakubali sana michango yako sehemu nyingi, lakini kwenye hili nitatofautiana nawe kidogo!Humu mitandaoni watu wanapigwa sana. Kuna madalali humu wamejaa shuhuda za kutunga na zinavutia sana!
Kama kungekuwa na huu ushirikina wa kumfanya mtu akulipe mahakama kusingefurika kesi za madai. Ama mahakama zetu zingekuwa na afueni kubwa sana...
Kwanza ifahamike Mimi sio mganga wa kienyeji na siungi mkono sana mambo hayo, hasa kwasasa ambapo nimeamua kumrudia mwenyezi Mungu muumba mbingu na ardhi.
Sisi wote ni binadamu na kwanamna Moja au nyingjne tumejikuta tumepitia au kufanya mambo ya aina hiyo kwenye maisha. Kuhusu mganga anayeweza kumfanya mdeni wako akulipe nimewahi kushuhudia kwa macho yangu hilo likitendeka tena ni mwaka huu huu mwanzoni.
Kuna jamaa mmoja alikuwa anafanya kazi kiwanda cha rasta pale Mbagala (sikumbuki kama ni kiwanda cha Angels au Darling). Kiwanda hiki kiliwasimamisha kazi wafanyakazi wengi kikiwa na lengo la kuwaachisha kazi bila ya kuwalipa mafao yao na malimbikizo yao ya mishahara kwa zaidi ya miezi 6.
Huyu jamaa alielekezwa kwa mganga mmoja Mwana mama (msukuma). Aliniomba nimsindikize kwahuyo mganga, Akampatia dawa ya kuoga, jamaa alikuwa anawasiwasi sana kama atafanikiwa, maana aliidharau sana ile dawa, baada ya kuiogea ile dawa kesho yake alipigiwa simu kuitwa kiwandani kulipwa mafao yake yote pamoja na malimbikizo yake ya mshahara. Jamaa hakuamini hata Mimi sikuamini mpaka alipokabidhiwa fedha zake.Jamaa aliniomba nimsindikize akampe shukrani yule mama mganga.
Japo siamini sana mambo ya kishirikina wala siwashauri watu waende huko lakini mambo haya yapo, na Mimi ni shaidi wa jambo hili, mwisho naomba radhi kama ushuhuda huu utamgusa mtu yeyote, lengo ni kusimulia na sio kumtaja mtu.