Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Ligi za barabarani kati ya madereva nyingi zimesababisha majanga mengi kwa:
Madereva,
Abiria,
Waenda kwa miguu,
Magari,
Na uharibifu wa mali.
Kuna Watu leo hii ni marehemu, wakiwa wameacha wajane na yatima kwa sababu ya hizi ligi. Kuna watu leo hii ni walemavu na wamegeuka tegemezi kwa asilimia mia kwa sababu ya hizi ligi. Hasara ni nyingi, na madhara ni mengi pia.
Lakini je, ulishawahi kujiuliza hao wanaokimbia sana barabarani wanakimbilia nini? Wanawahi nini? Wao sio Polisi kwamba wanawahi eneo la tukio; sio fire kwamba wanawahi kuzima moto mahali; sio ambulance kwamba wanawahi kuokoa uhai mahali.
Katika maisha yao yote wamekimbia, lakini hawana walichotuzidi... labda ajali! Walikowahi hawakupata kikubwa zaidi... labda fumanizi!
Barabarani, nenda mwendo wako. Usiige, usifanye ligi za bure. Hazina mwamuzi, hazina kombe.
Unayefanya naye ligi:
Hujui uzima wa gari yake,
Hujui uzima wa tairi zake,
Hujui umahiri wake kwenye usukani na pedeli,
Hujui changamoto zake kwenye maisha.
Sasa unashindana naye ili iweje?
Maisha yako ni muhimu zaidi ya ligi zisizo na faida. Una wapendwa wanakusubiri nyumbani. Wafikirie hao kwanza kabla hujaamua kukoleza mwendo ili kuonesha ushujaa usio na pongezi.
Jioni njema, Tanganyika!