Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi nina maneno yangu nikiwa nadrive kwamba kila mtu ana safari yake,hata nikiwa nafanya jogging hvyohvyo akitokea jogger mwenzangu na mimbio yake namuacha aende zake wala simfuatishi,imenisaidia sana mentality hiyoLigi za barabarani kati ya madereva nyingi zimesababisha majanga mengi kwa:
Madereva,
Abiria,
Waenda kwa miguu,
Magari,
Na uharibifu wa mali.
Kuna watu leo hii ni marehemu, wakiwa wameacha wajane na yatima kwa sababu ya hizi ligi. Kuna watu leo hii ni walemavu na wamegeuka tegemezi kwa asilimia mia kwa sababu ya hizi ligi. Hasara ni nyingi, na madhara ni mengi pia.
Lakini je, ulishawahi kujiuliza hao wanaokimbia sana barabarani wanakimbilia nini? Wanawahi nini? Wao sio polisi kwamba wanawahi eneo la tukio; sio fire kwamba wanawahi kuzima moto mahali; sio ambulance kwamba wanawahi kuokoa uhai mahali.
Katika maisha yao yote wamekimbia, lakini hawana walichotuzidi... labda ajali! Walikowahi hawakupata kikubwa zaidi... labda fumanizi!
Barabarani, nenda mwendo wako. Usiige, usifanye ligi za bure. Hazina mwamuzi, hazina kombe.
Unayefanya naye ligi:
Hujui uzima wa gari yake,
Hujui uzima wa tairi zake,
Hujui umahiri wake kwenye usukani na pedeli,
Hujui changamoto zake kwenye maisha.
Sasa unashindana naye ili iweje?
Maisha yako ni muhimu zaidi ya ligi zisizo na faida. Una wapendwa wanakusubiri nyumbani. Wafikirie hao kwanza kabla hujaamua kukoleza mwendo ili kuonesha ushujaa usio na pongezi.
Jioni njema, Tanganyika!
Lakini nilikuwa najisemea moyoni kuwa huyu bwana mdogo hana siku nyingi za kuishi....π₯Ίπ₯Ίπ₯ΊAsante ndugu yangu kwa ukumbusho murua hakika vijana wana la kujifunza.......
Nilipewaga lift na bwana mdogo mmoja nilikuwa naenda mazikoni huko upareni......ilikuwa ni hizi Prado Tx......
Kati kati ya safari akaja kupitwa na jamaa mwenye Mark X.....mzozo ukaanzia hapo..... ilikuwa mshike mshike....mtu mzima nimeshikilia roho....
Dua zangu ilikuwa tufike salama Korogwe tu niamuachie gari yake maana vurugu ilianzia Kabuku kuitafuta Segera.........
Nikashukia Korogwe nikawaacha na ligi yao.....
Lakini nilikuwa najisemea moyoni kuwa huyu bwana mdogo hana siku nyingi za kuishi....
Hii akili ingelikuwa na madreva woteingelipunguza kiasi kikubwa cha ajari barabaraniLigi ka ligi kuuu baraaa
Yaaanii ka wewe ni dereva endesha ukitambua wewe ndo mwenye akili awo wengine ni hawaelewi chochote
Barabara Kuna maeneo yanatambulika kwa kafaraaa
Get prepared
Sala/ibada muda wote
Ka nchi kao kadogo vile; hizo gari wanakimbizia wapi? Ujumbe hauwahusu wale yakheeWa zanzibar umewasahau mkuu