Usije Dar es Salaam -- huko mkoani usafiri, hali ya hewa, usalama viko vizuri sana

Usije Dar es Salaam -- huko mkoani usafiri, hali ya hewa, usalama viko vizuri sana

Nigga What

Senior Member
Joined
May 1, 2021
Posts
164
Reaction score
448
Ebwana kama upo mkoani unafanya kazi au biashara unapata average income usijaribu kuwaza kuja jijini DAR, kwa sababu huko mkoani usafiri, hali ya hewa, usalama viko vizuri sana.

Kama uko Mbeya, Iringa, tulia usafiri wa mbeya ni rahisi na magari ni mazuri sana, hali ya hewa shwari, nyumba za kupanga kibao, vyakula ndio nyumbaani haswaa

Kama upo Dodoma endelea kuenjoy utulivu wa nchi, hakuna jam na hali ya hewa ni favourable, makazi ni ghali kidogo lakini hakuna kero kumetulia.

Kama upo lindi, Mtwara kula upepo wa bahari, usafiri buku unapanda boda mpaka unaacha, vyakula si sana lakini kuna utulivu na hali ya hewa safi.

Morogoro, Tanga, Arusha, Moshi hali ya hewa ni shwari chakula cha kutosha, utulivu wa hali ya juu na maisha yanasonga vizuri.

Shida ni jiji la DAR hapa ndugu yangu Mvua ikinyesha siku 2 mawasiliano ya kinondoni na ilala yanakata kabisaa, kama unaishi ilala upo kinondoni tafuta lodge ulale maana salendar hupiti na mkwajuni hupit.

Joto ndio usiseme babu, huko mkoani unalala bila feni na madirisha closed huku ni tofauti unafungua madirisha yote na feni unalala nayo hata wakati wa kula gemu majirani lazima wachabo,dala dala kufika mjini nako kero utakaa kwenye foleni mpaka utakuta kuijua dar na muda wa kurudi hivyo hivyo.

Huku huwezi kuamua sehemu ya kupanga nyumba kama bajeti yako ndogo uswahilini, uchafu ndio usiseme jiji chafu balaa, usalama ndio haupo kabisa wezi, wahuni, wadangaji kama wote najua hata nikoani vitu hivi vipo ila huku ni chuo kikuu
 
Kuishi dsm lazima uwe kichaaa.

Binadamu wa kawaida hawezi kuishi hili jiji.

Mkandamizo wa hewa, uchafu, joto, kila mtu ana hasira anafuta jasho ,maisha flani ya kishetan kabisa.

Dsm haifai kabisa,NILIKUWA NAOMBA IBOMOLEWE.

kabisa
 
Mi nilifika stendi nikapokelewa na jamaa sema alikuwa spidi sana nilisahau kumwambia naenda wapi hadi wa Leo sijamuona dar wakalimu ww
 
Kusema kweli Dar hapafai kabsa. Siku ya kwanza kufika Dar nilikuwa sina kitambaa cha kufuta jasho aiseee nilikoma. Usiku unatamani utoke ukalale nje maana si kwa joto hilo.
 
Yaani nimesoma mada… nikasoma comments zote… wengi wa wasoma comments Dar wamekuja kusalimia ndugu tu..
Sasa endeleeni kudanganyana kuhusu dar.
Kwa maneno machache DAR PATAMU SAAAAAANA.
 
Back
Top Bottom