Usije Dar es Salaam -- huko mkoani usafiri, hali ya hewa, usalama viko vizuri sana

Usije Dar es Salaam -- huko mkoani usafiri, hali ya hewa, usalama viko vizuri sana

Inakuwaje sasa waliolazimishwa na mwendazake kwenda dom wanamlaani mpka kesho?
Inakuwaje sasa ikifika tu ijumaa mchana mabasi yote ya dom daf yanajaa, ndege zinajaa, mashangingi yanashindana tu mibio kuwahi dar?
Halafu mbona mabalozi wa nchi zoote wamegoma kuhama hapa kwenhe jiji unaloita la mashetani ingawa walipewa viwanja huko dom?
Nasiku hzi matamko yote ya nchi yanatokea jumba jeupe pale magogoni karibia na bahari inayonuka.
WACHA WIVU SEMA UNAJILIWAZA KISA UMEHAMISHIWA DODOMA AMBAPO WATU WOOOTE ETI MNAKUTANAGA BAMBALAGA [emoji1787]
[emoji23][emoji2][emoji2][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inakuwaje sasa waliolazimishwa na mwendazake kwenda dom wanamlaani mpka kesho?
Inakuwaje sasa ikifika tu ijumaa mchana mabasi yote ya dom daf yanajaa, ndege zinajaa, mashangingi yanashindana tu mibio kuwahi dar?
Halafu mbona mabalozi wa nchi zoote wamegoma kuhama hapa kwenhe jiji unaloita la mashetani ingawa walipewa viwanja huko dom?
Nasiku hzi matamko yote ya nchi yanatokea jumba jeupe pale magogoni karibia na bahari inayonuka.
WACHA WIVU SEMA UNAJILIWAZA KISA UMEHAMISHIWA DODOMA AMBAPO WATU WOOOTE ETI MNAKUTANAGA BAMBALAGA [emoji1787]
😂😂😂😂 We jamaaa umenifanya nicheke mpaka watu wananishangaaa🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kama una plan ya mkoan andaa eneo kabisa. Mfano kama mkoa wa morogoro kuna sehemu zamani palikua ni mashamba na mapori lakini siku hizi watu wamejenga so overtime nako kutakua na maeneo machache.
Nishajiandaa tayari Nina mashamba ambayo nayalipia serikali ya Kijiji na pia nayaendeleza pia mkoani mjini Nina kiwanja kikubwa tu ambacho kinatosha kujenga nyumba hata nne na ukichukulia Nina vijana wawili na Sina mpango wa kuongeza panatutosha hata kuzikana.
 
Nenda Kibaha nunua eka 3 - 5 jenga, lima bustani, fuga, panda miti upate hewa nk...

Kibaha to town,Magu katuwekea njia tano tunapuyanga tu mpaka posta 45mins....
Nina eneo Bagamoyo mizani pale la kutosha kiasi Ila kibaha ni good spot na bei bado nzuri, hela ndio kikwazo maana Hali haijatengamaa. Ila kibaha pazuri pia
 
Nimekulia dar ... kazi niko mkoa ila kila nnapokuja dar nashindwa kuinjoy maisha mambo ya foleni nshasahau so kila nikija huko napata tabu sana japo ndo nyumbani ila sikai zaidi ya wiki narudi zangu mkoani

Dar imenifunza akili nyingi na hasira ya maisha so huwa nakuja kufanya reflection tu then hasira nazihamishia mkoani huko..

Dar kwa sasa siwezi kuishi kabisa ni kusalimia ndugu tu naosha
 
Kuishi dsm lazima uwe kichaaa.

Binadamu wa kawaida hawezi kuishi hili jiji.

Mkandamizo wa hewa, uchafu, joto, kila mtu ana hasira anafuta jasho ,maisha flani ya kishetan kabisa.

Dsm haifai kabisa, NILIKUWA NAOMBA IBOMOLEWE.
Mkuu[emoji2960][emoji23][emoji23]
 
Uzuri wa dar kupata pesa sio kazi kama huko mikoani kwenu.
Mtu kushika hela kwa tabu sana mikoani mpka msimu wa mavuno.
 
Uzuri wa dar kupata pesa sio kazi kama huko mikoani kwenu.
Mtu kushika hela kwa tabu sana mikoani mpka msimu wa mavuno.
Mkoani kuna pesa sana halafu life lipo normal vyakula vizuri bei za kawaida, nyumba nzuri bei za kawaida chumba 25000, thelathini twende kwenye mbususu acha kabisa ni za kumwaga sasa maisha ya hapa Dar ni ya kingese sana naishi room ya 80000 mijoto mitupu, mbususu zinatumia pesa nyingi unajikuta unafuta namba kila kukicha yaani namalizia mishe zangu nikaendelee kula maisha kistaarabu kwenye jiji la miamba kwenye sato wengi saaafi kwaa, mtu mwenye mpango wa kuhamia Dar hasa kikazi hamna cha maana huku vinginevyo take home isipungue milioni kidoogo uta survive otherwise njoo ule bata rudi zako mkoa.
 
First tym naingia Dsm kutokea A town, nikiwa kwenye lift ya gari la watu, nafika pale bagamoyo tu ghafla naona hali ya hewa imechange kama hewa imekuwa nzito fulani hivi alafu nikasikia harufu kama bahari hivi yenye ushombo wa samaki nukajisemea sasa kweli hii ndo daslam niliyokuwa naisikia au kuiona kwenye runinga, Nikajiombea kwa Mungu wangu mji huu ukawe wa baraka kwangu Amen, now naelekea kula Christmas ya 5[emoji16] nimeshakuwa mwenyeji sasa.... Kuhusu level of life bado naweza sema nipo normal Ila najitegemea kimaisha, naweza kujilisha,kujivesha na kujitibu maana nilikuja sina hili wala lile nikatulia kwa ndugu, nilikuwa na miaka 17.... Lengo la kuandika hivi ni kusihi tu kuwa Ukimshirikisha Mungu popote unaishi poa tu.
 
Wa mikoani bana shida sana!!! hata mie niliambiwa hivhivi lkn nikadhamiria moyoni hukohuko kwenye joto ndo napataka!! kweli bana joto kali hatare!! kuuumbe kuna sehemu ziko poa sana utadhani siyo Dar km

sala sala mawee!! kwa wabarikiwe weee ni utakaa chini baridiiiii mkoani hapafai! Mabibo mbona fresh tu!!

lkn pale kipawa ni bonde la mpungua lile . sinza, Manzese mwee! magomeni hayo yalikuwa ni mabonde ya mipunga watu wakajenga
 
Kuishi dsm lazima uwe kichaaa.

Binadamu wa kawaida hawezi kuishi hili jiji.

Mkandamizo wa hewa, uchafu, joto, kila mtu ana hasira anafuta jasho ,maisha flani ya kishetan kabisa.

Dsm haifai kabisa, NILIKUWA NAOMBA IBOMOLEWE.
Nakumbuka 2011 mara ya kwanza nakuja Dar, nikakuta mlemavu amekaa kwenye vibaiskeli vyao anauza leso akawa amegeukia pembeni. Nikamuita brother huku nimemgusa begani. Aiseee, niliogolea matusi kweli siku hiyo. Eti kwanini nimemgusa begani wakati namuita? Siku ile ningepata kesi ya mauaji ila jamaa yangu akaniambia, huku Dar kila mtu ni kichaa. Toka siku ile nikijaga huko Dar, simgusi wala muongelesha nisiyemjua.
 
Ni pesa tu ndgu yangu wala jiji sio baya kiasi hicho.

Kuna watu hawayapitii hayo maswahibu unayopitia wewe.

Ila kama una kipato cha kuunga unga ushauri wako ni mzuri sana.
 
Watu wanatucheki mitandaoni tunavyoflex basi wanaona maisha ndo yalipo wakija wanaanza lawama
 
Back
Top Bottom