Unajua ni kwanini? Huwa hatupigi hesabu ya faida tunayopata tunaangalia anachopata mwingine na kama ni kikubwa bora biashara ife au malalamiko yanaanza.
Mtu anaweza jenga nyumba kwa thamani ya m10, akasema anaiuza m15. Huyu ataridhika kabisa na hiyo m15 ikipatikana ila dalali atakapoleta mteja wa m35 na kumwambia achukue 15 zake nyingine azitoe biashara inaweza kufa. Sababu ni hajaangalia tena 15, ameangalia anayopata mwingine.
Mfano hapa, mtu analalamika gharama ya laki tatu kwa mwaka ni kubwa mno ila hapigi mahesabu hiyo laki nne anayokaa nayo inaweza kuzalisha kiasi gani ili apime kama laki tatu ni kubwa au ndogo, yeye kaangalia tu hiyo laki tatu.
Jiulize huo ukubwa wa laki tatu unaolalamikiwa umepimwa vipi?