Usijizime data! Wewe kama ni msomi unaijua fika kuzimu hile ya Biblia ikoje!

Usijizime data! Wewe kama ni msomi unaijua fika kuzimu hile ya Biblia ikoje!

Morning_star

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2018
Posts
6,042
Reaction score
17,320
Utangulizi: Katikati ya kiini cha dunia kuna joto kali sana, na halijoto ni kuanzia 7200–9000℉ (4000–5000℃) linasababisha kuungua na kufanya uji wa mawe, miamba na madini magumu kama nickel. Hapa kwenye kiini (core/mantle) kuna joto lenye shinikizo (pressure) kubwa kiasi cha kuweza kutoka nje ya uso wa dunia na kulipuka kutengeneza miamba na milima ya volcano.

1. KUZIMU ndo hapo juu nilipopaelezea. Sasa hapa ndo kuzimu ambapo nafsi na roho za wenye dhambi hutupwa au zitatupwa siku ya hukumu.
Wanadamu tunaishi juu ya uso wa dunia na panaitwa duniani. Juu ya uso wa dunia kuna anga. Kwenye anga ndiko penye mawingu kunakotoka mvua, juu ya anga kuna mbingu; kwenye mbingu ndiko kuliko na mfumo wa sayari na jua na pia ndiko kilipo kiti cha enzi cha shetani ,(mfalme wa uweza wa anga, "Efeso 2:2"). Juu ya mfumo huu juu sana kilometers nyingi zisizoesabika ndo mbinguni anapokaa Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.
Kutoka uso wa dunia kwenda kuzimu kwenye moto ni kilometers 6,378. Ni umbali kama wa kutoka Tanzania mpaka Ufaransa (kama utanyoosha). Sasa kutoka hapa katika uso wa dunia na kuzimu kuna makazi ya kila aina ya viti vya enzi vya mashetani/na mapepo kwasababu ufalme wa shetani umefitinika. Yako mataifa hayamjui Mungu wa Biblia lakini yanaendesha maisha yao na yana nguvu kwa kutumia aina fulani ya miungu inayokaa katikati kuelekea kuzimu. Sasa hawa wachawi wanaotunishiana misuli katika ulimwengu wa wanadamu inategemea wanapata nguvu kutoka ufalme wenye kiti kipi!. Huyo Baba lao (Ibilisi/lucifer) kiti chake cha enzi cha kuongoza ufalme wake kiko kwenye anga kwenye mfumo wa jua, mwezi na sayari na uingia maagano na mashetani mengine ambayo nayo yana ufalme wao humu duniani kutokea kuzimu nilipopataja!
Sasa sikia, Mungu wa Biblia ni Mungu wa haki halazimishi umfuate lakini kwa vile ndiye aliyeumba mbingu na nchi na kila kitu, alitengeneza mifumo ya kuwezesha mwanadamu achague kati ya chema na kibaya. Kwa mfano, katika kitu chochote hapa duniani kina ulinganifu wake kwa upande mwingine: mfano: utii na uhasi, nuru na giza, juu na chini, haki na dhuruma, kiangazi na mvua, upendo na chuki, umasikini na utajiri, nk, nk,. Sasa binadamu alipewa akili ya kuchagua. Uchaguzi unaoufanya kama binadamu ndio unaotengeneza mustakabali wa maisha yako. Sasa ufalme wa shetani ni ufalme wa uhasi. Ni ufalme uliofitinika! Hata makuhani wa shetani hapa duniani ambao ni waganga wa kienyeji na wachawi na wao pia wamefitika. Hata hawa wanaojiita watumishi wa Mungu wanajifanya wanahubiri neno la Biblia wanaendaga kuzimu kupewa upako wa kujenga ufame wa kile kiti cha enzi cha yule au hile roho chafu. Na haya mambo ni dhahiri kabisa katika dunia hii ya maisha yetu ya kilasiku tunayoishi. Majirani, ndugu, jamaa na marafiki na kila sekta ya kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni lazima iwe na roho nyuma yake ya kuwezesha binadamu aishi na kufanikiwa. Sasa hapa ndo tunatambiana katika mlengo wa kufanikiwa kimaisha na kusema (mungu kanibariki). Kwa wenye akili tunajua kwa matendo yako tunajua ni mungu yupi??
Sasa nashangaaga watu tunajizima data na wengine kujiita "atheist" na kwamba hakuna Mungu. Hao ni waongo labda waseme mungu wanayemuabudu mbona wengine hawamjui? na wangependa na wengine wamjue!. Sasa wakija tukawaambia Mungu wa Biblia ambaye ndo Baba lao wanasema "huyo hayupo" Atheist Bwana!!!
 
UMEKWAMA MAENEO MENGI SANA.UFAHAMU WA BIBLIA BDO KWAKO
 
Back
Top Bottom