Ruksa kumbaka mkeo? Kwani kuna tofauti gani kati ya kumbaka mkeo na kumbaka mwanamke asiyekuwa mkeo? Naona kama hakuna tofauti. Lakini sheria zetu zimekuwa kimya juu ya ubakaji ndani ya ndoa. Whether or not ni ruksa kumbaka mkeo inategemea unambaka ukiwa nchi gani. Hii ni kwa sababu ubakaji ndani ya ndoa ni kosa la jinai kwenye nchi nyingi. Baadhi ya nchi hizo ni Argentina, Australia, Austria, Barbados, Belize, Bulgaria, Canada, Croatia, Cyprus, Denmark, Ecuador, United Kingdom, the Fiji Islands, Finland, France, Georgia, Germany, Honduras, Hong Kong, Ireland, Israel, Macedonia, Mexico, Namibia, Nepal, the Netherlands, New Zealand, Norway, the Philippines, Poland, South Africa, Spain, Sri Lanka, Sweden, Taiwan, Trinidad/Tobago, US, Uzbekistan, na hata Zimbabwe.