Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,831
- 5,489
Ni mwaka 1964 usiku mmoja hivi, wanaume wanne weusi walikutana ndani ya chumba kimoja na kuanza kuzungumza. Usiku huo ulikuwa mkubwa kwa Wamarekani weusi, haikuwahi kutokea watu wa namna hiyo mpaka leo hii kukutana na kuzungumza.
Watu hao walikuwa maarufu duniani, watu hao hata baada ya kufa waliacha alama kubwa sana kwenye vitu walivyokuwa wakivifanyia kazi. Nikwambie tu kwamba ulikuwa usiku mmoja wa kukumbukwa sana ambao ulipewa jina na kuitwa One Night in Miami.
Usiku huo uliwakutanisha vijana machachari kipindi hicho. Alikuwemo mwanamasumbwi, Muhammad Ali, alikuwemo Mwanaharakati, Malcom X, mwanaharakati, Jim Brown ambaye pia alikuwa maarufu kwenye mchezo wa Footbal (Ule wanaovaa element katika ligi ya NFL) na wa mwisho alikuwemo mwanamuziki Sam Cooke.
Kwa kipindi hicho hao watu walikuwa maarufu mno. Malcolm X alikuwa akiwapambania watu weusi, aliwaunganisha kwa pamoja na alikuwa akililia uhuru kwa watu hao kila siku.
Aliweka mikutano mingi, alizungumzia uhuru wa watu weusi. Kwa kipindi hicho ndicho ambacho Wazungu walijuta kwa nini waliwapeleka watu weusi nchini Marekani. Walikuwa wakizaliana na kwa kipindi hicho waliamua kuupambania uhuru wao.
Ni usiku huo ndiyo ambao Malcolm X alimwambia Muhammad Ali abadilishe dini kutoka Ukristo na kuingia Uislamu. Alichokuwa akikisema X kila siku ni kwenda tofauti na Biblia, yaani kama Yesu alisema ukipigwa kofi shavu la kulia geuza na la kushoto, alisistiza kwamba kwenye Uislamu hakuna hilo, mtu akikupiga, unatakiwa kurudisha, unatakiwa kupambana.
Wamarekani wengi weusi walimuelewa sana jamaa, na yeye ndiye alichochea weusi wengi kuufuata Uislamu. Akanzisha makundi ya Kiislamu na mengine mengi. Ali aliambiwa abadilishe dini, akakubali ila akasisitiziwa atangaze baada ya kuwa bingwa wa dunia kwani kama angejitangaza kabla ya kuwa bingwa, angefanyiwa fitina nyingi na asingefanikiwa kuwa bingwa.
Na kweli, baada ya kuwa bingwa wa dunia, akatangaza kuwa Muislamu, akabadilisha jina kutoka Cassius Clay mpaka Muhammad Ali. Kwa kutangaza hivyo ni kama dunia haikuamini kilichokuwa kimetokea, ilikuwaje jamaa abadilishe dini? Kwa nini yaani, lakini msisitizo wake ulikuwa huohuo kwamba hakutaka kuwa Mkristo tena.
Kwa Sam Cooke naye aliambiwa abadilishe. Yaani usiku huo ulikuwa ni wa Malcolm X kudhamiria kuwabadilisha dini majamaa hao kwa kuwa aliamini kwa kufanya hivyo basi watu wengi weusi wangeifuata dini hiyo.
Kwa Sam Cooke na Jim Brown walikataa kwa kuwa walilelewa kwenye misingi yote ya Kikristo na walijua ukiwa Muislamu utatengwa hata na baadhi ya watu weusi wenzako, hutoweza kuwa maarufu kama ulivyo, na kubwa zaidi hutokula tena mademu wala kunywa pombe kama ilivyokuwa kwa Malcolm X, wakakataa kishenzi, tena Sam Cooke alikataa huku kwenye chumba kingine akiwa na watoto wazuri.
So kwa watu ambao hawakuwa wakifahamu kuhusu harakati kubwa za Malcolm X unatakiwa kufahamu kwamba mchizi alikuwa na harakati kwa pande mbili, Uislamu na kuwatetea watu weusi. Alifanikiwa kwa asilimia kubwa kabla ya kuuawa.
Hakupendwa na Wazungu, hakufagiliwa sana na weusi wengine kutokana na harakati zake za kidini tu, ila alisapotiwa na watu wengi maarufu.
Huu ulikuwa ni usiku wa kipekee sana, hata ukiangalia muvi yake iitwayo One Night in Miami utainjoi sana. Ni usiku abao umekaa vichwani mwa Wamarekani weusi mpaka leo hii.
Yakumbuke majina hayo. Muhammad Ali, Malcolm X, Sam Cooke na Jim Brown.