Usiku wa mabingwa wa ndondi: Wabongo wawachakaza vikali Wamalawi

Kiukweli nimeshangaa jamaa amepiga haswaaa!!!
Yani Marefa waliposikia tu Rais na Waziri Mkuu wanawatch game nikajua watapendelea sijui wamfurahishe nani sasa.Yaani aibu kwelikweli.​
 
Kuna Uzalendo na Upumbavu kilichotokea kwa Mmalawi dhidi ya Mfaume ni dhulma. Tujue kutofautisha kati ya haki na Uzalendo.

NB: Au waweke sheria mpya mgeni ni lazima ashinde kwa KO katika ardhi ya Tanzania maana kwa points majaji wetu ni wazalendo sana kamwe hawawezi kushinda.
 
Ujinga tu, ushindi gani Mfaume kaupata? Umewahi kuona ushindi unaanza kutolewa ufafanuzi? Sirudi tena kwenye kuangalia ngumi bora ningelala tu. Ukumbini ulikuwa kimya mwanzo mwisho japo alikuja na watu wengi, walibaki wameshika tama tu, hizo hela agawane na majaji
 
Mzimbabwe alianza vizuri sema punch zake hazina nguvu.
Galiatano movement zake ziko poa huchoki kumwangalia sema punch zake bado hazina uzito wa kumkalisha mpinzani. Movement za Galiatano safi sana u anatamani pambano lisiishe.​
Yeah yule asingepata timing ingekuwa shida yuko well organised
 
Tanzania ni nchi ya Hovyo sana ,
Tunalazimisha uzalendo wa kipumbavu kwa kudhurumu haki ya mtu mwingine.
 
Kiukweli nimeshangaa jamaa amepiga haswaaa!!!

Na Hii ndio sababu michezo ya Kitanzania haifiki mbali. Kwanza Mfaume Sio Professional and Strategic. Inaelekea amejifunza ngumi kwenye Viroba vya Mchanga na Matairi.

Yule Mmalawi ameshinda na hata 90% ya sapota wa Mfaume walikuwa wameshaanza kuondoka wakijua Mshind ni nani.

Mmalawi ameshinda idara zote. He is tactical, Observer and Professional. Japo alijua yeye ndio Mshindi, lakini wala hajamaindi Mfaume alipotangazwa.

Shida Watz hatujui kuwa dunia inatizama na hii inatuathiri kwenye international games . Hata majaji wetu watabaki kuwa majaji wa hapo hapo ; hawawezi kupanda kimataifa, they are stupid and ignorant. Hawathamini kazi yao kwa vi laki 3 wanavopewa kama Hongo. Ni ujinga.

Tutaishia humu humu. Haiwezekani mtu ashinde obviously na usimtangaze kisa game imechezwa kwenu —— SHAME ! And the worst part ni kwamba tunajiharibia wenyewe kimichezo.

Na hiyo Simba safari yake ya mwisho iwe Benjamin Mkapa . Hatuwezi kushiriki michuano ya kimataifa. We are not serious.
 
Yaani hadi nilijihisi aibu kuwa mtanzania kwa kile alichofanyiwa yule Mmalawi!
Usengelema mtupu!
 
mzimbabwe kapigwa na Tony Rashid from Tanzania
 
Mkuu hapo kwenye Simba ndi umeharibu. Uko ki utopolo zaid. Anyways umeingea points in general. Ukumbi ulikua kimya na wasiwasi mwingi kumaanisha mfaume kapigwa. Nilishangaa kwa kweli the other way round.
Kama ingalikua si pambano na mkanda baasi labda labda tungeiita draw.
 
Wachambuzi Ibrahim class na wenzie walishakosa cha kusema. Alafu hata Galiatano, mpinzani wake alishamuweza zamani. Ila ndio hivyo.. bora zile K.O tuliziona waziwazi
 
Yani watanzania tunazingua haiwezekan mtu kapigwa roundi zote halafu yeye anaibuka kuwa bingwa.
Kwa halii hii hatuwezi kufika mbali "Mfaume"
 
Mabondia wote wamecheza vizuri isopokuwa.
Mfaume na Galiatano.
Mgumi zao ni nyepesi sana, na sio za Professional Boxing.
Huyu Mfaume huwa anatamba sana na wapambe wake wanamsifia kuwa ndiye mwenye mgumi nzito zaidi katika uzito wake, hadi aliwahi kumpasua bondia mwenzake fuvu la kichwa.
Mfaume Huenda kalewa sifa, huku watangazaji waliendelea kumsifia eti amefanya mazoezi mengi mazito hadi anashindwa kurusha ngumi nzito, utadhani hana kocha.
Galiatano na Mfaume lazima wajifue zaidi kama unataka kuendelea na Boxing.
Galiatano alicheza round mbili tu kachoka hoi, anabaki anazunguka tu na kudokoa dokoa vi jab huku anakimbiakimbia ulingoni. Mpaka mpinzani wake anasimama na kumwuliza vipi huonekani. Mwisho akaamua ampigie saruti kabisa.
 
Sasa simba inaingia vipi kwenye boxing, ? Nenda kashabikie barcelona ndugu
 
Hahaaah galiatano alikua kama kipepeo
 
At least Galiatano kidogo alimpiga mpinzani wake akapata pointi nyingi raundi za mwanzo. Ila Mfaume Mfaume kadundwa wazi kabisa. Aliingia kwenda kulazimisha KO tangu raundi ya kwanza. Japo hiyo mbinu yake ilishindwa kufanya kazi toka mwanzo hakuwa na mbinu mbadala matokeo yake kila akipiga ngumi moja ya usoni yenye pointi jamaa anarudisha hapo hapo tatu. Naona majaji walikuwa wanachukua pointi za Mfaume wanampa mmalawi na za mmalawi wanampa Mfaume. Kiufupi Mfaume alipigwa kwa pointi nyingi sana kiasi ilihitijika moyo wa chuma na uso usio na haya kumpa ushindi na kumnyima mmalawi

Niwapongeze sana Azam kwa kurudisha hamasa ya mchezo wa ndondi nchini kwani mimi ni mmojawapo ambaye kila nikisikia kuwa ngumi huwa nawahi nyumbani kuangalia mapambano mwanzo mpaka mwisho hata kama saa kumi asubuhi. N ahuu mchezo umeshaanza kutoa ajira kwa vijana wengi Dar es salaam. Lakini majaji wanataka sasa kuurudisha mchezo wa ngumi shimoni tena. Ombi langu kwa serikali iingilie kati ili yaliyotokea ya maamuzi ya upendeleo kwenye pambano la Mfaume yasijirudie tena. Serekali ikiusimamia huu mchezo wa ngumi vizuri kwa kushirikiana na wadau kama Azam na mapromota mbalimbali nina hakika ndani ya miak hii miwili utakwenda kutoa ajira kwa vijana wengi kama ulivyo mpira wa miguu kwa sasa. Kwa mwelekeo uliopo ngumi zinakwenda kurudi enzi za akina Koba Kimanga, Emmanuel Mlungwa, Issak Mabushi, Nasoro Michael na wengineo wakati uo ngumi zilikuwa moto kweli kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…