Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Usije ukakurupuka huko baada ya kula zako Ugali matole, au mkande yako ya kisamvu ukaanza kujifanya mtetezi wa HAKI za Watanzania.
Kabla hujafanya hivyo ni muhimu kujiuliza, je ninaoenda kuwatetea HAKI zao wanahaki ya kutetewa? Yaani wanastahili kutetewa?
Mtu yeyote ambaye hahitaji kutetewa huyo huna HAKI ya kumtetea. Hustahili kumtetea.
Mtu ambaye hahitaji utetezi alafu wewe ukamtetea huyo ni kama nyoka mwenye sumu Kali. Nafikiri unaelewa nini hutokea unapoenda kumuokoa nyoka aliyekwenye Hatari.
Sio kila mtu anayeonewa anahitaji utetezi.
Wapo wanaostahili kuonewa. Yaani wapo watu ambao ni HAKI yao kuonewa. Haki ni kitu kizuri Sana lakini kwa upande mwingine HAKI ni mbaya Sana.
Yaani kuna mtu mtu anaweza kumwona anateseka kumbe yeye anaona hateseki. Hivyo hahitaji msaada wako. Hahitaji utetezi wako. Na endapo ukifanya hivyo wewe ndiye utaingia kwenye matatizo makubwa.
Hivyo ndivyo Watanzania wengi walivyo.
Usijiingize kwenye matatizo Kwa lengo la kumtetea mtu asiyestahili kutetewa. Hiyo Sio HEKIMA.
Ukiona kundi kubwa la watu linaonewa na kundi dogo basi elewa hapo huna haja ya kutetea HAKI za kundi kubwa linaloonewa kwa sababu hao wanastahili kuonewa.
Yaani haiwezekani watu Mia wawaonee watu milioni Moja alafu wewe uje utetee hao milioni Moja.
Ila ukiona watu milioni Moja wanaonea watu elfu Moja basi unaweza kutetea hao elfu Moja. Hiyo ni HAKI.
Acha nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam