Usilazimishe JF ya 2026 iendelee JF2006 kila kizazi na nyakati zake

Usilazimishe JF ya 2026 iendelee JF2006 kila kizazi na nyakati zake

Kwahiyo unataka tuchangie mawazo kwenye nyuzi ya "Demu wangu nimempigia simu hajapokea?" na Kuacha mijadala mikubwa ya Katiba Mpya ,Kupinga utekaji ,tanzania kunyimwa misaada .tunapigwa chini jumuiya ya madola?
Kama sio mikato yangu,na sio lazma uchangie
 
Naona nyuzi nyingi zikikosolewa na kupuuzwa eti "JF imevamiwa,ooh watoto wa FB,mara vitoto vya 2000 hivi" hizo ndio akili za mwafrika,akili zimelala,hazitaki mabadiliko.

Kwa hiyo nyie wazee au wakongwe hamtaki JF ikuwe? hamtaki iwe na kizazi kingine? Au mna maanisha nini?
Facebook ya 2005 sio ya sasa
Mziki wa bongo flava wa 2000 sio wa sasa
Dunia ya 1990 sio dunia ya sasa
Vipindi vya radio na TV vya zamani si vya sasa
Watangazaji wa zamani si kama wa sasa.

Usipobadilika kulingana na nyakati utateseka sana. Kwa hiyo mnataka kizazi cha JF 2006 kiendelee kuwa kile kile,kama kikifa chote? Na mtandao ufe? Ni mtazamo mbaya sana,jamii forum ipo kwa ajili ya jamii zote.

USIBISHANE NA NYAKATI UTAUMIA BURE
Naunga mkono hoja.

Kila zama na zama zake.
Chapeni kazi Gen Z
 
JF ya miaka ile tulikuwa tunaingia kutafuta programs za computer za uhakika kwa free, vitabu vikali, ushauri mzuri na msaada katika ngazi mbalimbali hadi serikalini na ngoma kali mbalimbali ambazo huwezi kuzipata hata youtube. Lakini sasa hivi ni tofauti ni vijembe tu, umbeya na umalaya ndo vimekithiri.
Hapana huu ni uongo.

Hebu leta uzi kudhibitisha hilo...
 
Back
Top Bottom