Usipo enjoy maisha yako ukiwa chuo basi tena hutokaa ule raha zisizo na stress maishani. Chuo ndo sehemu ya kupiga bata mpaka kuku waone aibu. Kazi yako iko well defined : Kuattend lectures, kuattend seminars, kufanya assignments na mitihani.
Sasa usipokula raha hapo unasubiri hadi uje mtaani, uanze kulipa kodi ya nyumba, nyumbani wakutupie wadogo zako kadhaa uwalipie karo, hapo una ka girlfriend na kichango ya harusi kibao. Waacheni watoto wa chuo wakaramke, wajiachie, wajipe rehersal ya maisha ya mtaani. Haya mambo ya kutaka washinde library halafu wakiingia mtaani mnawacheka na mashati yao ya kariakoo na suruali za lesi lesi ni mbaya sana.