Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Unapovuka daraja na kwenda upande wa pili basi usilivunje hilo daraja kwakuwa tu umevuka upande wa pili,huenda kuna siku ukahitaji kuvuka daraja hilo hilo tena na tena,kwani maisha yana njia zake zisizo tarajiwa
Unapofanikiwa katu usiwasahau walio bado kitaani endelea kujenga mahusiano mazuri nao kwani huenda kuna siku ukajikuta unawahitaji kwa namna moja au nyingine,unapokuwa juu vile vile usiwasahau walio chini yako kwani huenda likawa daraja ambalo huenda siku moja ukahitajika kulivuka kwenda katika mafanikio
Napenda kutoa mifano,kama miaka minne iliyopita wakati nipo kampuni fulani nilifahamiana na jamaa fulani ambao walikuja kwenye kampuni yetu kama washauri,niliwapokea vizuri na wakafanya kilicho waleta,sikuvunja daraja baada ya wao kuondoka kwani tuliendelea kuwasiliana hapa na pale
Leo hii daraja lile ambalo sikulivunja nimejikuta nalivuka tena na leo wale jamaa ambao walikuwa washauri wa kampuni yetu ndio maboss wangu wapya mpaka mda huu ninaoandika huu uzi,walinitafuta na sasa nafanya nao kazi
Hii yote imetokana na kutovunja daraja ambalo leo nimejikuta nalipita na kuvuka ng'ambo ya pili,haijalishi upo katika nafasi ipi na neema ipi,hakikisha hauvunji daraja ambalo huenda ipo siku moja litakuwezesha kuvuka upande wa pili na kwenda nchi ya ahadi
Ni hayo tu