Mafian cartel
JF-Expert Member
- Nov 19, 2021
- 3,876
- 7,118
Nasubiri sehem ya kumi na nne
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ahsante sana mkuu. Stori tamuSEHEMU YA KUMI NA TATU
Ilipoishia,,,,,,,,,,,,,
Basi chuma ikaamsha taratibu, Sity akawa analikimbiza gari paka likatoka nje ya kituo, Basi gari ikakamata morogoro road, Sity tukamuacha kasimama tu pale kaduwaa gari inaondoka, Basi chuma ikaamsha Arusha moja hiyo
Endelea,,,,,,,,,,,,,,,,
Chuma ikawa inatambaa balaa, safari imeshika kasi, watu naona wana mzuka kinoma na safari, naona kama wana enjoy, tofauti kabisa na mimi, sina raha, mawazo kibao, pembeni nimekaa na mtoto mzuri wa kichaga lakini sina hata time nae ( Nilijua ni mchaga baada ya kusikia akiongea na simu kichaga),
Nipo zangu kimya sina story na mtu mara simu ikaita, kucheki nikakuta ni Sity anapiga, nikapokea, Akauliza tumefika wapi, Nikamwambia tupo mbali sana, maana hata maeneo mi siyajui huko njiani, Basi akasema yeye kalala anahisi kama anaumwa vile, nikamwambia aende basi akachek maleria, akasema wala si maleria , ni mawazo tu anawaza ataishi vipi bila mimi, Ana feel upweke hadi anaumwa, Nikamwambia tuombe Mungu tu mambo yakikaa fresh tutaonana soon, basi tukaingia porini porini huko hakuna network simu ikakata,
Basi safari ikaendelea, mara nikapitiwa na usingizi nikalala sana, Kuja kushtuka nakuta gari imesimama watu wanashuka, nikamuuliza yule dada wa kichaga, dada hapa wapi, Akasema Mombo watu wanashuka kwenda kula, kucheki saa ni saa saba, kwenye simu kuna miscall za Sity kama zote, Nikampigia, Akasema mmefika wapi, nikamwambia ndo tupo mombo sehemu ya kula panaitwa Liverpool, Akauliza, we umekula, nikamwambia mi hata hamu ya kula sina, akanibembeleza na kunisihi sana, kwamba nikienda kula hata yeye atapata faraja,
Basi nikaona isiwe shida, nisije nikamuudhi mtoto mzuri bure, nikashuka nikaenda toilet, nikatoka nikaenda kununua sambusa mbili za nyama na soda nikarudi kwenye gari nikatulia,
Basi watu wakarudi gari ikaamsha, tukafika moshi mjini kama saa kumi hivi, Basi likaingia stendi, wenye kushukia moshi wakashuka, Wakapanda wengine wanaoenda Arusha, Basi likakaa pale kama nusu saa hivi hatimae likaondoka, safari ya kuelekea Arusha ikaanza,
Tukafika Arusha kama saa moja hivi usiku, Nikashuka pale kama mtu anaejua anapoenda vile, ili machalii ya r yasije niona wakuja yakanidandia maana stori zao nnazo,
Basi nikazunguka zunguka pale stand mwisho nikaamua nikae kwenye vile vibanda vya abiria, Pembeni kuna mama mmoja kaweka vitu vyake pale anauza chakula, Nikamsalimia yule mama, nikamuuliza eti kiwanda cha nguo kipo maeneo gani, akasema kipo kisongo kinaitwa a to z, nikamuuliza ni mbali kutoka hapa, akasema ndio, ni nje ya mji, unapanda kihiace ( daladala) nauli mia tano, Nikamuuliza hivyo vihiace vipo hapa, akasema inabidi uende standi ndogo inaitwa kilombero, huko ndo kuna vihiace vinavyoenda nje ya mji, basi akanielekeza ilipo hiyo stand, ila nikaona hata nikienda saivi ni usiku ntapata shida tu huko, ni bora nitulie tu pale stand paka kesho asubuhi ndo nianze hizo mishe,
Basi nikatoa simu nikampigia Sity nimjulishe nimefika salama, tukapiga stori pale kidogo basi tukamaliza,
Pale stand abiria wanaolala pale ni wengi tu, wanaotoka maeneo ya mbali ambao wanasubiri magari ya alfajiri sana, basi nikawa sina wasiwasi,
Muda ulivyoenda nikaweka begi langu kama mto, nikatia mbonji pale kwenye benchi, ila nikawa nalala kwa machale, kila saa nashtuka shtuka wasije machalii ya r wakapita na mimi,
Basi asubuhi ikafika, nikaenda kwenye kamgahawa flani hivi nikaomba maji nikanawa uso, nikapiga chai pale fresh, Nikatoka nikashika njia kuelekea stand ya kilombero huku naulizia maana ni mbali kidogo,
Kufika pale daladala kama zote, basi nikaskia kisongo kiwandani!!, Kisongo kiwandani!!, Basi nikajua ndo hii na hicho kiwanda itakiwa ndo hicho cha nguo, basi nikazama ndani, badae kikajaa hicho kikaamsha,
Basi tukatembea weeee tukatoka nje ya mji kabisa, tukafika sehemu tukakata kushoto tukatembea kiasi hivi mara nikaskia wale wa kiwandani!!, wale wa kiwandani!!, basi tukashuka, abiria wengine wakabaki gari hiyo ikageuza tulipotoka,
Basi pale ndo kiwandani, kuna geti kubwa na walinzi hapo nje, sema geti ni la nondo kwaiyo ndani unapaona, ila ndani tena kuna geti jingine huko ndo huwezi kuona maana geti si la nondo,
Basi pale nje kuna maduka na vibanda vingi tu, Nikajivuta kwenye kibanda kimoja nikanunua soda nikakaa nakunywa huku nasoma mazingira, nikajaribu kumuulizia jamaa pale kuhusu chance za kazi pale kiwandani, akasema pale kila ijumaa wnakujaga hapo getini wanachukua watu, nikapiga hesabu siku hiyo ilikuwa jumatano,kwaiyo inabidi nisubiri paka ijumaa ndo nije,
Basi nikajaribu kumuulizia kuhusu wale jamaa zangu kama anawafahamu lakini wapi, basi nikakaa sana pale paka jioni wafanyakazi wakaanza kutoka, aisee!! ni wengi kichizi, basi nikawa nawaulizia kama wanawajua wale jamaa zangu ila hakuna hata mmoja anaewajua, Nikasema sasa hapa kazi ipo.,
Basi kigiza kikaanza kuingia, hapa sasa nitafute pa kulala, mfukoni nna kama elf 60 hivi na machenji, nikaulizia gest maeneo yale nikaambiwa gest paka kisongo,
Basi nikachkua boda pale buku paka kisongo, nikaulizia gest pale nikaelekezwa gest moja maeneo yale, nikafika nikaulizia chumba nikaambiwa single elf 5 nikasema fresh, basi nikapewa chumba nikaeka begi langu nikaenda kuoga, nikatoka nikaenda kucheki msosi huko road,nikala nikarudi zangu room, nikajilaza kitandani nikampigia Sity tukaanza kupiga story,
Itaendelea
Kwamba ni uongo ama vipi😆😆😂😂... Sity akawa analikimbiza gari paka likatoka nje ya kituo, Basi gari ikakamata morogoro road, Sity tukamuacha kasimama tu pale kaduwaa ...
Wachache sana wanaweza kuelewa.maisha unayosimulia ni uhalisi kabisa watoto wa mama tu ndio watasema chai...mimi binafsi niliishi maisha hayo baada ya kumaliza chuo naliona elimu yangu ni bure kabisa nakumbuka vizuri nilikuwa hata natamani niwe konda niliona konda anamaisha kuliko mimi na nilikuwa mbali na nyumbani kama wewe mkuu acha kabisa nilikuwa nanunua mkate ule mkubwa nakula huo huo hata siku nne nisife tu, nimelala bila kula hata kwa siku mbili mara nyingi sana, nikipata unga ni ugali tu then maji nalala nilikuwa naongea mwenyewe kama chizi na kucheka kabisa..wanaume tunateseka sana...kipindi hicho unakaa hata miezi minne hakuna simu unapokea na sikuwa na mwanamke yoyote nilipambana ile kihard core..
lakini namshukuru Yehova hayo maisha yamekuwa historia taratibu lakini hayo maisha yamenifundisha kuja kuishi bila huruma kabisa yaani mtu akija analialia msaada namwaangalia tu wala sijali
Anajiita Akili sina we ulitegemea awaje. Akat hana akili.bora tu mpwayungu village yeye arudi tu hewani,story yake ilikuwa inatusisimua na kutuelimisha sana .....Ila huyu akili sina yeye anahaso lakini muda huohuo na yeye anawaza mbususu tu,kweli tutafika mwisho wa story akili sina atakuwa na watoto zaidi ya kumi
Mkuu amemaanisha passport size Na barua ya kiongozi wa mtaa wake sHapa tu ndio umekosea. Passport hauwezi kuipata siku hiyi hiyo...
Safi kabisa mkuu huwezi kuulizwa safari Ni Nini? Upo bar ukasema Ni kitendo Cha kutoka sehem fulani kwenda sehem nyingne kwa umbali kadhaaInategemea na muktadha sasa..., Passport ya kusafiria sio document common kihivyo hadi mtu aichanganye na passport picture, kwani huko kwenye interview aliyosema jamaa watahitaji passport ya kusafiria ya nini?
Mimi mara kibao nikishughulikia mambo yangu ofisi za serikali naambiwa inahitajika nyaraka kadhaa na passport, na kulingana na muktadha naelewa ni picha wanamaanisha
Mbona Mpwayungu alitaka kubaka!bora tu mpwayungu village yeye arudi tu hewani,story yake ilikuwa inatusisimua na kutuelimisha sana .....Ila huyu akili sina yeye anahaso lakini muda huohuo na yeye anawaza mbususu tu,kweli tutafika mwisho wa story akili sina atakuwa na watoto zaidi ya kumi
story lazima tuuziwe ila tunakolezwa kwanzaKak uwe makini Kuna lijamaa la twita huko linajita buyobe atakuaja kuiba hii story na kwenda kuuza huko telegrams. Kama alivyo iba story ya yoga huku wew ukiwa ujapata lolote story Ni nzuri Sana Bora ukaiuze tu kuliko kuleta huku bure
Fany kitu hi story uiuze upige pesa mambo ya bure bure ishapitwa na wakt
Ni hayo tu
daah....umenikumbusha Kiwanda cha A to Z ngoja niweke kambi ukute lbda hata nakujuaSEHEMU YA KUMI NA TATU