Usilogwe ukaondoka nyumbani na kwenda usipopajua kwa kigezo cha kutafuta maisha

Usilogwe ukaondoka nyumbani na kwenda usipopajua kwa kigezo cha kutafuta maisha

Nilizaliwa mwishoni mwa miaka ya themanini katika kijiji cha chabutwa wilaya ya Sikonge mkoa wa Tabora, nilifanikiwa kupata elimu yangu ya msingi hapo kijijini, shuleni nilikuwa vizuri sana, si walimu tu bali hata wanafunzi walinipenda. Familia yetu ilikuwa ya maisha ya kawaida sana kwani baba na mama wote ni wakulima wadogo wadogo tu, kwetu tulizaliwa wawili tu mimi na mdogo wangu wa kiume.

Basi baada ya kumaliza shule ya msingi nilichaguliwa kujiunga na shule ya skondari Chabutwa iliyopo pale katani. Kwa vile nilikuwa John kisomo basi maisha ya shule hayakuwa mabaya ki ufaulu, Paka namaliza form four nilikuwa naongoza pale shuleni, Baba yangu alipenda kunihusia kuwa nisipende kujionesha kwa watu kuwa nina akili maana si wote wanapenda kuona watoto wao hawafanyi vizuri alafu watoto wa wengine wanafanya vizuri

Basi nilijitahidi sana kufata ushauri wa mzee ingawa kama unavyojua haya mambo hayafichiki, Kata nzima ilikuwa inanifahamu, kwenye vikao vya shule ndo usiseme maana niligeuzwa sample space (Sehemu ya wengine kujifunzia).

Basi nikamaliza four pale na Mungu si Athumani nikafaulu vizuri na kuchaguliwa kujiunga na shule ya Pugu Secondary kwa ajili ya five na six. Mzee wangu alifurahi sana si kwa sababu ya kufaulu tu bali nilichaguliwa shule ya mbali na pale nyumbani maana mzee alikuwa hana amani kabisa na majirani wa pale katani

Basi bana, siku ya siku nikatimba shule ya baba wa taifa, Askwambie mtu nilikutana na life la kibabe sjawahi kuona
Picha linaanza shule haina maji, Maji utajua pa kuyapata, kama utaenda mtaani kununua utajua mwenyewe, Ukitaka uzame pondi ( Huko bondeni kuna visima wanatumia wanakijiji ila maji yake yana magadi na fangasi wa kutosha)

Kufupisha story sitaelezea sana life la Pugu, ila kiukweli lilikuwa la kiume, Miongoni mwa vitu sitavisahau ni bweni letu la Mapinduzi 3 ambalo ndo lilikuwa linaaminika bweni la watu wakorofi shule nzima, pia nikiwa bado mgeni nilikaribishwa kwa kupigwa nguo zangu zote nikabaki na nliizokuwa nimevaa tu, yaani siku hiyo nimetoka pondi nimefua nguo zangu nikaanika kwenye ukoka, nikaondoka kwenda kutembea majohe, kurudi jioni nakuta ukoka unanikodolea tu hakuna nguo yaani Hadi boxer walichukua wahuni wale.

Kingine sitasahau ni tukiwa karibu kumaliza six, tumebakiza paper ya practical ya chemistry, siku hiyo ilikuwa jioni ki giza ndo kinaingia, nimetoka kupiga zangu nguna maharage, najisogeza taratibu naelekea kwenye kipindi cha dini, Mara ghafla naona watu wanakuja wengi wanakimbilia eneo la shule, Wa baba, wa mama wengine wana watoto, nikajiuliza kimoyomoyo haya maandamano ya nini tena, nikiwa bado nashangaa ghafla nikaona kitu hicho ndo kilifanya nione hii issue ni serious, nikamwona teacher wetu wa darasa nae anakuja mbio, tena mbaya zaidi ana kitambi sasa akikimbia balaa, na alikuwa na spidi maana ilikuwa kawaida yake kila asubuhi anatukimbiza ambao hatuendi assemble.

Duuh, nlipoona hivyo na mimi nikaliunga tukaanza kukimbia, kuna sehemu wanafunzi wanapenda kuangalia tv nikakuta nao wamesepa wameacha tv pale, Daaah sasa wote tunakimbia halafu hatujui tunakimbia nini, Sasa wakati naendelea kukimbia nikakutana na mlemavu mmoja yupo kwenye kiti chake cha matairi ( Maana ile shule ina wanafunzi walemavu pia),. Sasa hana mtu wa kumsukuma na kile kiti chake, kila mtu anaokoa nafsi yake, basi huruma ikaniiingia nikaanza kunsukuma huku tunakimbia, ebwanaeeh tumekimbia mwisho nikaona hapa nafeli, maana watu wanazidi kukimbia kuelekea bondeni huko alafu kelele zimekuwa nyingi, nikaona usintanie nikamwacha yule mlemavu nikaanza kukimbia mwenyewe.

Nikakimbia hatimae nikafika pondi, pale kidogo nikakuta watu wamerundikana kidogo,wanaulizana ni nini ila hakuna anaejua, ila juu angani anga limegeuka rangi, limekuwa jekunduuu kama vile jua lataka kushuka, alafu kelele kama vile watu wanapiga mabati huko angani au kama vile msitu unaungua sasa zile kelele za miti, daah hapo nikajua ndo mwisho wa dunia huu, wakati nageuka huku na kule mara namwona yule mlemavu ila saivi hayupo kwenye kiti bali anatambaa chini, nikajiuliza huyu kakimbia au kabebwa? Nikabaki nimestaajabu ila nikajichanganya asije kuniona akasema huyu broo ana roho mbaya, maana jinsi anga lilivyo jekundu yaani Hadi watu mna onana kabisa

Basi bana kelele zikazidi, watu woga ukaongezeka basi mbio zikaanza , tukapanda juu tukatokea Barbara kubwa ya pugu kajiungeni, Barabara imejaa watu wanakimbia, magari ndo usiseme, basi tukawa tunakimbia kelele zikizidi ukitazama juu unaona kama kimondo cha moto kinakuja hivyo unalala chini, kikipita unaamka tena unaaza mbio, Basi tukafika njia panda ya kisarawe na chanika, tukala kulia kuelekea kisarawe, mbio mbio unafika mahali unakutana na mdada anakimbia kanga inaanguka anabaki na chupi lakini hana muda wa kuokota kanga,ni kukimbia tu, mi pia sikuwa hata na hamu ya kutazama hayo mambo, maana unakimbia ukilala chini unasali ili likimondo lipite, basi ni kukimbia na kusali tu

Basi mara tukafika shule ya secondary Minaki , kulikuwa na wanafunzi pale nao wakaungana na sisi kukimbia, tukakimbia mara tukatoboa kisarawe,hapo ni usiku hata siijui saa ngapi, Basi pale kisarawe tukakuta watu wengi kinyama, yaanii pale ndo ikawa kama makutanio, watu wanaulizana ni nini,lakani hakuna anaejua dhahiri ni kitu gani kimetokea, Basi wakati tunashangaa pale mara ule mwanga na yale makelele yakawa takekaribia tena, watu wakaanza kuondoka kuendelea mbele,

Daah kwa jinsi nlivyokimbia na miguu ilivyokuwa inauma nikasema mi skimbii tena, kama kufa nife tu, basi nikaona cruzer moja imejaza watu nyuma inaondoka, nikaikimbilia nikaidaka, nikadandia yenyewe ikachanganya, sasa wakati natafuta sehemu ya kuweka mguu nikakosa, mikono ikachoka kubembea nikarudisha miguu kwenye lami, acha niburuzwe, nikaskia watu wanasema umeuaaaa, gari ikasepa nikaamka kujiangalia, nilikuwa nimevaa jinsi lakini ililiwa na lami paka ikakutwa Ngozi, nilichubuka vibaya, damu zinatoka balaa vidole vinatoa damu, ndala Sina maana zulikatika toka huko nikiwa nakimbia

Basi, mara nikaona cruiser moja imechorwa msalaba mwekundu, watu wanaikimbilia, na mimi nikazama, sasa wakati nazama kuna mama mmoja alikuwa mbele yangu, nikamvuta nyuma mi nikazama ndani, kumbe ni mke wa yule dereva anae endesha lile gari


Itaendelea
Mm mkuu nimefika sikonge mwak 2015 hap mjini tu na kufanikiwa kula mbususa ya mwanmke wa nmb pale afsa mikopo Soo napafahafumu skonge sanaaa
 
Chai hii mna pata faida gani kuandika uongoo..





[emoji81][emoji81][emoji81] tuna test mitambo kesho na uyu lazima akimbie kama yule wa story ya lindi
 
Siyo lazm iwe kweli kwani riwaya ulisosoma shulen Ni za kweli au utunzi tu acha wivuu toa Uzi wako na wew

Siangesema tu mapema tu kuwa yupo kazini anaandika riwaya kuliko kujifanya ni uhalisia kumbe [emoji477]️ chai tu,anaboa sana huyo kiumbe
 
SEHEMU YA NANE

Ilipoishia,,,,,,,,,,,,,,

Asubuhi wanakuja rafiki zake pale, ni wale nlikuwa nawaona pale wanajiuza, akawa anawatambulisha kuwa mi ni shemeji yao, basi sawa, nikakaa paka mchana tukala ugali fresh, Nikaondoka zangu kurudi chuo

Endelea,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Nikafika chuo nikalala sana siku hiyo maana hatukuwa na pindi, Nilipo kuja kushtuka nikaanza kutafakari yote yaliyotokea jana, Nikajilaumu sana maana hii yote ni sababu ya kuanza mapenzi ukubwani,

Basi ikawa ndo tabia yangu, usiku ukifika natinga kofia yangu najiachia buguruni, Nafanya yangu huko narudi room night kali nalala, Siku moja nikiwa na Jane kwenye vile vyumba vya short time mara mlango ukagongwa kwa nguvu, " Tokeni huko nyie washenzi" , Jane akaniambia hao ni polisi, Nikasema mbona hiki kisanga tena, sasa itakuwaje, itakuwaje sasa? Akasema kwa nyie hawana shida, kwa sisi ndo shida,

Basi mlango ukaendelea kugongwa, Jane akaenda kufungua, jamaa wakaingia wakatukamata na matusi kibao, tukatoka nje, kuna wengine nao wamekamatwa, Basi sisi wanaume tulikuwa kama sita, tukafungwa mashati wawili wawili, tukaswagwa na wale mademu paka kwenye gari ya polisi,

Tukazama ndani, tume kaa chini gari ikaamsha, Nikamuuliza Jane hapa tunaenda wapi? Akasema kituoni,
Basi tukazungushwa pale buguruni, mwisho tukapelekwa kituoni buguruni rozana , tukaambiwa vua mikanda,vua viatu, toa kila kitu weka mezani, tukafanya hivyo,

Haya kaa chini, tukaandikishwa majina pale, tuka kaa tunaskilizia, wale maaskari tuliokuja nao na gari wakawa wameondoka na gari, wakabaki wale tuliokuwa tumewakuta pale kituoni,

Baada kama lisaa tukiwa tumekaa pale nawaza sijui itakuwaje taarifa zilifika chuo, nikiwa bado nawaza, ndipo askari mmoja akasema oyaa, nyie semeni mna nini muondoke hapa, mkikaa hapa paka kesho tunawapeleka mahakamani, nikasema ukisikia kirangasi ndo hichi sasa,

Basi jamaa mmoja akasema mi nna elf 10 afande, Nikasikia we mwana haramu nini!! Yaan hao malaya uwape elf 10 na sisi utupe elf 10! Hanisi wewe, eeenh na nyie wengine, Mi nikasema nna elf 10 pia, Yule afande akasema nyie mna leta utani, ebu sogeeni hapa,

Basi tukaenda pale mezani, Akasema toeni hizo hela, Basi mi nikaomba walet yangu ilikuwa pale mezani, nikatoa buku ten, nikachukua vitu vyangu nikasepa, na wale wengine nao wakatoka tukawaacha wale mademu kule maana walikuwa chumba kingine, Basi nikatoka pale nikadandia gari nirudi zangu chuo, moyoni najiapiza sirudii tena yaan leo ndo mwisho, nikarudi room nikalala,

Ikapita kama wiki hivi sjatia maguu tena buguruni, Ila badae uzalendo ukanishinda, nikaona usintanie nikajiachia huyooo kama kawa, Nikakutana na Jane nikamuuliza siku ile ilikuwaje, akasema walilala paka asubuhi pale kituoni, kesho yake wakadeki mule ndani na kufagia nje alafu wakaachiwa,

Basi ikawa ndo tabia yangu, siku nyingine simtafuti Jane nabadilisha ladha, Nikaotea chimbo lingine mwanzoni huku kabla hujafika sheli kunasehemu wanauza mbao, basi pale ni chap kwa haraka, nyuma ya zile mbao tu mmna malizana unampa buku tatu yake unasepa,

Basi siku moja nipo room Happy akanipigia akaanza kuongea analia, analalamika siku hizi nimemtupa hata simpigii, Nikajitetea pale kwamba shule imekaba ndo maana, Alafu akaniambia kwamba ana miezi kadhaa haoni siku zake, Ukisha ambiwa hivyo unajua tu ni nini kinafata,

Basi akasema anahisi ana mimba maana dalili zote zimeshajionesha hadi home wameshamtilia mashaka, Basi nikampooza pale kuwa ntamtumia hela aende hospital akapime, Basi tukaongea mengi, nikaahidi bado nna mpenda na hata kama ana mimba mimi kwangu ni furaha kuitwa baba,

Basi siku zikaenda, test zikaja, UE hii hapa, tukapiga pale shule ikaisha watu wakasepa zao kwenye mafield huko, Mimi field yangu nikafanyia hapa hapa Dar, Happy nikamtumia hela akaenda kupimwa akakutwa na mimba ya miez mi nne, Kidume ukiskia mziki ndo huo, Basi home kwao walipogundua dingi yake akamfukuza aende kwa mwanaume alie mpa mimba, Basi akaenda kuishi kwa Anti yake kijiji cha jirani,

Itaendelea
 
Back
Top Bottom