Usilogwe ukaondoka nyumbani na kwenda usipopajua kwa kigezo cha kutafuta maisha

Usilogwe ukaondoka nyumbani na kwenda usipopajua kwa kigezo cha kutafuta maisha

SEHEMU YA KUMI NA TANO

ilipoishia,,,,,,,,,,,,,

Kweli kesho ikafika, Daah ni siku ambayo sitakaa niisahau maishani mwangu, yani yaliyonipata siku ile ni Mungu tu aliingilia kati, daah!! We acha tu, Basi bana siku ilianza fresh tu yaani,kulipambazuka vizuri nikajiandaa pale niende zangu moshi,

Endelea,,,,,,,,,,,,

Nikachomoka kiwandani nikapanda daladala pale nje huyoo paka town, Nikashuka pale nikadandia kosta ya moshi nauli buku mbili fresh,

Nikafanikiwa kufika moshi town pale, basi nikaona hieace za majengo, nikamuuliza konda zinafika majengo secondary akasema eeeh!! panda twende, Nikapanda pale ngoma ikajiachia hiyoo,

Basi tukafika sehemu konda akasema we wa sekondary sogea mbele, basi nikajivuta mbele, mara gari ikasimama nikashuka, Kumbe shule ipo njiani kabisa haina hata haja ya kuulizia, Maana nliposhuka tu nikaona wanafunzi, nikaona na kibao Majengo Secondary school nikasema yes mambo si ndo hayo, maana mi nlijua kuna mambo ya kuchukua bodaboda,

Basi nikasogea pale getini nikakuta mlinzi pale, nikamwelezea shida yangu, basi mlinzi akaniambia, bwana hata nikikuruhusu kuingia hutofanikiwa sababu mwalimu mkuu wiki ya pili sasa hayupo, Kaenda dodoma kwenye vikao vyao, na yeye ndo muhusika mkuu, Nikushauri tu uende alafu urudi siku nyingine, Basi nikasema sawa,

Basi nikaondoka zangu sijui hata nielekee wapi, Wakati nawaza au nirudi zangu nikapande gari nirudi Arusha basi nikaona upande wa pili zile fremu za maduka zilivyojipanga lazima zitakuwa zimezunguka uwanja wa mpira,

Basi wazo likanijia niingie huko ndani uwanjani, Basi kuna kageti hivi nikaingia kweli bana ni uwanja mkubwa sana wa mpira, Basi nikawa natembea tembea huko uwanjani na begi langu mgongoni,

Sa wakati natembea nikahisi kama kuna watu nyuma yangu, ile kugeuka hivi kweli bana kuna majamaa mawili yananifata, Nikipinda kushoto nao wana pinda, nikienda kulia nao wanaenda nikasema hawa ni vibaka, sasa hapa cha msingi ni kufunga mota tu, Basi kwa mbele kule kulikuwa kuna dada mmoja na yeye anapita pale uwanjani, Nikasema nikimbilie alipo yule dada,

Basi nikatoka nduki hiyo, jamaa wakaanza kunikimbiza, sasa wakawa wanapiga makelele kamata mwizi huyo!!, kamata mwizi huyoo!! , Basi yule dada alipogeuka akaniona nakimbilia ule upande wake akajua mi ndo mwizi, acha aachie yowe hilo, mwiziiii!!! Mwizi!!! huku anakimbia, heeeh! , Mara naona watu hao wanatoka pande tofauti tofauti wananikimbiza, basi nikasema nisimame, wale vibaka wakanikamata wakaanza kunipiga, wakachukua lile begi langu,
wananipiga wanasema mi mwizi,

Basi watu wakajaa nikaanza kupigwa, Najitetea jamani mimi si mwizi, wezi ni wale wamechukua begi langu, hakuna mtu ananisikiliza, Nikapigwa mtama huo,Nikaanguka chini, nikapigwa, Nikakatwa katwa, najaribu kujitetea hakuna mtu ananisikiliza, mwenye jiwe, mwenyet fimbo, mwenye rungu, mapanga ndo usiseme, nilipoona nimezidiwa nikainama chini wapige tu sehemu zote lakini si usoni,

Basi nikapigwa sana, yaani namaanisha sana yani, Mwili wote umetapakaa damu, basi mi nimejiinamia nalia tu, Nalia paka makamasi yanatoka yanachnganyikana na damu, Nasema jamani mnaniua mimi nimewakosea nini, msiniue jamani mimi si mwizi,

Basi nilipigwa na kitu hicho mgongoni nahisi ni tofali lile, nikasikia kama uti wa mgongo umevunjika yaani, nikajinyoosha nikalala na tumbo, hapo sa ndo naona nakufa sasa, maana nalia hata sauti haitooki, Watu hawajui mzee, waoo wanapiga tu, basi sasa nikawa siskii tena hata maumivu, wanapiga mi hata siskii,

Mara macho yakaingia nuru flani hivi kama miale ya jua la jioni, Basi nikawa naona kama naelea angani vile, Mara nikamwona Sity anakuja kunikumbatia anatabasamu na vidimpo vyake vile, Mara namwona Da J kama ananipa mikono hivi anipokee, Mara anatokea mama kama ananiita vile, namwona baba na yeye, Mara nikaona watu kama malaika hivi wanakuja kunichukua, mara wakapotea, nahisi fahamu zikawa zimenirudi nikawa naskia kelele za watu, kumbe bado wanajipigia tu mi sijui,

Basi nikaona kama nimekalishwa hivi, nikahisi kitu kama tairi nimevalishwa huku nikekaa, Mara namwagiwa kama maji hivi kumbe ni mafuta taa, nikajaribu kufungua macho kwa mbali nikaona watu wamenizunguka, mmoja ana kibiriti anahangaika kukiwasha, Basi nataka nimwambie nisamehe usifanye hivyo ila mdomo haufunguki, nataka ninyooshe mkono nimzuie ila siwezi, Mara nikapigwa na kitu sjui ni nini, kuanzia hapo ndo sikujua nini kiliendea tena, nikawa nimefloot,

Itaendelea
Daaaah kote tumecheka na kusikitika lkn hapa #15 its too sad. Hili jaribu lilikuwa zito sana. Pole sana mkuu kwa uliyopitia hizi elimu zetu hizi daaah.
 
SEHEMU YA KUMI NA TATU

Ilipoishia,,,,,,,,,,,,,

Basi chuma ikaamsha taratibu, Sity akawa analikimbiza gari paka likatoka nje ya kituo, Basi gari ikakamata morogoro road, Sity tukamuacha kasimama tu pale kaduwaa gari inaondoka, Basi chuma ikaamsha Arusha moja hiyo

Endelea,,,,,,,,,,,,,,,,

Chuma ikawa inatambaa balaa, safari imeshika kasi, watu naona wana mzuka kinoma na safari, naona kama wana enjoy, tofauti kabisa na mimi, sina raha, mawazo kibao, pembeni nimekaa na mtoto mzuri wa kichaga lakini sina hata time nae ( Nilijua ni mchaga baada ya kusikia akiongea na simu kichaga),

Nipo zangu kimya sina story na mtu mara simu ikaita, kucheki nikakuta ni Sity anapiga, nikapokea, Akauliza tumefika wapi, Nikamwambia tupo mbali sana, maana hata maeneo mi siyajui huko njiani, Basi akasema yeye kalala anahisi kama anaumwa vile, nikamwambia aende basi akachek maleria, akasema wala si maleria , ni mawazo tu anawaza ataishi vipi bila mimi, Ana feel upweke hadi anaumwa, Nikamwambia tuombe Mungu tu mambo yakikaa fresh tutaonana soon, basi tukaingia porini porini huko hakuna network simu ikakata,

Basi safari ikaendelea, mara nikapitiwa na usingizi nikalala sana, Kuja kushtuka nakuta gari imesimama watu wanashuka, nikamuuliza yule dada wa kichaga, dada hapa wapi, Akasema Mombo watu wanashuka kwenda kula, kucheki saa ni saa saba, kwenye simu kuna miscall za Sity kama zote, Nikampigia, Akasema mmefika wapi, nikamwambia ndo tupo mombo sehemu ya kula panaitwa Liverpool, Akauliza, we umekula, nikamwambia mi hata hamu ya kula sina, akanibembeleza na kunisihi sana, kwamba nikienda kula hata yeye atapata faraja,

Basi nikaona isiwe shida, nisije nikamuudhi mtoto mzuri bure, nikashuka nikaenda toilet, nikatoka nikaenda kununua sambusa mbili za nyama na soda nikarudi kwenye gari nikatulia,

Basi watu wakarudi gari ikaamsha, tukafika moshi mjini kama saa kumi hivi, Basi likaingia stendi, wenye kushukia moshi wakashuka, Wakapanda wengine wanaoenda Arusha, Basi likakaa pale kama nusu saa hivi hatimae likaondoka, safari ya kuelekea Arusha ikaanza,

Tukafika Arusha kama saa moja hivi usiku, Nikashuka pale kama mtu anaejua anapoenda vile, ili machalii ya r yasije niona wakuja yakanidandia maana stori zao nnazo,

Basi nikazunguka zunguka pale stand mwisho nikaamua nikae kwenye vile vibanda vya abiria, Pembeni kuna mama mmoja kaweka vitu vyake pale anauza chakula, Nikamsalimia yule mama, nikamuuliza eti kiwanda cha nguo kipo maeneo gani, akasema kipo kisongo kinaitwa a to z, nikamuuliza ni mbali kutoka hapa, akasema ndio, ni nje ya mji, unapanda kihiace ( daladala) nauli mia tano, Nikamuuliza hivyo vihiace vipo hapa, akasema inabidi uende standi ndogo inaitwa kilombero, huko ndo kuna vihiace vinavyoenda nje ya mji, basi akanielekeza ilipo hiyo stand, ila nikaona hata nikienda saivi ni usiku ntapata shida tu huko, ni bora nitulie tu pale stand paka kesho asubuhi ndo nianze hizo mishe,

Basi nikatoa simu nikampigia Sity nimjulishe nimefika salama, tukapiga stori pale kidogo basi tukamaliza,

Pale stand abiria wanaolala pale ni wengi tu, wanaotoka maeneo ya mbali ambao wanasubiri magari ya alfajiri sana, basi nikawa sina wasiwasi,

Muda ulivyoenda nikaweka begi langu kama mto, nikatia mbonji pale kwenye benchi, ila nikawa nalala kwa machale, kila saa nashtuka shtuka wasije machalii ya r wakapita na mimi,

Basi asubuhi ikafika, nikaenda kwenye kamgahawa flani hivi nikaomba maji nikanawa uso, nikapiga chai pale fresh, Nikatoka nikashika njia kuelekea stand ya kilombero huku naulizia maana ni mbali kidogo,

Kufika pale daladala kama zote, basi nikaskia kisongo kiwandani!!, Kisongo kiwandani!!, Basi nikajua ndo hii na hicho kiwanda itakiwa ndo hicho cha nguo, basi nikazama ndani, badae kikajaa hicho kikaamsha,

Basi tukatembea weeee tukatoka nje ya mji kabisa, tukafika sehemu tukakata kushoto tukatembea kiasi hivi mara nikaskia wale wa kiwandani!!, wale wa kiwandani!!, basi tukashuka, abiria wengine wakabaki gari hiyo ikageuza tulipotoka,

Basi pale ndo kiwandani, kuna geti kubwa na walinzi hapo nje, sema geti ni la nondo kwaiyo ndani unapaona, ila ndani tena kuna geti jingine huko ndo huwezi kuona maana geti si la nondo,

Basi pale nje kuna maduka na vibanda vingi tu, Nikajivuta kwenye kibanda kimoja nikanunua soda nikakaa nakunywa huku nasoma mazingira, nikajaribu kumuulizia jamaa pale kuhusu chance za kazi pale kiwandani, akasema pale kila ijumaa wnakujaga hapo getini wanachukua watu, nikapiga hesabu siku hiyo ilikuwa jumatano,kwaiyo inabidi nisubiri paka ijumaa ndo nije,

Basi nikajaribu kumuulizia kuhusu wale jamaa zangu kama anawafahamu lakini wapi, basi nikakaa sana pale paka jioni wafanyakazi wakaanza kutoka, aisee!! ni wengi kichizi, basi nikawa nawaulizia kama wanawajua wale jamaa zangu ila hakuna hata mmoja anaewajua, Nikasema sasa hapa kazi ipo.,

Basi kigiza kikaanza kuingia, hapa sasa nitafute pa kulala, mfukoni nna kama elf 60 hivi na machenji, nikaulizia gest maeneo yale nikaambiwa gest paka kisongo,

Basi nikachkua boda pale buku paka kisongo, nikaulizia gest pale nikaelekezwa gest moja maeneo yale, nikafika nikaulizia chumba nikaambiwa single elf 5 nikasema fresh, basi nikapewa chumba nikaeka begi langu nikaenda kuoga, nikatoka nikaenda kucheki msosi huko road,nikala nikarudi zangu room, nikajilaza kitandani nikampigia Sity tukaanza kupiga story,

Itaendelea
Vp kuhusu mwanao yule wa kijijini mbona humgusii tena kwenye stori zako
 
Sipingi stori ya mtu mkuu wala sina tabia hiyo ....katika hali ya kawaida huwezi tuambia athari za kuondoka sehemu uliyozaliwa then ukanza kutueleza maisha ya shule ...hatakama hko mbeleni alibadili lakini ameanza vibaya .....why stori itengeneze mashaka ndani ya sehem ya kwanza tu?
Ukisoma story yote ndio utagundua uhalisia wa hiyo Title.

Msimuliaji Yupo sahihi. Hekaheka za kunusurika kufa kazipata akiwa Arusha.
 
Kama ulikwisha safiri nje ya Tanzania unajua passport ni nini. Wakati mi naonyesha ujuaji, wee unaonyesha umbumbumbu. Kwamba kwenu picha zinaitwa passport. Katika akili yako unajua kabisa kuwa picha zinajulikana kama passport!!??
Acha ujuaji, wakati unaelewa kabisa anamaanisha passport size
 
Akili nyingi mtu wangu, umeandika ki uanaume sana.
Unataka aanze kulingana ubongo ama mind itakavyo comply or contemplate. Mbona watu hamuheshimu tofauti tulizo nazo binadamu mkuu. Mie mfano mpira sipendi yaani naonaga watu wanajazana nawatani kuwa suala la kuona mwanaume mwenzangu akimeki mane namie napoteza muda hiyo jobu Sina.
Ila Sasa akija hapa like Shakira hata Kama kiingilio 10M ninayo nitaenda kumcheki MTT wa kilatino. Ama wanamieleka akina Huko Hougan na Cena wakija hapa bongo kwa show nahudhuria Kama iyo gharama naimudu.
Hujui kuwa Ana Mana gani kuanza kuelezea ivyo. Yaani Kuna logic behind so Kama huwezi Iona subiria huko mbele mkuu.
Kila mtu huwa Ana namna ya kuwasilisha kitu. Yaani umeshawahi kuwa na marafiki wa madhehebu yote ama dini ambazo sio asili ya afrika ukawauliza ni kwa Nini unasali ama kuswali ama kuabudu hapo ulipo kila mtu Ana reasons zake na ziko sawa kulingana na yeye.
Listen two men, one says impossible and onother says possible both are equal/alright.
Halafu Sasa mfano kupinga baadhi ya vitu vya maana huo ubavu hatuna. Mfano umeshawahi kuona detects zilizopo katika Newton's laws kweli. Ama Tesla alivyogundua umeme umeshawahi fanya research ukatoa andiko kuwa ni kwa Nini alianza vibaya wewe ukaweka vizuri.
Ama hizi chanjo u critize mkuu negative sides zake uje na njia mzuri ya chanjo.
Ama namna ya barabara zinavyojengwa uje na materials mbadala ya kutumia tusitumie lami Mana ghali sana.uje na option ya material simple Sana cheap ili uokoe our global Kama watu walivyokuja na magari ya umeme ili kuiokoa our global na global warming Mana tunaharibu ozone.

Sasa Kama huwezi Bora ukakaa kimya ili tupeane koneksheni na kupeana ujanja wa kula mbususu mpaka itetemeke Mana blacks hatuna zaidi ya akili ya kuichakata mbususu ili ituheshimu.

Yaani mie unakuta mtu anakuwa makini kinouma nukta kwa nukta badala hata uje na mbadala wa songaz, bandari ya bagamoyo kwa mustakabali wa Taifa letu. Ama elimu gani kizazi Cheri kipate ili kisitegemee ajira Bali waweze kujiajiri.
 
Mtoa story kama ni story ya ukweli basi mtoa mada ni msimulizi mzuri na mwandishi hodari, kama niyakutunga mmsimulizi ni mwerevu sna , kama kakopy mahali basi mtoa mada anajua watu wanataka nini na anafaa kuwa kiongozi hodari.[emoji122]
 
SEHEMU YA KUMI NA SITA

Ilipoishia,,,,,,,,,,

Mara nikapigwa na kitu sjui ni nini, kuanzia hapo ndo sikujua nini kiliendea tena, nikawa nimefloot,

Endelea,,,,,,,,,,,,,,,

Nilikuja kupata fahamu nikajikuta nipo wodini, Nimelala kitandani nimetundikiwa drip, nimepigwa bandeji karibu kila mahali, Sa najiuliza nimefikaje fikaje pale ,Kumbu kumbu haziji kabisa, Naona tu manesi wanapita pita, watu wana pitapita,

Basi nesi mmoja akaja kwenye kitanda changu, akaangalia angalia ile drip, anataka kuondoka nikamuuliza, Nesi hapa ni wapi? Akasema pale ni Majengo hospital, Nimefikaje hapa? Akasema uliletwa hapa na polisi ukiwa na hali mbaya sana, basi akaondoka,

Sasa pale ndo kumbukumbu zikaanza kunijia, nikaanza kukumbuka matukio, Nikakumbuka wale vibaka, nikakumbuka nilivyokuwa napigwa, Daah machozi yakawa yananitoka, Nikakumbuka begi langu walichukua wale vibaka, mbaya zaidi lilikuwa na vyeti vyangu vyote kuanzia vya shule paka cheti cha kuzaliwa,

Ahhhah niliumia sana, nikasema sasa yote haya ni nini, kwanini yanitokee mimi, Basi nikamkumbuka Sity nikasema lait angekwepo angenisaidia, Nikakumbuka maneno ya Da J siku ile namwambia kwamba nataka kuondoka niende Arusha, alisema "Usiende huko Utakufa" Nikahisi Da J alifunuliwa yatakayokwenda kunikuta huko,

Basi nikakaa pale hospitali, kumbe polisi bado wananilinda, Wanakuja pale kitandani wananiangalia wanaondoka, Basi nikawa nasikia watu pale wodini wananong'onezana huku wananinyooshea kidole, Wanasema yule pale ni mwizi, Aliletwa hapa hafai ila saivi kapata nafuu, Moyoni nikawa naumia sana maana mi najua mi si mwizi, sema ndo hivyo nani ataniamini,

Basi badae nilikuja kufahamu kilichotokea siku ile, Kumbe wakati wanataka kunipiga kibiriti pale chini kumbe polisi wakatokea, Watu walivyoona polisi wakakimbia wakaniacha ndo ikawa ponea yangu, Kumbe kituo cha polisi cha majengo hakipo mbali na pale uwanjani kwaiyo polisi walipopata taarifa wakaja fasta, Basi nikatiwa kwenye gari yao wakanileta pale hospitali, kumbe hospitali yenyewe ilipo na pale uwanjani imetenganishwa na barabara tu,

Basi nilikaa sana pale hospitali, paka majeraha yakaanza kupona, polisi wapo tu na mimi hawaniachi, basi siku ya siku nikapewa ruhusa, basi polisi wakanichukua paka pale kituoni, Nikaandika maelezo pale badae wakanitia ndani kwenye kiselo chao pale kituoni , mzee baba maisha ya huko selo sitaki hata kuyasimulia,

Basi siku ya pili nikapandishwa mahakamani pale moshi mjini mahakama ya mwanzo, nikasomewa shitaka langu la kutaka kuiba kwa kutumia nguvu, Akaja askari mmoja wa kituo cha majengo kutoa ushahidi, akaelezea jinsi walivyopata taarifa, na jinsi walipofika pale wakanikuta napigwa, pia akasema dada ambaye nilitaka kumuibia pia walimpata na yeye akatoa maelezo yake,

Badae akaitwa dada aliyetaka kuibiwa na yeye atoe ushahidi, basi akapanda yule dada, akasema yeye alikuwa anakatiza pale uwanjani huku anaongea na simu, mara ghafla mimi nikatokea nikaanza kumkimbiza nataka kumnyang'anya simu, alipoona vile ndo ikabidi ajitetee kwa kukimbia na kupiga ukunga,

Basi na mimi nikaambiwa nijitetee na kama nina mashahidi pia nilete, Mi nikasema sina mashahidi nitajitetea mwenyewe, Basi nikaileza mahakama kila kitu, kuanzia nilipoenda pale shule, nilivyokimbizwa na wale vibaka, nilivyopigwa mpaka nilipojikuta hospitali,

Basi hakimu akasema kesi imeahirishwa mpaka kesho kwa ajili ya hukumu, kwa sasa nitaenda mahabusu ila milango ya dhamana ipo wazi, Nani sasa wa kuniwekea dhamana, ikabidi nipelekwe mahabusu gereza la Karanga lilopo pale moshi,

Mzee kwa mara ya kwanza natimba gerezani, wacha kabisa!! Siku hiyo sikulala kabisa, niliwaza mambo mengi sana, Nikakumbuka maneno ya Sity " Ebu jichunguze ni wapi ulipo mkosea Mungu", Nikakumbuka sana kijijini kwetu, Nikasema bora na mimi ningesepaga home kama Kidosho, Nikamkumbuka Happy na Mwanamgu Joyce, toka nimwone kwenye picha sijawahi kumwona tena, nikawaza saivi atakuwa mkubwa, sijui kama nitawaona tena,

Itaendelea
Kwa Sasa nimeanza kuelewa mahusiano ya kichwa Cha Uzi na masimulizi yako. Nategemea utakuja kuishia baada ya kuamua kurudi nyumbani na kuaga vizuri maisha yalikuwa mazuri na Sasa yanaendelea vizuri. Pole sana na hongela kwa simulizi la maisha yako
 
Okay. Nilikwishaenda serikali za mtaa nikaombwa kitambulisho. Wakasema hata passport ni sawa. Nikatoa passport. Ikakubaliwa. Kwa hiyo mi nilijua wewe uliombwa passport na ukaomba Uhamiaji na ukaipata siku hiyo hiyo!

Anyway, niko na wewe mpaka mwisho. Najua siku hizi uko kwenye Baraza la Mawaziri. Nasubiri story ya siku uliyosikia uteuzi huo.
Hii nchi hii, ndiyo maana mtu kama Jiwe aliweza kuwa Rais
 
maisha unayosimulia ni uhalisi kabisa watoto wa mama tu ndio watasema chai...mimi binafsi niliishi maisha hayo baada ya kumaliza chuo naliona elimu yangu ni bure kabisa nakumbuka vizuri nilikuwa hata natamani niwe konda niliona konda anamaisha kuliko mimi na nilikuwa mbali na nyumbani kama wewe mkuu acha kabisa nilikuwa nanunua mkate ule mkubwa nakula huo huo hata siku nne nisife tu, nimelala bila kula hata kwa siku mbili mara nyingi sana, nikipata unga ni ugali tu then maji nalala nilikonda nikabaki kichwa tu nilikuwa naongea mwenyewe kama chizi na kucheka kabisa..wanaume tunateseka sana...kipindi hicho unakaa hata miezi minne hakuna simu unapokea mtu akutafuten ili nini msg, nikiona sms ni za mtandao au bili ya maji au baba mwenye nyumba anakumbusha kodi inakaribia kuisha najua ni hao tu watanichek na sikuwa na mwanamke yoyote nilipambana ile kihard core..
lakini namshukuru Yehova hayo maisha yamekuwa historia taratibu lakini hayo maisha yamenifundisha kuja kuishi bila huruma kabisa yaani mtu akija analialia msaada namwaangalia tu wala sijali
Uko sahihi mkuu,watoto wali nazi ndio wataona hii ni chai,ila kuna visa tukija kuvitoa humu raia wataona ni chai ilozidi tangawizi tena bila kashata,au ni movie la Kihindi kumbe ndio uhalisia wa maisha yetu.
 
Kama ulikwisha safiri nje ya Tanzania unajua passport ni nini. Wakati mi naonyesha ujuaji, wee unaonyesha umbumbumbu. Kwamba kwenu picha zinaitwa passport. Katika akili yako unajua kabisa kuwa picha zinajulikana kama passport!!??
Huna akili, nyie ndiyo darasani mlikuwa mnakariri tu. Umesema passport huwezi pata ndani ya siku moja ila akili yako imekwambia alipeleka passport ya kusafiria then unabisha, sasa hapo unadhani uko sawa kichwani? Ni sawa na wale wanaosema jamaa aka left group, wewe na akili zako utaanza kubisha kwa kuwa ulitaka waseme jamaa aka leave group. Akili matope hizi
 
Back
Top Bottom