Usilolijua ni kwamba Aron Kagurumujuli amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kutoka Wilaya ya Kinondoni

Usilolijua ni kwamba Aron Kagurumujuli amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kutoka Wilaya ya Kinondoni

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Kwa wageni wa JF ama labda na Wenyeji lakini Wasahaulifu , Aron Kagurumujuli alikuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni , aliyeshiriki kikamilifu kutokomeza Demokrasia na kuhusika kwa Udi na Uvumba kwenye Mauaji ya Akwilina , Mwanafunzi wa chuo cha NIT , aliyepigwa risasi na Polisi na kupasuliwa kichwa ndani ya Daladala , kwenye Mauaji ambayo walengwa hasa walikuwa viongozi wa Chadema , Kagurumujuli alishirikiana Kikamilifu na RPC wa Kanda Maalum aliyeitwa Lazaro Mambosasa .

Hadithi hii ni ndefu sana , na nina hakika kwa dondoo hizo hapo juu angalau nimewakumbusha jambo .

Bali itoshe tu kusema kwamba Kagurumujuli , aliyekuwa Msimamizi wa Uchaguzi unaoandaliwa na Tume ya Uchaguzi , Amechaguliwa kwa kishindo kuwa MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM TAIFA kutokea Wilaya ya Kinondoni , kwa tafsiri ya haraka , inaonyesha kwamba wanaccm wa Kinondoni wamemlipa Kagurumujuli kwa kazi nzuri ya kukisaidia chama chao na kushiriki mauaji ya Akwilina .

#Katiba mpya ni sasa
 
Kwa wageni wa JF ama labda na Wenyeji lakini Wasahaulifu , Aron Kagurumujuli alikuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni aliyeshiriki kikamilifu kutokomeza Demokrasia na kuhusika kwa Udi na Uvumba kwenye Mauaji ya Akwilina , Mwanafunzi wa chuo cha NIT , aliyepigwa risasi na Polisi na kupasuliwa kichwa ndani ya Daladala , kwenye Mauaji ambayo walengwa hasa walikuwa viongozi wa Chadema , Kagurumujuli alishirikiana Kikamilifu na RPC wa Kanda Maalum aliyeitwa Lazaro Mambosasa .

Hadithi hii ni ndefu sana , na nina hakika kwa dondoo hizo hapo juu angalau nimewakumbusha jambo .

Bali itoshe tu kusema kwamba Kagurumujuli , aliyekuwa Msimamizi wa Uchaguzi unaoandaliwabna Tume ya Uchaguzi , Amechaguliwa kwa kishindo kuwa MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM TAIFA kutokea Wilaya ya Kinondoni , kwa tafsiri ya haraka inaonyesha kwamba wanaccm wa Kinondoni wamemlipa Kagurumujuli kwa kazi nzuri ya kukisaidia chama na kushiriki mauaji ya Akwilina .

#Katiba mpya ni sasa
Tutarajie kuona laana akimfuata kila aendako pamoja na chama chake
 
wabongo kwa kulalamika hatujambo mwacheni kama kachaguliwa afanye kazi hizo habar za kumuua mwanafunzi sote tunasikia stori tu hakuna aliekuepo kwenye tukio na hata kama alikuepo kwenye tukio chumvi lazma iongezeke japo kidogooo
 
Tatizo huko watu wanapewa majukumu maalumu,utawekwa kwenye mfumo kisha utaambiwa wewe kazi yako ni kutukana tu,ama kuropoka tu kuharibu hali ya anga,cha kuzungumza utapewa.Sasa ni tujue kabisa kuwa huko watu wapo tayari kupokea maagizo na kuishi kwa mtindo huo Hakuna aliyemzuri huko.
 
Huyu jamaa nikisikia jina lake nakasirika moyoni.Ni Jirani yangu kwa huku mkoani,lakini aisee kitendo kile alichowafanyia mawakala wa CDM kilichosababisha vurugu hakitasahaulika kamwe .Daima ataandikwa katika historia kama kiongozi katili asiyependa demokrasia ambaye alikuwa tayari kufanya chochote kulinda tumbo lake.
 
Back
Top Bottom