think tank01
JF-Expert Member
- Aug 11, 2022
- 270
- 400
Hapa nchini tangu zamani tumekuwa tukisikia, kushiriki au kuona (kushuhudia) MIRADI mbalimbali inayoanzishwa na kusimamiwa na Serikali kwa lengo la kuleta maendeleo kwenye Jamii husika. Mfano: Miradi ya Maji, Umeme, Barabara, Shule, Vyuo na Vituo vya Afya n.k
Miradi hii baadhi imekuwa ikitekelezwa (kujengwa) kwa viwango vya juu na bora hatimaye kuleta manufaa kwa Jamii kwa kukamilika na kufanya kazi au kutoa huduma iliyokusudiwa. Lakini vilevile imekuwepo miradi iliyojengwa chini ya viwango au kutokukamilika kabisa na hatimaye kukwamisha huduma iliyokusudiwa kutolewa na mradi husika kwenye Jamii.
Hoja yangu:
Kwa kutumia Wataalam wa Mifumo ya Tehama nchini, Serikali haioni kuna haja sasa ya kuanzisha Mfumo utakaokua na uwezo kuonyesha kila linalofanyika kwenye mradi husika kwa Jamii?
Ili nieleweke nitolee mfano:
Kwenye mradi wa ujenzi wa kibanda cha mlinzi chuo cha veta (haihusiani na kibanda cha mlinzi kule Tabora)
Nondo 109 mm12 bei 4,600,000/=
Tofali 200 bei 340,000/=
Bati 20 G26 bei 1,400,000/=
Saruji mifuko 130 bei 3,504,000/=
Mlango 1 msani bei 1,300,000/=
Dirisha Aluminum 2 m1.4 bei 700,000/=
Kitasa 1 bei 120,000/=
Lengo Jamii tuweze kuona na kusimamia matumizi sahihi ya fedha zetu ambazo ni Kodi tunazozichangia sisi.
Pia tuweze kukemea na kusemea pale tunapoona matumizi yasiyo sahihi (wizi wa fedha za miradi kwa watumishi wanaopewa dhamana za kusimamia ujenzi wa miradi hio)
KARIBUNI kwa maoni wadau.