RWANDES
JF-Expert Member
- Jun 12, 2019
- 1,788
- 4,401
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof Mbarawa amesema pamoja na Serikali kuwekeza tsh 1 trillion pale Bandarini bado performance imekuwa hairidhishi.
Tatizo la bandari yetu kuchangia bajeti 37% ni kwasababu ya usimamizi mbovu ambapo hupelekea baadhi ya vigogo wa serikali na watu mashuhuri kipitisha mizigo yao bila kulipa kodi yoyote si hayo tu pesa za ukarabati wa bandari na kutengeneza mifumo mizuri ya teknolojia imekuwa ikiharibiwa na watendaji wa bandari na kutonunuliwa kabisa,tumekuwa tunaona matukio mbalimbali kama hayo nchini yanasemwa na serikali yenyewe. kwa hiyo uzembe wa serikali katika usimamizi na kupeana vyeo kwa kujuana ndiyo unapelekea uchangiaji mbovu.
Prof. kutuambia kwamba DP WORLD itachangia kiasi cha 67% ya bajeti ya taifa ni hisia zake mwenyewe. pesa mmekopa kwa ajiri ya upanuzi wa bandari zaidi ya trion moja hizo pesa kumbukeni mtatesa watanzania kuzilipa.
Tanzania hii haitokuja kuendelea kwa mifumo hii ya kupeana vyeo kwa kujuana na kulindana kwani kufanya hivo ndiyo imepekekea utendaji mbovu katika sekta mbalimbali.
Mashirika mengi ya umma yatakufa kwa mtindo huu ccm inavyoendesha nchi kwa kujuana.
Nasema endeleeni kupeana vyeo mara huyu anastaafu mara yule mnapeana board.