Usimamizi mbovu wa mifumo ya huduma mtandao hutumika kuiba mabilioni katika kutoa huduma. Rais, agiza ukaguzi wa mifumo yako utanishukuru

Usimamizi mbovu wa mifumo ya huduma mtandao hutumika kuiba mabilioni katika kutoa huduma. Rais, agiza ukaguzi wa mifumo yako utanishukuru

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Nilianza kupata ubuyu huu kwenye mjadala wa vijana flani nikashtuka Sana, katika udadisi na kujielimisha kupitia maandiko mbalimbali ya huduma mtandao ( e- services) nikagundua ipo haja yakuikumbusha serikali umuhimu wa kufanya ukaguzi maalumu katika mifumo ya utoaji huduma zinazolipiwa kwa control namba au e- service.

Naomba niwaeleze namna watu wanavyoiba na hii itufumbue macho nakuwakamata watengenezaji wa mifumo hii pale itakapothibitika wapo watu kwenye makampuni haya yaliyopewa dhamana wanaofanya uhalifu huu.

Kabla sijatoa mianya iliyo wazi napenda kuwakumbusha kwamba mifumo hii ya e service imekufa kwenye halmashauri kwa visingizio mbalimbali na pale ambapo inatumika hasa serikali kuu imehujumiwa kuanzia utengenezaji wake na hata matumizi yake, hujuma hii inafanywa Kati ya watengenezaji wa mifumo hii na wasimamizi wa serikali huku ikifanywa kwa Siri na kuzuiwa kukaguliwa ubora wake. Naleta kwenu dondoo za maeneo yanayotajwa yanayovuja kwenye mifumo hii kwa majadiliano lakini pia kwa ajili ya serikali kupitia eGA kufukua nakunweleza Mhe. Rais ukweli wa uozo huu ambao ungesima iwa vyema hata tozo tusingelazimika kulipa: NANUKUU VIJANA WASEMAVYO KWENYE MIJADALA YAO TANZANIA NA DUNIANI, NTAANDIKA KWA INTERNAL CONTENT KUZONGATIA MAZINGIRA YA TANZANIA

1. Wapo watengenezaji wa mifumo wanaouza control number ambazo zimeshatumika. Mfano control number ya bili ya maji inajazwa kwenye control number ya bili ya ardhi hivyo ukiona risiti ya kielektronic unaamini kweli umepewa huduma sahihi kumbe usomeki kwenye huduma husika. Hapa watu utumia control number moja kutoa huduma hata mia moja na kwa kuwa huu ni wizi wa mfumo wanaopaswa kuzihakiki hizi control number awafanyi hivyo.

2. Watu kutengeneza bili bandia, hii inaelezwa vyema kwenye huduma za Visa ambapo online visa Duniani uathiri mapato pale ambapo wanaohakiki visa wakati wa kuingia watashindwa kufanya uhakiki. Eneo hili la huduma mtandao utumiwa Sana na vishoka wakimataifa kutengeneza pesa kwa kuwajazia watu maombi ya visa na kuwapa uthibitisho wa malipo ambao haupo au kuwapa number za malipo zilizokwisha tumika ila zikiwa na details zote Kama hati halali ya malipo

3. Baadhi ya mifumo ya fedha kudukuliwa na kuchepushwa kiasi flani Cha fedha. Unakuta wakandarasi wanachepusha baadhi ya malipo ya serikali kwa kutengeneza number za malipo za kwao na hivyo fedha kuingia kwenye akaunti za wakandarasi. Huku ndipo uchepushiwa fedha za serikali na wataalamu waliokabidhiwa mifumo ya serikali.

4. Kufuta taarifa za waomba huduma kwenye mifumo. Baadhi ya vijana wanaofanya kazi kwenye makampuni ya utengenezaji mifumo ya serikali hasa kwa hapa Tanzania na mataifa mengi wamekuwa na tabia yakufuta taarifa za baadhi ya waomba huduma hasa baada ya kutumia wateja hao kuiba. Mfano unakuta units zinafutwa au taarifa zote za wateja zinaondolewa kwenye sever kwa ushirikiano na menejimenti, kwa ushirikiano na wanunua taarifa au kwa kukwepa tracing. Hapa ndipo takwimu kwenye mifumo ushuka, na bila wakaguzi kufanya ulinganisho wa data ni vigumu kugundua. Upo ushahidi wa baadhi ya vijana kufuta data za huduma kwa makusudi

5. Negligence, ipo tabia ya mifumo ya private na serikali kutengenezwa huku ikiendelea kutoa huduma. Mwanya huu utumika kufanya uharamia kwenye mifumo ya serikali na ikibainika wakandarasi ujificha kwenye kivuli Cha matatizo ya kimfumo. Kipindi hiki ndipo wakandarasi ucheza michongo na kupenyeza mambo yao

6. Baadhi ya tafiti zinadai zipo taasisi zimeruhusu utengenezaji wa reserve number za huduma kwa ajili ya kutoa huduma mfumo ukiwa chini. Kwa njia nyingine utasikia menejimenti na wapigaji wengi wakilazimisha wawe na reserved number let say reserved control number. Taasisi yoyote yenye reserved control number imeifilisi serikali. Hapa hizi number utumika kutoa huduma kinyume kabisa na utaratibu uliowekwa na wakandarasi wanapotengeneza reserved control number lazima utengeneza za kwao. Ukaguzi ukijikita eneo hili mtanishukuru kwa uzi huu

7. Mifumo mingi ya serikali inatumika bila kukamilishwa ili watu watumie mapungufu kupiga fedha. Sometimes fedha upigwa kwa kipengele Cha maintainance au wakati mwingine mfumo ule ule kulipiwa mara mbili kwa kisingizio kwa mahitaji yamebadilika. Makampuni ya kigeni wanatumia Sana mbinu hi na Sasa makampuni ya wazawa mengi hasa Yale yaliyoaminiwa na serikali wakapewa tenda wamekuwa wakitengeneza mifumo mibovu ili kila wakati waitwe kurekebisha .Mwaka juzi nilikuwa na kampuni moja hapa nchini inayotengeneza mifumo ikiwemo ya serikali,ukiangalia udhaifu wa mifumo wanayotengeneza na ukiambiwa eGa wanakagua na kupitisha unajiuliza hii nchi ipo salama kimifumo? eGA aidha kwakukosa Wataalamu wameidhinisha mifumo mingi isiyo na sifa kwa kukosa userious na baadhi ya watendaji kukosa utashi wa kukosoa wakandarasi wa nje na hata wa ndani waliopewa kazi na serikali.

8. Makampuni yanayotengeneza mifumo ya serikali hayatoi ajira kwa watu wenye ueledi, mifumo nyeti inakabidhiwa wanafunzi wa vyuo Tena sometimes ikiwa na data zilizo live. Hapa ndipo Siri uvuja na kupelekea wadukuzi kutumia mianya ya mifumo hiyo kudukua na kupiga fedha kwa kuchepusha au kuuza credentials kwa makampuni makubwa. Nimefanya kazi kwenye makampuni mengi hapa bongo, wanafunzi wanapewa uwezo wa kuingia kwenye mifumo na wakati mwingine hata wakiacha kazi wanaendelea kuwa na uwezo wa kuingia kwenye mifumo.

9. Mifumo mingi haiana usalama na wanaoisiamamia siyo watu committed. Menejimenti nyingi za seriakali zimekaliwa na watu wasio na uwezo wa kubaini changamoto za ICT lakini Hawa ndio wanaopitisha fedha za mifumo. Tujikite kuweka watu sahihi maeneo sahihi, meneja anapewa mradi anachowaza yeye ni kiasi anachopata kwa umeneja lakini mifumo ina ubora gani hajui.

10. Ubovu wa server au kufungwa server zenye uwezo mdogo ambazo zinapojaa uepusha kufanyika kwa verification hasa kwenye huduma zenye central server na min server ya vituo. Lengo la kununua server ndogo nikuruhusu manual way ya kupush data wakati huo huduma imeshatolewa bila mfumo kujiridhisha na uhalali wa huduma hiyo. Server nyingi za vituo vya huduma za serikali hazina capacity ya kutosha na zilinunuliwa hivyo makusudi kwa maana kitaalam hapa ndipo uzalishwa upotevu wa data. Makampuni binafsi uwezi kupewa mradi ukanunua server ndogo kuliko uwezo wakakuaacha salama, serikalini sijui kama kuna mtu anagaika kukagua uwezo wa vifaa zinavyofungwa na niombe niwafumbue macho, sehemu zote zenye servers zisizokidhi wapo watu wamewekwa kusukuma data manually na bila Siri hiyo kugundulika na ikitokea ukaguzi data ufutwa kwenye server kuruhusu data mpya na hapa ndipo wakaguzi ukutana na clean data tu.

Kwa wale wanaosoma masuala ya mitandao na huduma zake wataniunga mkono kwamba serikali inapojikita kwenye huduma mtandao lazima iwekeze kubaini wizi la sivyo tutakuaja kushtuka tumebigwa mabilioni. Lakini pia serikali iache kabisa kuamini makampuni binafsi kwenye utengenezaji wa mifumo kwa sababu waaajiriwa wengi wanalipwa mishahara midogo lakini pia ni vijana ambao hawana vifua kuficha Siri hivyo kurubuniwa na kuuza data au kutongozwa Ni kazi rahisi Sana kwao.

eGA kupitia tips hizi fanyeni utafiti mtagundua wizi unaofanywa kwenye huduma Ni mkubwa Sana. Kwa Sasa hivi upo uwezekano fedha ikaonekana imekwend benki lakini isifike na kutrace imepotelea wapi ni vigumu.
 
Serikali kwa kweli sina cha kuisaidia hata kipindi kile LUKU inasumbua kiukweli watu walikuwa wanafanya yao, sasa kwa kuwa serikali ni kipofu na jeuri ipo busy kukiua chama cha chadema acha watu waibe tuu.

KITU KINGINE, KUNA HAJA YA SERIKALI KUFANYA UCHUNGUZI KWA NINI WATU WANAIBA ?? KIUKWELI SERIKALI INATAKIWA IBORESHE MASLAHI YA WATU WAKE NA KUWEKA USAWA WA KIMASLAHI NA KUWEKEZA KWA RASILIMALI WATU WENYE WELEDI.

huwezi kumlipa mtu laki tano mwezi mzima bila posho wala overtime halafu akuletee tija kazini bila kuiba wakati anakuona wewe unaishi maisha ya anasa.

Watumishi wengi mno wanaiibia serikali sio pesa tu hata muda wa kuwepo kazini effectively.
 
Acha unoko kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
Natamani sana kuwa upande wake Ila nimeshaamua kuwa upande wa wapigaji. Marekani na ubabe wao bado kuna watu Wana hack mifumo yao. Bahati mbaya dunia ipo hivyo, ni bora kujipanga kuihujumu serikali. If you can't beat your enemies join them. Halafu hela za mtandaoni za kutumia ubongo na akili ni tamu sana asikwambie mtu.
 
Huduma yoyote ya kimtandao (e-service) ina mapungufu makubwa ya uaminifu, kwa sababu kuu kwamba hakuna mawasiliano ya ana kwa ana ya pande mbili (mtoaji na mpokeaji wa huduma). Tatizo lingine ni wizi/ulaghai ambao siyo rahisi kuugundua, km muda wa hewani wa simu kuisha haraka bila mtumiaji kujua.

Kwa sababu hiyo huduma mtandaoni ya Serikali (eGA) haijasalimika na haitasalimika hivi karibuni. Labda swali la kujiuliza kuhusu wizi wa fedha ya Serikali kwa huduma mtandaoni ni kubwa kiasi gani kuliko wakati wa awali (manual-service)? Na, je, TCRA inao uwezo wa kudhibiti udanganifu unaofanyika kwenye huduma mitandaoni?
 
Back
Top Bottom