SoC01 Usimamizi wa haki za Dijiti/Digitali

SoC01 Usimamizi wa haki za Dijiti/Digitali

Stories of Change - 2021 Competition

Poshie

Member
Joined
Jul 18, 2021
Posts
5
Reaction score
1
USIMAMIZI WA HAKI ZA DIJITI/DIGITALI; NINI KIFANYIKE?​

Ni ukweli usiofichika teknolojia imekuza uchumi wa nchi hii kwa kasi mno. Kampuni na watu binafsi hasa wafanyabiashara hutumia ulimwengu wa elektroniki (e-world) kama nyanja yao kuu ya mawasiliano na wateja wao. Katika mawasiliano yao, wafanyabiashara hawa huwa na haki zao za kidijiti ambazo zinatambulika ulimwenguni na hulindwa kwa sheria mbalimbali za nchi husika.

Haki za dijiti ama digitali ni mfumo mzima wa kuzuia utumiaji, utengenezaji au uboreshaji na usambazaji wa kazi zenye hakimiliki kwenye mtandao au ulimwengu wa elektroniki bila ya kibali au ruhusu kutoka kwa wamiliki wa kazi hizo. Katika nchi hii, Tanzania, haki hizi za dijiti hutambulika na hulindwa chini ya sheria yetu ya hakimiliki “Copyrights and Neighbouring Rights Act” iliyofanyiwa maboresho mwaka 2019. Hivyo, kwa kupitia sheria hiyo wamiliki wa hakimiliki kwenye ulimwengu wa digitali hupata haki zao zote; iwe haki za kimaslahi ama haki za kimaadili.

Hata hivyo, ni watanzania wachache sana wenye uwelewa au hata ufahamu juu ya haki hizi za dijiti. Kampuni na wafanyabiashara wa mitandaoni wanapoteza haki zao za msingi za dijiti bila ya wao kujua. Wengine huchochea uvunjifu wa haki hizi wakiamini kwa usambazaji wa kazi zao bila hata ruhusu zao ndiyo wanakua kibiashara bila kujali kwamba kwa kufanya hivyo wanapoteza haki zao na hata mamilioni ya pesa. Mfano wa hali hii unachorwa dhahiri kwa wafanyabiashara wetu wa mtandaoni, unaweza kuta mchoraji anatangaza na kuuza biashara yake kwenye mitandao ya kijamii. Anakuja mfanyabiashara mwingine anachukua picha za mchoraji kutoka ukurasa wa mchoraji na anatangaza katika kurasa yake, mwisho wa siku hupelekea uvunjifu wa haki za mchoraji.

Ni kwa ushauri wangu, mitandao ya kijamii, digitali na ulimwengu wa kijitali uheshimike na haki za wamiliki wa hakimiliki zilindwe kwa namna zinavyotakiwa. Kwa dhumuni ya kufanikisha ushauri huu, COSOTA (chombo cha usimamizi wa hakimiliki) itoe elimu juu ya haki za dijiti kwa washikadau wake na kwa umma kiujumla. Ni vyema pia, serikali izingatie umuhimu wa haki hizi kwani, ni nyanja mojawapo ya kuongeza kipato cha taifa.

Hivyo basi,kuna uhitaji mkubwa wa kuunda mamlaka ya utawala kusimamia haki dijiti za watengeneza programu, waandishi na watumiaji wa dijiti.
 
Upvote 2
Ukisema habari za hati miliki kwa Tanzania , utakosesha ajira watu wengi. Watu zaidi ya 10000 wamejiajiri kupitia kazi ya kuuza CD ambazo ni copyrighted - hiyo ni kwa Dar tu je Tanzania nzima. Kuna watu kama DJ MACK , DJ MURPHY wamekuwa matajiri kwa sababu wa hii kitu. Kuna wale wa vibandani wa nyimbo na movie wakuweke kwenye simu na CD, na wako wengi. Ishu ya hatimiliki itawanufaisha watu ambao wako nje ya nchi , kuliko hata ya waliomo ndani. Na ukipambana na hii kitu utakosesha vijana wengi kazi na usijue pa kuwapeleka
 
Hii ni excuse ambayo imekua ikitumiwa na copyright infringers. Ifike mahala tutambue wrong is wrong hata kama inanufaisha wrongdoers mfano tunaweza kuona kwenye wasanii wetu wa bongomovies wamekua na majina makubwa ila kipato hamna hii ni kwasababu kazi zao ndiyo zinaongoza kuwa infringed. Elimu sahihi ikitolewa juu ya haki za dijiti na kukiwa na usimamizi wa haki hizi naamini miaya ya kuiba kazi za watu itapungua na wamiliki wa kazi wataona matunda ya kazi zao
 
Ubunifu na kutokua na waigizaji wenye vipaji(waimba ngonjera) na watu wenye maono au spirit(Directors, Camera-man,Salesman) - ndo kumeiua sanaa ya bongomovies. Tokea nizaliwe sijawahi kuona kibanda kinacho-burn bongomovies au wauza CD za bongo movies. Kama unamaanisha kuua soko la movies za nje ili uipandishe bongo movies , biashara haiendi hivyo - sana sana utaongeza uhitaji na kumbuka kuna kitu kinaitwa internet huko watu watamalizana bila hata ya kelele
 
kwenye internet ndo kuna hizo haki za dijiti (Digital Rights Management) ukipata wasaa pitia hicho kitu uone wenzetu wanavyonufaika na DRM.
 
Ndo utambue unainfringe haki za watu. Kabla ya kushare hizo movie unatakiwa upate kibali husika ambacho at end of day kitakunufaisha pia kwenye mgao atakaopata huyo mmiliki wa hiyo kazi kutakua na percent yako. Elimu ya hakimiliki na Intellectual Property kwa ujumla bado sana nchini mwetu ndomana wengi wanashindwa kunufaika nayo.
 
Hasara hizo zinaletwa na wezi wa haki zao...bro don't justify wrong kisa wewe unafanya kuna wengine wanaumia out of yo wrongs...periodt
 
Hapa shida sio kuuza CD kibandan bali zinauzwa bila ya mwenyewe kujua na inafanya mwenye kazi yake kutofaidika. Mwandishi nimemuelewa kabla ya kuchukua kaz ya mtu kuwe na mawasiliano kati ya mwenyekazi na huyo mtumiaji.
 
Back
Top Bottom